Nisamehe Rais wangu Magufuli

Nisamehe Rais wangu Magufuli

Mimi ni kati ya Watanzania ambao tulikuwa hatukuelewi kipindi ukiwa hai. Ni kweli, kama mwanadamu ulikuwa na mapungufu yako. Lakini jambo moja ni hakika, uliipenda Tanzania na Watanzania kwa moyo wako wote.

Kila nikisikiliza ule wimbo wa Msechu huwa ninatokwa na machozi. Pumzika kwa amani Rais Magufuli. Hakika tunakulilia kama ulivyosema tutakukumbuka kwa mema yako.
Umefanya jambo jema kwasababu JPM ameusikia msamaha wako. Mtu akifa, kinachokufa ni mwili tuu lakini roho haifi, hivyo JPM yupo na amekusikia! Life After Life: Je, wajua Magufuli huko alipo anayaona yote? Je, tuendeleze 'double standards' ya 'cherry picking' au tuiachie Karma iwashughulikie?

P
 
Kinachonishinda kuelewa sasa hivi bila kujali mengine yote ni hili:

Ilikuwakuwaje hadi watu wawili ambao ni tofauti kabisa; yaani Magufuli na Samia wakaweza kufanya kazi pamoja muda wote ule?

Ni wazi kabisa udhaifu mkubwa sana uliomo ndani ya chama cha mapinduzi.

Samia na Magufuli ni watu wawili wanaotofautiana sana, siyo kwa mazuri yao tu; bali hata katika mabaya yao. Katika hali ya kawaida hawa watu wasingeweza kamwe kufanya kazi kwa pamoja.

Ukiniuliza nitaje ni wapi hawa wawili walipofanana katika kulitumikia taifa hili nitapata wakati mgumu kukupa mfano halisi. Kwa mfano, Samia anawapenda sana watu wake, wanaonufaika na asali ya nchi hii chini yake, kiasi kwamba hizi takataka nyinginezo zinazoishi katika nchi hii kwake ni kama uchafu tu!
Kwa upande wa Magufuli, yeye alionyesha (hata kama ni kwa kupenda sifa, hilo sijui) kuwa taifa hili linahitaji kuwanufaisha na kuinua hali za aliowaita wanyonge. Lile kundi ambalo sasa Samia kalikumbatia kwa nguvu kabisa, likawa ni kama maadui wakubwa wa taifa kwake.
Sasa hawa watu waliweza vipi kuwa pamoja na kufanya kazi vizuri pamoja?

Samia kajipambanua wazi kabisa, kwamba kwake, nchi ya Tanzania kwake ni fursa tu ya kuwawezesha wenye kamba na wengineo toka nje. Moyoni mwake hakuna linalomuumiza kuhusu hatma ya nchi hii. Magufuli yeye kwa upande wake, alipiga kelele nyingi sana (sijui kama zilikuwa za kweli au ghelesha tu); lakini alijipambanua kuwa anapigania maslahi ya nchi/taifa; lakini kasahau kwamba maslahi hayo ni ya watu, hata wale wakorofi waliokuwa na choyo binafsi. Badala ya kutumia njia na taratibu za kuwakomesha hawa, kwake ikawa kutumia njia za mkato, za kuumiza. Huu ndio udhaifu mkubwa uliomfanya asitambulike zaidi kwa yale yote mazuri aliyoyafanya kwa faida ya nchi hii; ambayo sasa ndio yanayofanya wengi, hata wale waliokuwa wanasita kumpa heshima yake wakati huo, sasa wanamlilia, bila shaka bila kusahau madhaifu yake!

Je, Samia na yeyey leo hii akiondoka kwenye kiti hicho, naye atakumbukwa kwa uzuri wake - hasa kule kutotumia njia za kikatili alizotumia Magufuli? Hii itatosha kumlilia Samia, kama anavyoliliwa Magufuli wakati huu?
Tuisubiri Historia itazungumza yenyewe.
Kwa Samia sahau hilo kwa maana wapenda Bata huwa hatuwakumbuki kabisa kama hao waliopita
 
Mimi ni kati ya Watanzania ambao tulikuwa hatukuelewi kipindi ukiwa hai. Ni kweli, kama mwanadamu ulikuwa na mapungufu yako. Lakini jambo moja ni hakika, uliipenda Tanzania na Watanzania kwa moyo wako wote.

Kila nikisikiliza ule wimbo wa Msechu huwa ninatokwa na machozi. Pumzika kwa amani Rais Magufuli. Hakika tunakulilia kama ulivyosema tutakukumbuka kwa mema yako.
CCM chama changu ndio kiliifanya KAZI ya jpm kuwa ngumu sana ndio Maana hatukumuelewa!!

Chama kinaruhusuje wizi,ufisadi na ubadhirifu kukita mizizi kiasi hiki!!?

Akija mwenye Nia njema lazima atateseka sana kusafisha chama na serikali!

Rip comrade jpm!
 
Kwa Samia sahau hilo kwa maana wapenda Bata huwa hatuwakumbuki kabisa kama hao waliopita
Wewe unajisemea upande wako mkuu, ambao ni upande wa Magufuli. Kuna "wala Bata" ambao hawasikii lolote kuhusu mtu wao huyo, hata kama huwasikii mara kwa mara. Akina JK hadi leo wanao wafuasi, usisahau.

Ngoja nisiondoke bila kukupa ushauri huu.
Ni vizuri kumkumbuka kiongozi mliyeona anafanya kazi nzuri kwa maoni yenu. Hiyo haitoshi, hasa katika wakati huu.
Kumuenzi kiongozi wenu ni kufanya juhudi ya kuondoa yale mnayoona kiongozi huyo hakuyapenda. Ni jukumu lenu sasa kujipanga kuhakikisha kuwa haya msiyoyapenda yaondoke haraka. Haitoshi kubaki mnalalama tu na kumlilia kiongozi. Lindeni 'legacy' yake kwa kuhakikisha aliyokuwa akiyasimamia hayavurugwi kama yanavyovurugwa sasa hivi.
Anzieni kampeni zenu huko ndani ya chama chenu.
 
Nimeiona hii picha nimelia sana hadi muda huu machozi yananilengalenga hadi nashindwa kuona vizuri herufi kwenye keyboard.Nikikumbuka namna nchi inavyoharibiwa na kuuzwa Kwa waarabu ambao ni kichaa pekee anaweza kukubali hayo matwakwa yao.pumzika Kwa amani mzalendo.ulisema kweli tutakukumbuka
 
Hakuna lolote, Rais asiyetoa ansurance ya usalama wa wananchi wake hata wale wanaomkosoa basi huyo hafai hata kidogo.

Bora ulale njaa ila una uhakika wa haki ya kuishi.
Kanyima haki za kuishi kwa baadhi ya watu ambao hatunao leo.

Apumzike anapostahili.
 
Wewe unajisemea upande wako mkuu, ambao ni upande wa Magufuli. Kuna "wala Bata" ambao hawasikii lolote kuhusu mtu wao huyo, hata kama huwasikii mara kwa mara. Akina JK hadi leo wanao wafuasi, usisahau.

Ngoja nisiondoke bila kukupa ushauri huu.
Ni vizuri kumkumbuka kiongozi mliyeona anafanya kazi nzuri kwa maoni yenu. Hiyo haitoshi, hasa katika wakati huu.
Kumuenzi kiongozi wenu ni kufanya juhudi ya kuondoa yale mnayoona kiongozi huyo hakuyapenda. Ni jukumu lenu sasa kujipanga kuhakikisha kuwa haya msiyoyapenda yaondoke haraka. Haitoshi kubaki mnalalama tu na kumlilia kiongozi. Lindeni 'legacy' yake kwa kuhakikisha aliyokuwa akiyasimamia hayavurugwi kama yanavyovurugwa sasa hivi.
Anzieni kampeni zenu huko ndani ya chama chenu.
Any chama gani unaongelea maana mie niko chamaless
 
Nimeiona hii picha nimelia sana hadi muda huu machozi yananilengalenga hadi nashindwa kuona vizuri herufi kwenye keyboard.Nikikumbuka namna nchi inavyoharibiwa na kuuzwa Kwa waarabu ambao ni kichaa pekee anaweza kukubali hayo matwakwa yao.pumzika Kwa amani mzalendo.ulisema kweli tutakukumbuka
Kama zingekuwepo hata barua kwenda Mungu walu ningemwambia jinsi hawa viongozi uchwala wanavyo iharibu yoyote aliunda upya jembe letu na kumnoa jembe ambaye akija atafyeka wala rushwa zaidi ya kim jong
 
Mimi ni kati ya Watanzania ambao tulikuwa hatukuelewi kipindi ukiwa hai. Ni kweli, kama mwanadamu ulikuwa na mapungufu yako. Lakini jambo moja ni hakika, uliipenda Tanzania na Watanzania kwa moyo wako wote.

Kila nikisikiliza ule wimbo wa Msechu huwa ninatokwa na machozi. Pumzika kwa amani Rais Magufuli. Hakika tunakulilia kama ulivyosema tutakukumbuka kwa mema yako.
"Na Mimi nataka niseme Watanzania mtanikumbuka na mtanikumbuka kwa mazuri na si kwa mabaya kwasababu nimesacrifice maisha yangu kwa wananchi masikini"
 
Hayo yote unayoeleza watu wameyasikia tokea Magufuli akiwa hai ila bado watu wanamkumbuka Magufuli. Athari za mapungufu ya Samia ziko wazi na zinawagusa watu kiuhalisia kuliko mengi yaliyoelezwa kuhusu Magufuli.
Kama yapi? Taja moja tu
 
Back
Top Bottom