Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Mimi
Kwa sisi ambao tumetembea sehemu nyingi hii nchi,karibia Kila sehemu kunafanana fanana. Mabadiliko ni machache mno mkoa kwa mkoa. Na mtwara imepazidi sehemu nyingi tu siyo kubaya kihivyo.

Kuna dada yeye ametokea kuoachukia Dodoma vibaya mno. Ukimsikia anavyopaponda Dodoma unaweza sema huko mahali ni kuzimu na wanaoishi huko ni mashetani.
binafsi sipakubali kwasababu ya joto ila somehow pazur msimbati kule beach ipo vzr
 
Tangu nifike Mtwara miezi kadhaa iliyopita, mambo ninayokutana nayo sikuyategemea kabisa. Picha inaanza wakati nakuja kuripoti, ile nafika bus stand ya Mkanaredi naambiwa hapa ndiyo Manispaa ya Mikindani na ndiyo mjini.

Sikuamini! Mr. akanitia moyo na kuniambia nitazoea mazingira. Nikasema, "Sawa, maadam ni mjini, kitu cha msingi ni huduma."


Tukachukua lodge (na lodge zenyewe maji hayatoki, wanategemea maji ya mvua... yani ni tafrani tupu!). To cut a long story short, maisha ya Mtwara ni magumu kwenye nyanja zote! Maji ni shida, bei ya vitu iko juu sana kuliko hata Dar es Salaam, na miundombinu hafifu inafanya usafiri kuwa wa tabu.

Huduma za kifedha ni chache na ziko mbali, yani kulala au kushinda njaa ukiwa na hela mfukoni ni kitu cha kawaida sana hapa!

Ikifika saa 3 usiku, barabarani ni nyeupe kabisa—huoni mtu, na maduka yanafungwa mapema. Viwanja vipo, lakini The Shooters ndicho kiwanja pekee nilichoelewa, na nikiwa hapo najihisi kama niko Dar es Salaam.

Serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa!
Maadam umewakuta wengine wanaishi, nawe uta-adopt tu!
 
Mikoa yote inafanana Tu kama Akili yako umeipanga izoee mazingira utaweza kuishi popote
Unataka uishi kama upo DAR hapo ni kujidanganya, TANZANIA bado Sana hasa Huko mikoani hata hiyo DAR nayo imechoka sanaa sioni utofauti na mikoani tu
Inategemea Dar sehemu gani, kuna sehemu Dar watu wanaishi kama wapo Beverly Hills.
 
Back
Top Bottom