Nipo tayari kulumbana (Debate) na yeyote kuhusu chochote

Nipo tayari kulumbana (Debate) na yeyote kuhusu chochote

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Kama kichwa cha habari kinavyosema. yeyote yule, anzisha mada yoyote tulianzishe ki mdahalo (debate), wakati wowote.

Karibuni sana. Uwanja wa wazi huu, yeyote anaweza kuchangia na kuingilia mada. Hakuna kanuni rasmi isipokuwa kanuni za JF na za dola ziheshimiwe.
 
FaizaFoxy swala la serikali "kutaka" kumpa mwekezaji kutoka nje Mwendokasi "UDART" mi naona sio sahihi. Wangewapa vipaumbele wafanyabiashara wadogo wadogo wawekeze. Yaani iwe serikali yake ni miundombinu ila magari ya wafanyabishara mbalimbali. Serikali inakua inaobserve "Quality Assurance". Wewe unasemaje?
 
Tafadhali anza kwa kuitambulisha mada unayotaka tuijadili. Mada ni nini hapo?
 
Kama kichwa cha habari kinavyosema. yeyote yule, anzisha mada yoyote tulianzishe, wakati wowote.

Karibuni sana. Uwanja wa wazi huu, yeyote anaweza kuchangia na kuingilia mada. Hakuna kanuni rasmi isipokuwa kanuni za JF na za dola ziheshimiwe.
Uliambiwa ufanye mdahalo na Nyani Ngabu ukakimbia, hapa unatuambia nini tena ndugu, yaani umeshiba futari hapo Daresalama unaanza kutuambia utabishana na yeyote.

Acha hizo, ushakuwa mtu mzima sasa.
 
Nataka kubishana na wewe kuhusu mavazi. Je kujifunika gubigubi na joto la dar kunakupeleka mbinguni?

Wanawake wavae mavazi ya heshima ila tu kujifinika kuanzia nywele na mabaibui kunasababisha harufu mbaya maeneo yote yenye nywele
Hapo unasemaje
 
Mada ni nini hapo?

Watanzania hamuelewi hata namna ya kuanzisha mada?

Anza kwa kuainisha unachotaka tujadili na uainishe wewe upo upande upi katika hiyo mada (pros and cons).
Swali limekuzidi uwezo na hivyo una sweep generally kwamba watanzania hawajui kuanzisha mada? Bila shaka huko shule ulienda kuzagamua ujinga
 
MADA: CHANGAMOTO YA WANAWAKE KUKOSA KUJIAMINI.
Wanawake tumekua na changamoto ya uoga na kutojiamini ni kitu kama nature...
Kwenye masuala ya muhimu katika jamii
Mfano hapa jf mada karibia zote za muhimu zinazofundisha, zinazoishi kila siku zimeanzishwa na wanaume

Siamini kama wanawake wa humu hatuna mada za madini za kuanzisha kuleta manufaa kwa wengine.

Nini kifanyike kuondokana na changamoto hii katika jamii japo hapa nimetolea mfano kwa wanawake wa jf lakini hili tatizo lipo katika jamii yote.

Tufanye nini kutatua au tuache kama ilivyo liwe suala la nature na tukubaliane nalo?
 
Wanawake tumekua na changamoto ya uoga na kutojiamini ni kitu kama nature...
Kwenye masuala ya muhimu katika jamii
Mfano hapa jf mada karibia zote za muhimu zinazofundisha, zinazoishi kila siku zimeanzishwa na wanaume

Siamini kama wanawake wa humu hatuna mada za madini za kuanzisha kuleta manufaa kwa wengine.

Nini kifanyike kuondokana na changamoto hii katika jamii japo hapa nimetolea mfano kwa wanawake wa jf
Au tuache kama ilivyo liwe suala la nature na tukubaliane nalo?

Mada ni nini, wanawake au wanawake wa JF au kujiamini na kutojiamini kwa wanawake?
 
Back
Top Bottom