Kinachonishinda kuelewa sasa hivi bila kujali mengine yote ni hili:
Ilikuwakuwaje hadi watu wawili ambao ni tofauti kabisa; yaani Magufuli na Samia wakaweza kufanya kazi pamoja muda wote ule?
Ni wazi kabisa udhaifu mkubwa sana uliomo ndani ya chama cha mapinduzi.
Samia na Magufuli ni watu wawili wanaotofautiana sana, siyo kwa mazuri yao tu; bali hata katika mabaya yao. Katika hali ya kawaida hawa watu wasingeweza kamwe kufanya kazi kwa pamoja.
Ukiniuliza nitaje ni wapi hawa wawili walipofanana katika kulitumikia taifa hili nitapata wakati mgumu kukupa mfano halisi. Kwa mfano, Samia anawapenda sana watu wake, wanaonufaika na asali ya nchi hii chini yake, kiasi kwamba hizi takataka nyinginezo zinazoishi katika nchi hii kwake ni kama uchafu tu!
Kwa upande wa Magufuli, yeye alionyesha (hata kama ni kwa kupenda sifa, hilo sijui) kuwa taifa hili linahitaji kuwanufaisha na kuinua hali za aliowaita wanyonge. Lile kundi ambalo sasa Samia kalikumbatia kwa nguvu kabisa, likawa ni kama maadui wakubwa wa taifa kwake.
Sasa hawa watu waliweza vipi kuwa pamoja na kufanya kazi vizuri pamoja?
Samia kajipambanua wazi kabisa, kwamba kwake, nchi ya Tanzania kwake ni fursa tu ya kuwawezesha wenye kamba na wengineo toka nje. Moyoni mwake hakuna linalomuumiza kuhusu hatma ya nchi hii. Magufuli yeye kwa upande wake, alipiga kelele nyingi sana (sijui kama zilikuwa za kweli au ghelesha tu); lakini alijipambanua kuwa anapigania maslahi ya nchi/taifa; lakini kasahau kwamba maslahi hayo ni ya watu, hata wale wakorofi waliokuwa na choyo binafsi. Badala ya kutumia njia na taratibu za kuwakomesha hawa, kwake ikawa kutumia njia za mkato, za kuumiza. Huu ndio udhaifu mkubwa uliomfanya asitambulike zaidi kwa yale yote mazuri aliyoyafanya kwa faida ya nchi hii; ambayo sasa ndio yanayofanya wengi, hata wale waliokuwa wanasita kumpa heshima yake wakati huo, sasa wanamlilia, bila shaka bila kusahau madhaifu yake!
Je, Samia na yeyey leo hii akiondoka kwenye kiti hicho, naye atakumbukwa kwa uzuri wake - hasa kule kutotumia njia za kikatili alizotumia Magufuli? Hii itatosha kumlilia Samia, kama anavyoliliwa Magufuli wakati huu?
Tuisubiri Historia itazungumza yenyewe.