Jamani poleni na majukum,kiukweli mshahara haunitoshi kabisaaaaaaa,natamani nifanye biashara lakini sijui ni ipi,nina kamtaji ka sh m5,nahitaji ushauri wenu,Mungu awabariki sana
kwa ushauri wangu tafuta frame maeneo yenye biashara kama k/koo but frame za bei rahisi na zinapatikana kwenye nyumba za kizamani then unaweza kufungua biashara zifuatazo.
1. barbershop
- matengenezo ya frame pamoja na vifaa vyake yanaweza kugharimu 1.5 - 3.5ml including aluminium door, viti, mashine, nk
- kila kiti kimoja yule kinyozi anakulipa kati ya 6000 - 10000 kwa siku kutegemea na makubaliano yenu. na kwa kawaida idadi ya viti huanzia 3 mpaka 5 include kimoja cha mwanamke kwa ajili ya sijui facial, scrubbing na upuuzi kama huo. so iwapo umeweka viti 4 ina maana kwa siku unapokea minimum tsh 24,000 na maximum ni 40,000. ambapo kwa mwezi utakuwa na kitu kama 720,000/- hadi 1,200,000 mbapo ndani ya miezi 8 utakuwa usharudisha mtaji wako na unaanza kula faida.
- mwanzo unawawekea kila kitu cha kuanzia, kuanzia umeme, mashine, powder, mafuta, maji nk nk but vikiisha au kuharibika ni jukumu LAO kuongeza au kutengeneza.
- unaweza kupitia pesa yako kila siku, ima kila wiki, au kila mwezi depends on your agreement. na wanamchagua kiongozi wao mmoja ambaye wewe ndo utakuwa unadeal na huyo tu.
- pia kuna wengine huwa wanapokea pesa ya mwezi mzima kutoka kwa kinyozi kabla ya kumkabidhi kiti na mashine but hii kidogo inahitaji huyo kinyozi mwenyewe awe na uwezo na awe tayari kukabiliana na chohcote like kukatika kwa umeme nk.
nina biashara nyingi zaidi ya 50 (ninazo kichwani but sio kama tayari nazirun) na ningependa kukupa zote ila ni mvivu wa kutype so utansamehe my dia.