Nisaidieni: 5mil Kuanzia biashara

Nisaidieni: 5mil Kuanzia biashara

tatizo ni mda dia
Peal, pole sana na mshahara mdogo najua utakuwa kwenye take home ya six digits, nakushauri ufuge kuku wa mayai - pesa uliyonayo inatosha sana kwa kuanzia
hakuna biashara yeyote utafanya zaidi ya hiyo niliyokuambia - inalipa sana na after 5 years utakuwa mbali sana.

kwa hiyo 5m uliyonayo unaweza kuanza na kuku 500 then as you go on utaongeza
 
biashara ziko nyingi ila kuna moja ninataka nikushauri ila inahitaji tuwasiliane au ikiwezekana tuonane ana kwa ana, hapa hakuna utani ni serious, ukiweza nicheki kwa 0762 223 662, kwa kuanza utatakiwa uanze na m2 tatu unaweka pembeni

karibu

Andika hiyo biashara yako ili hata wana JF wengine wakiipenda wakutafute, si pearl pele yake watu kibao wana shida hizo.
 
My dia,zamani nilikuwa nafuga mwenyewe but nowdays naona gharama zinakuwa kubwa pia mm niko kazini vijana wanasumbua wat i do nowdays,nachukua oder kwa wiki jmosi nasafiri vijijini kwenda kuchukua mzigo ,jpili nachinja na kupaki kwenye mifuko,jtatu nawapelekea wateja kabla ya kuja kazini

Hapo kazi kuna kitu kinafanyika kweli au project planning ya next week? Kama unamudu hayo yote na kazi za boss zinakwenda basi wewe ni kichwa. Unatakiwa kutupa ushauri (wengi wetu) wa jinsi ya kuwa mjasiriamali badala sisi kukushauri.
 
Andika hiyo biashara yako ili hata wana JF wengine wakiipenda wakutafute, si pearl pele yake watu kibao wana shida hizo.

Kweli E, watu watupatie uzoefu wao kwani hapa tunaweza kuwa tunasoma ushauri hewa. Kuna watu ambao hawajawahi hata kuuza karanga au maji kwenye stesheni za reli, lakini hapa watamwaga mipointi ya nguvu kumbe ni njonzi tu! Ni kama mchezo wa kumshauri mkulima jinsi ya kuzalisha mazao bora wakati huna hata bustani ya mchicha!
 
my dia kila kitu ni mipango tu,lazima ufanye kazi kama mtumwa ili uishi kama mfalme,thast how I do alwys,kama nikiwa tite sanaa,kule vijijini wanajiua so nawaambia wanichagulie vzr then wanatuma kwenye basi naenda kuwapokea,hayo ndo maisha yangu nafurahi kuwa mtoto wa mkulima tena maskini,lkn naupinga umaskini na Mungu ananiwezesha yote hayo.
Hapo kazi kuna kitu kinafanyika kweli au project planning ya next week? Kama unamudu hayo yote na kazi za boss zinakwenda basi wewe ni kichwa. Unatakiwa kutupa ushauri (wengi wetu) wa jinsi ya kuwa mjasiriamali badala sisi kukushauri.
 
siwezi kufanya hivyo as long as Mungu kanipa Miguu na Mikono nitafanya kazi tu kwa njia halali,ukiskia wateja wa hivyo niuzavyo plz niambie kuku wa kienjeji wkubwa sana tu ninao wengi

Nakushauri upanue zaidi biashara yako ya kuku wa kienyeji. Njia mojawapo ni kuanzisha utaratibu wa kuwauzia watu siku za Jumapili na Ijumaa katika misikiti na makanisa. Pia angalia suala la bei. Lengo kuu liwe ni kupata faida kiasi fulani kwa wiki au mwezi. Hii maana yake ni kuwa usiweke bei ya juu sana kwa kuku mmoja ili ikusaidie kuuza kuku wengi katika wiki moja au mwezi mmoja. Pia angalia uwezekano wa kuwauza hao kuku wako katika jiji la Nairobi. Kama una mtu huko muombe akufanyie utafiti huko.

Biashara nyingine nzuri kwa huo mtaji wako na kununua nyanya mikoani (km Arusha, Tanga Iringa etc) na kisha kuja kuziuza kwa bei ya jumla katika masoko ya hapa Dar.
 
Biashara nyingine nzuri kwa huo mtaji wako na kununua nyanya mikoani (km Arusha, Tanga Iringa etc) na kisha kuja kuziuza kwa bei ya jumla katika masoko ya hapa Dar.

Hii inaitwa malimbichi; simshauri kabisa aingie huku ikiwa soko lake kuu ni hayo masoko uliyotaja; badala yake atafute wanunuzi wa jumla kwenye masoko mengine makubwa na ya kati kwa kuwa kweny haya masoko makuu kuna mchezo wa bidhaa kufungana na maranyingi hii ni wakati wa msimu. Na pia wakati mwingine ni biashara inayotaka ufuatiliaji wa karibu kama unategemea kuuza sokoni wewew mwenyewe
 
Nakushauri ufuge kuku wa kienyeji watakutoa unaweza kuanza na vifaranga 300 kama uko serious ndani ya miezi 6 utakuwa unazungumza lugha nyingine. Unachohitajika kuwa nacho ni kuwa na eneo lisilokuwa chini ya eka 1. Kwa ushauri zaidi jinsi unavyoweza kufuga na wapi utapata vifaranga na kuku uwafuge vipi nipigie simu namba 0755394701. Pia nakushauri utafute kitabu changu- Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri kinaelezea ni jinsi gani unaweza kujitoa katika umasikini kwa kuanzisha biashara, pia kina mifano hai (case studies) 20 ya biashara ambazo unaweza kuchagua mmoja wapo utakaokufaa.
CHARLES NAZI
Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara.
 
Ninachoweza kukushauri, kwa mtaji wa Million 5 ni bora uka-invest kwa kununua hisa pale dar stock exchange.
 
Ninachoweza kukushauri, kwa mtaji wa Million 5 ni bora uka-invest kwa kununua hisa pale dar stock exchange.

Mkuu ungemwambia share za kampuni fulani ambayo unajua inafanya vizuri ingekuwa poa, je akinunua hisa za Tol au Nicol itakuwaje?
 
Mi niko ktk biashara kwa zaidi ya miaka 20. 5ml ni nyingi sana pia ni kidogo sana ktk kuanzisha biashara.Hivyo basi MOSI KUWA MAKINI ZAIDI UNAPOFIKIRIA KUHUSU AINA YA BIASHARA, angaria vema khs soko, upatikanaji wa bidhaa au huduma.Muda unaotumia.Risk zilizo katka biashara ni nyingi kuliko faida hivyo kuwa makini sana.
Ila na shauri pindi utakapo amua biashara yakufanya please usitumie mtaji wako wote bali unaweza kuanzia na 2.5ml au 3ml then unaangalia maendeleo yake .Elewa kuwa mazingira ya biashara ni ya ushindani mkubwa sn, pia kuna tatizo la UAMINIFU hasa kwa Wafanyakazi nk.
Nimekupatia dondoo kidogo tu ila elewa kuwa kila Biashara inalipa tu inategemea na jinsi ulivyo jipanga, lakini vema ukaanza kidogo kidogo Usipende kuangalia Faida kubwa tu, KM UNAFIKIRIA FAIDA FIKIRIA KUHUSU HASARA PIA.LAKINI USIOGOPE KUFANYA MAAMUZI. LAKINI YAKUPASA KUFIKIRIA VEMA.maana kupoteza 5ml ni Rahisi sana LAKINI KUITAFUTA NI VIGUMU SANA.
 
thx Mungu akubariki sana

Malila umenikumbusha TOL ; Mungu wangu hata cjui hatima ya hisa zangu 500 nianznie wapi kuwafuatilia?
 
Check this out,buying and selling dollars,public transport(hiace), or even a bajaji,with that money you can have two reconditioned bajaji from which you can make a small fortune for yourself if you manage its revenues well ofcourse.Will check some more and keep you posted
"Always resources are scarce,learn how to use effectively and efficiently what you have regardless of its size or amount"
 
thx juniour will do that

Ungekuwa mkaka ningekwambia jaribu kununua misitu midogo ya miti ya mbao na kupasua mwenyewe. misitu midogo inaweza kupatikana kuanzia Tsh 500,000/ kwa shamba/kitalu cha miti 600.

Mashamba haya yapo vijijini ambako unahitaji kuwa jasiri kiasi,lakini faida ya biashara hii ni kubwa sana na inakuwa kwa speed nzuri.

Sasa kwa sababu jina lako linaonekana wewe ni mdada,inakuwa ngumu kidogo vinginevyo uniambie wewe ni mdada wa shoka. 5M uliyosema inatosha kwa kuanzia.
 
Vipi peal - mambo ni aje?
Tatizo hili umelimaliza maliza kiaje? au umeliweka pending - tupe updates please! kama umepata shuruhisho please share with us hapa JF.
 
Back
Top Bottom