Nipo tayari kutoa milioni 5 kwa mtu atakayenionyesha hili andiko

Malpighian

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2015
Posts
232
Reaction score
305
Habari Wakuu.

Nimekuwa nikifuatilia mafundisho mbalimbali katika makanisa kuhusu somo la Ubatizo (Baptize), kwa sehemu kubwa kila inaonekana kila kanisa Lina namna yake ya uelewa juu ya ubatizo.

Hoja yangu ni hii, Kama dini ya kikristo muongozo wake ni Biblia. Nipo tayari kutoa kiasi cha Tsh milioni 5 kwa atakaye nionyesha ni wanafunzi gani au watu gani katika biblia waliowahi kubatizwa kwa Jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu.
 
unakuja kusumbua watu humu,hujui chatgpt ni Nini?
hiyo 5 M kaanzishe kijiwe Cha games za watoto utatoboa
 
Mathayo 28:19

[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

Go ye therefore, and teach all nations, baptizing them in the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Ghost:
 
Wapi katika Biblia tunaweza kuona wanafunzi au watu waliobatizwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kama ilivyoandikwa katika Mathayo 28:19?

Sasa tuchambue kwa ushahidi wa maandiko:

1. Amri ya Yesu mwenyewe – Mathayo 28:19
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.”

Hapa Yesu mwenyewe anatoa agizo kwa mitume wake kabla ya kupaa mbinguni. Hii ndiyo amri kuu ya ubatizo, na inatajwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

2. Utekelezaji wa agizo – Matendo ya Mitume
Watu wengi walibatizwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, lakini kwa jina la Yesu Kristo:
a) Matendo 2:38 – Siku ya Pentekoste
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo…”

b) Matendo 8:16– Watu wa Samaria
“…kwa maana alikuwa hajamshukia hata mmoja wao ila walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.”

c) Matendo 10:48 – Kornelio na watu wake

“Akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo.”

d) Matendo 19:5– Wanafunzi wa Yohana
“Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.”

Hoja ya Kulinganisha:

Ingawaje agizo lilikuwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, utekelezaji wake katika matendo ya mitume wote waliobatiza walitumia jina la Yesu Kristo. Hii imeibua mijadala ya kiteolojia juu ya kama “jina” hilo linawakilisha utimilifu wa Baba (Mungu), Mwana (Yesu), na Roho Mtakatifu ndani ya utambulisho wa Yesu Kristo.

Mwisho kwa Ushahidi:
  • Hakuna maandiko katika Biblia yanayoeleza moja kwa moja kwamba mtu alibatizwa kwa kutajwa maneno “kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu” wakati wa tendo la ubatizo.
  • Hata hivyo, maandiko yako wazi kwamba agizo lilitolewa na Yesu mwenyewe kwa maneno hayo (Mathayo 28:19), lakini mitume walibatiza kwa jina la Yesu Kristo, wakiamini kuwa ndilo jina lililobeba mamlaka ya Utatu mtakatifu.
Ushauri wa Kiutafiti:
Tafsiri ya “jina” katika Mathayo 28:19 kama “Yesu” inatokana na fundisho la kuwa Yesu ndiye utimilifu wa Mungu katika mwili (Kol 2:9). Ndiyo maana ubatizo kwa jina la Yesu Kristo unaonekana kuwa ni utekelezaji wa ile amri ya Mathayo 28:19.

Niwekee mil 5 sasa na Ubarikiwe !
 
Habari Wakuu.

Nimekuwa nikifuatilia mafundisho mbalimbali katika makanisa kuhusu somo la Ubatizo (Baptize), kwa sehemu kubwa kila inaonekana kila kanisa Lina namna yake ya uelewa juu ya ubatizo.

Hoja yangu ni hii, Kama dini ya kikristo muongozo wake ni Biblia. Nipo tayari kutoa kiasi cha Tsh milioni 5 kwa atakaye nionyesha ni wanafunzi gani au watu gani katika biblia waliowahi kubatizwa kwa Jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu.

kwanza kabisa, lazima tujue ubatizo ni Agizo la Bwana Yesu mwenyewe

“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;"
— Mathayo 28:19 (Biblia Takatifu)
pili: baada ya kanisa kuanza (Matendo ya Mitume 2) Mitume walitekeleza Agizo hiilo la Bwana YESU kwa kuwabatiza waliomwamini Yesu kwa "Jina la Yesu Kristo."
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu."
— Matendo ya Mitume 2:38 (Biblia Takatifu)

kubatizwa kwa Jina la Yesu ni sawa na kubatizwa kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu kwa sababu Jina la Yesu ni utimilifu wa Uungu wote. Kuna tofauti ya jina la Yesu kabla ya kufa na kufufuka na baada ya kufa na kufufuka kwake.
Wakolosai 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁸ Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
¹⁹ Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;
²⁰ na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.

Wakolosai 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁹ Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.
¹⁰ Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka.
 
Wapi katika Biblia tunaweza kuona wanafunzi au watu waliobatizwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kama ilivyoandikwa katika Mathayo 28:19?

Sasa tuchambue kwa ushahidi wa maandiko:

1. Amri ya Yesu mwenyewe – Mathayo 28:19
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.”

Hapa Yesu mwenyewe anatoa agizo kwa mitume wake kabla ya kupaa mbinguni. Hii ndiyo amri kuu ya ubatizo, na inatajwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

2. Utekelezaji wa agizo – Matendo ya Mitume
Watu wengi walibatizwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, lakini kwa jina la Yesu Kristo:
a) Matendo 2:38 – Siku ya Pentekoste
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo…”

b) Matendo 8:16– Watu wa Samaria
“…kwa maana alikuwa hajamshukia hata mmoja wao ila walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.”

c) Matendo 10:48 – Kornelio na watu wake

“Akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo.”

d) Matendo 19:5– Wanafunzi wa Yohana
“Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.”

Hoja ya Kulinganisha:

Ingawaje agizo lilikuwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, utekelezaji wake katika matendo ya mitume wote waliobatiza walitumia jina la Yesu Kristo. Hii imeibua mijadala ya kiteolojia juu ya kama “jina” hilo linawakilisha utimilifu wa Baba (Mungu), Mwana (Yesu), na Roho Mtakatifu ndani ya utambulisho wa Yesu Kristo.

Mwisho kwa Ushahidi:
  • Hakuna maandiko katika Biblia yanayoeleza moja kwa moja kwamba mtu alibatizwa kwa kutajwa maneno “kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu” wakati wa tendo la ubatizo.
  • Hata hivyo, maandiko yako wazi kwamba agizo lilitolewa na Yesu mwenyewe kwa maneno hayo (Mathayo 28:19), lakini mitume walibatiza kwa jina la Yesu Kristo, wakiamini kuwa ndilo jina lililobeba mamlaka ya Utatu mtakatifu.
Ushauri wa Kiutafiti:
Tafsiri ya “jina” katika Mathayo 28:19 kama “Yesu” inatokana na fundisho la kuwa Yesu ndiye utimilifu wa Mungu katika mwili (Kol 2:9). Ndiyo maana ubatizo kwa jina la Yesu Kristo unaonekana kuwa ni utekelezaji wa ile amri ya Mathayo 28:19.

Niwekee mil 5 sasa na Ubarikiwe !
Hela yenyewe ya kununua bundle tu tunaipata kwa mbinde, ndiyo iwe hiyo milioni tano?🤣
 
Mathayo 28:19

[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

Go ye therefore, and teach all nations, baptizing them in the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Ghost:
Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Kwa sababu hii, nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati.”

NB: Ubatizo huu ufuatane na mafundisho. Kama alivyosema ktk neno lake.
 
Back
Top Bottom