Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Tangu nifike Mtwara miezi kadhaa iliyopita, mambo ninayokutana nayo sikuyategemea kabisa. Picha inaanza wakati nakuja kuripoti, ile nafika bus stand ya Mkanaredi naambiwa hapa ndiyo Manispaa ya Mikindani na ndiyo mjini.

Sikuamini! Mr. akanitia moyo na kuniambia nitazoea mazingira. Nikasema, "Sawa, maadam ni mjini, kitu cha msingi ni huduma."

Tukachukua lodge (na lodge zenyewe maji hayatoki, wanategemea maji ya mvua... yani ni tafrani tupu!). To cut a long story short, maisha ya Mtwara ni magumu kwenye nyanja zote! Maji ni shida, bei ya vitu iko juu sana kuliko hata Dar es Salaam, na miundombinu hafifu inafanya usafiri kuwa wa tabu.

Huduma za kifedha ni chache na ziko mbali, yani kulala au kushinda njaa ukiwa na hela mfukoni ni kitu cha kawaida sana hapa!

Ikifika saa 3 usiku, barabarani ni nyeupe kabisa—huoni mtu, na maduka yanafungwa mapema. Viwanja vipo, lakini The Shooters ndicho kiwanja pekee nilichoelewa, na nikiwa hapo najihisi kama niko Dar es Salaam.

Serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa!
Kwahio umepangiwa mtwara ile interview ya o lever ulitoboa😹😹
 
Mikoa yote inafanana Tu kama Akili yako umeipanga izoee mazingira utaweza kuishi popote
Unataka uishi kama upo DAR hapo ni kujidanganya, TANZANIA bado Sana hasa Huko mikoani hata hiyo DAR nayo imechoka sanaa sioni utofauti na mikoani tu
Mkuu Dar ipo tofauti sana na mikoa yote ya Tanzania Mainland.
Tatizo la Nyamwi255 anataka mkoani apate maisha ya Dar.
Mwanza, Arusha, Unguja, Moshi, Mtwara, Shinyanga, na miji mingi iliyobaki kwa huduma fasta na za kisasa hadi usiku mwingi kote huko hazijafikia kiwango cha Dar.
Dodoma wanajaribu lakini bado kijijini tu.
Dar hadi vichochoroni kabisa nje ya mji (suburbs) usafiri, chakula, duka za dawa, na sehemu za starehe almost zinakesha.
 
Dar ni nyoko biashara 24 hrs watu hawalali hata uamke 9 usiku unapata chochote unachotaka hata bucha la nyama lipo wazi
 
Mikoa yote inafanana Tu kama Akili yako umeipanga izoee mazingira utaweza kuishi popote
Unataka uishi kama upo DAR hapo ni kujidanganya, TANZANIA bado Sana hasa Huko mikoani hata hiyo DAR nayo imechoka sanaa sioni utofauti na mikoani tu
Mkuu Dar ipo tofauti sana na mikoa yote ya Tanzania Mainland.
Tatizo la Nyamwi255 anataka mkoani apate maisha ya Dar.
Mwanza, Arusha, Unguja, Moshi, Mtwara, Shinyanga, na mikoa miji mingi kwa huduma fasta na za kisasa Hadi usiku mwingi kote huko hazijafikia kiwango Cha Dar.
Dodoma wanajaribu lakini bado kijijini tu.
 
Nataka nkiwa mkoani mjini yani manispaa nipate huduma kama za dar (na sio kama nataka ni ndo inavotakiwa)
Kama hapa nipo mjini manispaa kabisa hali iko hivi haya huko kijijini itakuwaje??
Hapo utakuwa umenielewa kama ww ni muelewa.
Viongozi huko wanajua kujenga misikiti tu 90% ya watu wa Mtwara ni watu wa upande ule wa FaizaFoxy na Malaria 2
 
Back
Top Bottom