Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Hata na mimi nashukuru nilizaliwa familiya ilokuwa na uwezo wa kilisha mtaa mzima so ishu ya vyakula nyumbani ni tangu tukiwa wadogo.
Nakumbuka tukiwa wadogo baba akiwa hai, kwanza akitoka safari anachinja ng'ombe kijiji kizima wakija kumsalimia wanakula na nyama wanabeba.
Akitoka safari chakula kinapikwa kuanzia asubuhi hadi jioni yaani kila anekuja kumsalimia baba lazima ale.
Maisha ya mama baba akiwa hai ni full time jikoni na wafanyakazi wawili
Nyumbani wageni ni full time na wengine wanalala mpaka baba akisafiri tena ndo mama anapumzika.
wabibi, baba akifika kila jion wanafata mafuta ya taa na sukali hao wote lazima waondoke wamekula, chakula kikiisha lazima mama apike kingine hata kama ni usiku.

Nyumba yenye chakula cha kutosha haikosi wageni na wafanyakazi wa kutosha. Kwetu kulikuwa kama sherehe most of the times.

Siku baba yangu amefariki watu wazee kwa vijana walilia sana. Msiba ulimaliza zaidi ya mwezi na zilichinjwa ngombe zaidi ya 10 sikumbuki idadi maana tulikwa nazo kama 300 hivi.
Kama una uwezo lisha watu washibe ili ukifa tupate na machozi ya kukulilia.

Msibani kwa baba watu walikuwa wanalia hivi:,
Wazuri hawadumu, tulikula bure, nyama tulipewa bure, sukari bure mafuta bureee, wewe mtoto nini kimekupata? Wanapiga geneza wamama, amkaaaaa sisi tunakula wapi? Amkaaa watoto wetu wanalipiwa na ada na nani? fulani amkaaaaaaa. Loh nimekumbuka mbali.
Hata katika biblia Dorcas alililiwa sana na Yatima na wajane. Ndio hivyo vizuri havidumu sana.

RIP mzee.
 
Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Aaaah watu wapikiwe wale washibe haswa mambo mengine sio bajeti ni uchoyo
 
Kuna siku nilikuwa na wageni Fulani watasha sehemu Fulani, wao wanakula Kidogo sana, Mimi nikamsoma dereva maana mswahili mwenzangu, yeye anajifanya anazuga alafu anaaga anaenda kufata vocha aloo Kumbe anaenda kwenye mgahawa wa karibu na kupiga mapigo ya kibongo. Niliunga tela fasta siku inayofata nikamwambia na Mimi nataka nitume M-pesa sehemu akaniambia njiani asee Mimi huwa sishibi hiyo misosi nikamwambia sio peke yako, alicheka sana. Nikaagiza ugali sahani mbili chap, dereva alicheka sana. Hii ndio mipango. [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1] [emoji2] [emoji1]
 
Ila ugenini kunaweza kukufanya usiwe na raha kuna sehemu nilifikia kabla ya kulala usiku wanaka ibada wanakusanyika sebuleni wakiamka ahsubuhi saa 12 kaibada nami sijazoea hiyo michongo
Wewe si evilspirit..

Kidding
 
Hiki kisa kimenikumbusha miaka flani ya 2012 nilimtembelea braza Dodoma nilkua napita tu nikaona kwa kua n broza dam dam na miaka ming hatujaonana basi wacha nikite kambi walau kwa siku moja

Sasa kumbe maisha ya bro yamebadilika sana chakula hali tena kama zamani wametenga ka chakula (wali) kwenye ile hot pot ndogo ni kama walipika nusu kilo hivi basi na vipande vya kuku maharagwe kidogo na mboga za majani hahahaha

Ngoja nicheke kidogo[emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji1787] kumbe ndio chakula cha kula familia nzima (bro , mke wake, house girl na mtoto mmoja wa kama miaka sita hvi na mimi mgeni wao) basi wakanikaribisha huku wakinisisitiza nikapakue

Basi mzee nikainuka kwenda mezani nilivoona ule msosi akili ikaniambia kwa jinsi hiki chakula kilivyo kidogo itakua ni changu peke yangu nilipakua ule wali zaid ya robo tatu tia mboga ya majani na maharage na vipande kama vitatu vya kuku

Sasa baada ya dakika chache huku naendelea kuchakata nawaona na wao wanakuja mezani

Ilibidi niulize kwani na nyie ndio mnakula hiki hiki huku nikiwa na mshangao na taharuki ya hali ya juu ikabidi wajichekeshe chekeshe pale house girl akaingia jikon kupika ugali

Kesho yake niliamsha bila hata kupata breakfast maana siwezi kukaa nyumba yenye njaa mimi
[emoji3][emoji3]housegirl akaingia jikoni mida mibovu kurusha ugali
 
Hapo wanakufukuza kijanja.. Hawataki kukuona na inawezekana unalala sebuleni au nawatoto..
Usikute wala sio swala la kutaka kumfukuza ila ndo maisha yao,usiforce mfanane wala usitake kuwapa kazi wao kukufanyia interview kujua ulaji wako ukoje ila ni jukum lako kuswitch na mtindo wao wa maisha kwa muda utakaoishi nao
Mimi siamini kwmb Dsm watu wanakula kidg sijakutana na iyo experience kabsa kwa ndugu zangu wa Dsm,misosi ni shaziiii
 
Uwe unakula huko mtaani ukirudi unalala tu mbona rahisi sana
Au siku moja nunua chakula hapo pika kingi uone kama hawatakula msosi mwingi na wao
Hili nalo la msingi,siku moja omba kuingia jikoni tena shopping ya ivyo vyakula ifanye mwenyewe usiguse vilivyoko ndani afu pika vya kutosha tia mezani kuwa wakwanza kula tena wakiwepo wote,tia ujazo wa kutosha mtoto haruki [emoji23][emoji23] uwasikilizie zamu yao au unasepa unaachana nao utarud badae kuona walichobakisha
 
Mimi hadi leo huwa namtania mama kuwa kama asingeishi maisha ya kulisha watu sasa amezeeka angekuwa hata na nyumba 4. Yeye huwa anacheka na kusema kila mtu amekuja duniani kwa purpose fulani, Anyways.

Aisee kwetu kulikuwa na watu!!!! Sijui walikuwa wanatoka wapi wale watu, unakuta mtu na mdogo wake wote wapo kwetu... Ila chakushangaza msosi haukuwa kipengele. Mama alikuwa ninja sana, now naelewa ile menu plan yake, lengo ilikuwa watu wale washibe.
Asubuhi saa 1 uji na popcorn viko tayari.

Saa 4 vinapikwa viazi, mihogo na maandazi yakutosha na chai.

Saa nane ugali maharage,nyama na mboga majani. Au ugali, utumbo, mboga za majani na maharage, au ugali, maini, majani na maharage.

Usiku makande +wali na maharage/dengu/kunde/choroko na mboga za majani. Mchicha+chinese na ndizi mbivu au parachichi.

Juice za ukwaju na ubuyu, kipindi cha maembe ndio mnapata juice ya embe. inatengenezwa magaloni na magaloni yanajazwa kwa friza kama yote.

Vyakula vilikuwa havipishani muda sana, Watu wanajikuta bado wameshiba hawali sana.

Mchele ulikuwa unaletwa kutoka igunga magunia hata mawili, mahindi, maharage, mafuta ya alizeti na vitunguu vilikuwa vinaletwa kutoka kijijini kwetu, huko mzee mama alikuwa na mashamba kama heka 70 hivi... na kuna vijana wanakaa kwake (kijijini) wanalima, hadi wanavuna, na wenyewe wanachukua vyakula humo humo, vingine vinakuja mjini, vingine vinauzwa.

Anyways.. kwa maana ya chakula cha kujaza tumbo, kilikuwepo chakusaza kuhusu balance diet hapo ndio sina uhakika. Na sababu watu walikuwa wengi, hata watu wakupika na kuosha vyombo walikuwa wengi, unakuta wadada wa umri wa usichana wako wa5 au 6.
MAma alikua mtu poa sana
 
Back
Top Bottom