Mimi hadi leo huwa namtania mama kuwa kama asingeishi maisha ya kulisha watu sasa amezeeka angekuwa hata na nyumba 4. Yeye huwa anacheka na kusema kila mtu amekuja duniani kwa purpose fulani, Anyways.
Aisee kwetu kulikuwa na watu!!!! Sijui walikuwa wanatoka wapi wale watu, unakuta mtu na mdogo wake wote wapo kwetu... Ila chakushangaza msosi haukuwa kipengele. Mama alikuwa ninja sana, now naelewa ile menu plan yake, lengo ilikuwa watu wale washibe.
Asubuhi saa 1 uji na popcorn viko tayari.
Saa 4 vinapikwa viazi, mihogo na maandazi yakutosha na chai.
Saa nane ugali maharage,nyama na mboga majani. Au ugali, utumbo, mboga za majani na maharage, au ugali, maini, majani na maharage.
Usiku makande +wali na maharage/dengu/kunde/choroko na mboga za majani. Mchicha+chinese na ndizi mbivu au parachichi.
Juice za ukwaju na ubuyu, kipindi cha maembe ndio mnapata juice ya embe. inatengenezwa magaloni na magaloni yanajazwa kwa friza kama yote.
Vyakula vilikuwa havipishani muda sana, Watu wanajikuta bado wameshiba hawali sana.
Mchele ulikuwa unaletwa kutoka igunga magunia hata mawili, mahindi, maharage, mafuta ya alizeti na vitunguu vilikuwa vinaletwa kutoka kijijini kwetu, huko mzee mama alikuwa na mashamba kama heka 70 hivi... na kuna vijana wanakaa kwake (kijijini) wanalima, hadi wanavuna, na wenyewe wanachukua vyakula humo humo, vingine vinakuja mjini, vingine vinauzwa.
Anyways.. kwa maana ya chakula cha kujaza tumbo, kilikuwepo chakusaza kuhusu balance diet hapo ndio sina uhakika. Na sababu watu walikuwa wengi, hata watu wakupika na kuosha vyombo walikuwa wengi, unakuta wadada wa umri wa usichana wako wa5 au 6.