Nisaidieni, najihisi kabisa nimepewa limbwata

Wewe hujapewa limbwata isipokuwa umenogewa na viuno vya Kimakonde (Joking) 🤪
=========
Kama imefikia hatua, umewatelekeza watoto wako wa kuzaa mwenyewe huku ukilea wa huyo Mchepuko na kuwasomesha, basi una hali mbaya.

Hapo ukute umelishwa uchafu wote na huyo mchepuko ili uendelee kumwona ni mzuri na mrembo kuliko mkeo mliyeanza naye maisha.

Fanya mpango, upate urudi kwako na uache kula chakula chochote kitakachoandaliwa na mchepuko wako, lakini pia hamisha nguo zako zote uzirudishe nyumbani.

Baada ya hapo tafuta mtaalamu akutapishe hivyo ulivyolishwa. Thereafter utarudi kuwa normal na utaanza kuipenda upya familia yako.

Muhimu huyo mchepuko, hujazaa naye.
 
Ungekua umepewa limbwata usingekua na uwezo wakujitambua maswala ya kujihisi🤣🤣
 
Dodoma kuna watu maalum wa kufariji watumishi waliohamishiwa kule
Kuna jamaa yangu alihamia huko kama 4 years ss,
Mwaka wa kwanza wote alikuwa anarudi Dar kila weekend Ijumaa ama Jumamosi kurudi Dom tena J2 au J3,
Mwaka wa pili akawa anakuja Dar kuchek Familia Mara Mbili kwa mwezi,
Mwaka wa tatu akawa anarudi Mjini mara Moja kwa mwezi,
Mwaka wa 4, hv nnavyozungumza hajarudi tena mjini yapata miezi 9!
ama kweli Dodoma wapo wafariji!!
 
Anayelogwa huwa anajua?
 
Yaan upewe limbwata na bado fahamu uwe nayo, na unakua kabisa umepewa limbwata? Hivi unalijua au unalisikia?

Acha kufananisha limbwata na mambo ya kijinga.
 
Umepotea au ndio umefika (Kama roho yako imefika kwanini Hukatili roho; wewe kama ushalamba asali chonga mzinga) issue ni kwamba tu unapowekeza huenda hakuna reciprocation...

 
Usicheze kabisa na Dom, Bora hata Dar mtu anaweza kujikaza🤣
Shida Dom kuna kibaridi flani hivi cha kuamsha hamu🤣🤣🤣 lazima utafute kumbatio, ukinogewa unasahau familia.
Hata huyu jamaa mkewe naye alikuwa anamtafutia sababu, anarudije nyumbani bila kutoa taarifa🤣🤣
 
Yaan upewe limbwata na bado fahamu uwe nayo, na unakua kabisa umepewa limbwata? Hivi unalijua au unalisikia?

Acha kufananisha limbwata na mambo ya kijinga.
Hajarogwa huyu, Kwanza wamakonde tunaendaga kurogea Nchumbijiii kwenye origin yetu, Angeendewa huko angesahau hata Kama aliwahi kuwa na familia.....awaulize waliowapa wamakonde mapagala Yao walinde walivyoyasahau🤣🤣

Huyu kakolezwa tu na mapenzi matamu, kauli nzuri, mapishi, usafi na ukarimu....kurogwa hajarogwa.
 
Ni pm fastaa usupoteze dakika wala sekunde askari.
Wakati wa Mungu ushafika.
Ni wakati wa wewe kukombolewa .
Watoto wanakuita,amka
 
Poleee sana. Leo hii unaona mke hana umuhimu lkn ukiumwa hapo au ukikosa kazi utarudi kwa mke yule yule uliyemwona hana maana. Kesho watoto wasipokuheshimu utaanza kulalamika kuwa mama yao anawalisha sumu. Kama sio kulogwa kitu gani usahau hata watoto wako uliozaa mwenyewe ukasomeshe watoto wa wenzio.

Wanaume Mungu awasaidie sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wanaume very cheap, ukutane na mwanamke siku hiyo hiyo na umle siku hiyo hiyo?

Afya mcheki saa ngapi?
huwezi kufikiria kuwa analika kirahisi na hayupo sqlama?

Hilo ndio jambo limenishinda.

Mwanamke mrahisi kivile simtaki kabisa na naona kinyaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…