Nisaidieni: 5mil Kuanzia biashara

Nisaidieni: 5mil Kuanzia biashara

Nipo nyanda za juu kusini Pearl,biashara inayolipa ni mazao kuna mpunga,ulezi,mahindi,maharage n.k. Unachoweza kufanya: m5 kwa mazao ni kiasi cha kutosha kuanzia. Unaweza kununua mzigo vijijini kwa bei ya chini na kuleta mjini kuuza kwa bei ya juu na kurudi tena kijijini au unaweza kununua mzigo kijijini/mjini na kuweka stoo na kuuza baada ya bei kupanda,hii inahitaji mtaji zaidi ili utakapofika msimu wa kuuza upate faida nzuri. Pia zingatia muda ulionao,je unakuruhusu kusafiri mara kwa mara? Msimu mzuri wa biashara hizi ni kati ya mwezi wa 4 mwishoni hadi mwezi wa 12. Kwa mzigo uliopo stoo muda mzuri wa kuuza ni kati ya mwezi wa 12 hadi 03.
 
hiyo ni wazo zuri sana - tatizo pearl ataweza kusafiri hadi huko na kukusanya mzigo?
 
Ungekuwa mkaka ningekwambia jaribu kununua misitu midogo ya miti ya mbao na kupasua mwenyewe. misitu midogo inaweza kupatikana kuanzia Tsh 500,000/ kwa shamba/kitalu cha miti 600.

Mashamba haya yapo vijijini ambako unahitaji kuwa jasiri kiasi,lakini faida ya biashara hii ni kubwa sana na inakuwa kwa speed nzuri.

Sasa kwa sababu jina lako linaonekana wewe ni mdada,inakuwa ngumu kidogo vinginevyo uniambie wewe ni mdada wa shoka. 5M uliyosema inatosha kwa kuanzia.

Sorry malila hizo bei ni za wapi? Na je issue za vibali vya kusafirisg=ha hizo mbao vinapatikanaje? thanx!
 
Pearl, hizo t-shirt na shirts wauzia'pi? Una oulet yako ama nazo wampelekea mteja huko huko alipo. Naweza kukuungisha eneo hili kama una mzigo wa ukweli na sio zile za "ki Hu Ji Ntao".
 
hiyo ni wazo zuri sana - tatizo pearl ataweza kusafiri hadi huko na kukusanya mzigo?

....yote yanawezekana ELNINO,suala la msingi ni kuwa na
nia na malengo. Mtaji naona anao wa kutosha kuanzia.
 
Ninachoweza kukushauri, kwa mtaji wa Million 5 ni bora uka-invest kwa kununua hisa pale dar stock exchange.

kwa sasa hivi naamini share za twiga cement au /na simba sio mbaya kwa sababu shughuli za ujenzi nchini zimeshika kasi hivyo bidhaa zao, yaani cement, zina soko.
hata hivyo masuala ya mgao wa umeme yanaweza kuathiri faida yao.

kwa ushauri zaidi waone wataalamu. haya ni mawazo tu na uamuzi wa kuwekeza katika makampuni yaliyotajwa hapo juu ni wako peke yako.
 
Usiogope kufanya ujasiliamali kwa kuogopa kupata hasara - stock exchange kwa mtaji wako wa shiling 5m is wasting, hutapata mafanikio kwa muda muafaka labda kama unamwekea mwanao.

Faida ya miradi yako ndiyo unaweka kununua hisa badala ya kuweka benki - lakini hiyo 5m ni mtaji na si pesa ya kununua hisa pearl.
 
Sorry malila hizo bei ni za wapi? Na je issue za vibali vya kusafirisg=ha hizo mbao vinapatikanaje? thanx!

Hizo bei ni za mashambani huko Iringa. Hakuna vibali kwa misitu ya miti ya kupandwa.
 
Mambo yako yameishia wapi umepata ushauri gani na umefuata upi? nipe maendeleo.
 
Mambo yako yameishia wapi umepata ushauri gani na umefuata upi? nipe maendeleo.

kumekuwa na kimya kingi sana...jamani tupeni matokeo ni biashara gani ilikubalika...wengi tulikuwa tunafuatilia ushauri
 
Mi naona mtaji huu ushaliwa - 5m tangu asiseme zinahitajika kuwa invested, bado zipo tu? lol
 
kazi kweli kweli...kwa hiyo biashara ya mtaji wa mil5 hakuna
 
wa kwetu mpaka mgomo umesitishwa ndo umejitokeza?

wacha tu wakwetu naona tunakoelekea siko, nataka nijiunge na Pearl kwenye ujasiriamali...nimeamua kufuata ushauri wa mkulu wa kama sitaki niache kazi...nimeamua kuwa mbayuwayu
 
wacha tu wakwetu naona tunakoelekea siko, nataka nijiunge na Pearl kwenye ujasiriamali...nimeamua kufuata ushauri wa mkulu wa kama sitaki niache kazi...nimeamua kuwa mbayuwayu

bora, lakini utanyonywa tu kwenye kodi/ushuru!!!

eventually u will fill the pinch!! mi nimebuku kifrem pale kilombero na kila siku ya mnada mbauda, oldonyo n the like ntapeleka biashara yangu. wacha nijaribu hiyo.
 
hiyo ni afadhali, mimi nimeamua kuchukua vitunguu huku yaeda na mang'ola najua nitatoka...kama ukisikia mtu anataka maonion unishtue
 
Jamani poleni na majukum,kiukweli mshahara haunitoshi kabisaaaaaaa,natamani nifanye biashara lakini sijui ni ipi,nina kamtaji ka sh m5,nahitaji ushauri wenu,Mungu awabariki sana

kwa ushauri wangu tafuta frame maeneo yenye biashara kama k/koo but frame za bei rahisi na zinapatikana kwenye nyumba za kizamani then unaweza kufungua biashara zifuatazo.

1. barbershop
- matengenezo ya frame pamoja na vifaa vyake yanaweza kugharimu 1.5 - 3.5ml including aluminium door, viti, mashine, nk
- kila kiti kimoja yule kinyozi anakulipa kati ya 6000 - 10000 kwa siku kutegemea na makubaliano yenu. na kwa kawaida idadi ya viti huanzia 3 mpaka 5 include kimoja cha mwanamke kwa ajili ya sijui facial, scrubbing na upuuzi kama huo. so iwapo umeweka viti 4 ina maana kwa siku unapokea minimum tsh 24,000 na maximum ni 40,000. ambapo kwa mwezi utakuwa na kitu kama 720,000/- hadi 1,200,000 mbapo ndani ya miezi 8 utakuwa usharudisha mtaji wako na unaanza kula faida.
- mwanzo unawawekea kila kitu cha kuanzia, kuanzia umeme, mashine, powder, mafuta, maji nk nk but vikiisha au kuharibika ni jukumu LAO kuongeza au kutengeneza.
- unaweza kupitia pesa yako kila siku, ima kila wiki, au kila mwezi depends on your agreement. na wanamchagua kiongozi wao mmoja ambaye wewe ndo utakuwa unadeal na huyo tu.
- pia kuna wengine huwa wanapokea pesa ya mwezi mzima kutoka kwa kinyozi kabla ya kumkabidhi kiti na mashine but hii kidogo inahitaji huyo kinyozi mwenyewe awe na uwezo na awe tayari kukabiliana na chohcote like kukatika kwa umeme nk.

nina biashara nyingi zaidi ya 50 (ninazo kichwani but sio kama tayari nazirun) na ningependa kukupa zote ila ni mvivu wa kutype so utansamehe my dia.
 
Back
Top Bottom