Niseme tu namkubali sana Prophet Lovy Elias (Tarehe 08/12/2023 sio ya kukosa)

Brother!
Watanzania wengi wanaowaponda manabii hawa;Passion Java na Papa Lovy Elias Longomba hawafuatilii mafundisho yao kwa kina wanaangalia tu muonekano.

Wana nondo gani? Hata Makenzie alikuwa na nondo kwa kondoo wake. Nabii kipini na dread na matatoo mwili mzima. Mungu atusamehe kwakweli. Yani Java mwaka Jana tu alikuwa anavaa kishoga kwenye club za usiku na akawa DJ na ndiye Rais wa label ya Rayvanny. Sasa hapo mjinga nani? Nyie danganyikeni wenyewe msidanganye wengine.
 
we waache na ujinga wao watakua kama watoto waliodhihaki kipala cha Nabii Elisha unajua nn kiliwatokea ?

Wamekuja manabii wangapi Tanzania na kuondoka. Mbona akina Mwakasege wapo na hawashuki kiwango zaidi ya Mika 32?. Huyu Lovy alikuwa mwimba miziki ya kidunia na kundi lake la longombas akaenda marekani, ghafla Kawa nabii. Unategemea Nini hapo.
 
Wabongo wengi tunaangalia mambo juu juu sana yaani kama ni vitabu sisi rangi ya jalada tu inatutosha kusema chochote tusichokijua juu ya kitamu kama tumekisoma hivi...uvivu wa kufuatilia mambo na ugumu wa kuingiza maarifa mapya ni zaidi ya janga....

Acha upotoshaji. Biblia inasema tujitofautishe na walimwengu na njia zao. Wewe unataka ushoga na hapo hapo uwe Nabii. Hapana Hapana.
 
Basi hata wewe ni nabii
 
Huyu ana matatuu dread na vipini yani anapga mapigo ya diamond nadhani ni biashara maana wameletwa na wasafi si wanajua vijana siku hizi wanapenda swaga hadi kwenye imani basi wamewaletea nabii wao.
Ukristo sijui baada ya miaka 20 utakuwaje
Hawajaletwa na wasafi... Wameletwa na Malisa wa Kingdom Embassy pale kibangu
 
Biblia imeandika "msidanganyike Mungu hadhiakiwi"
Huyo si Mtumishi wa Mungu aliyeumba Mbingu na nchi ninaye mjua mimi
 
Acha upotoshaji. Biblia inasema tujitofautishe na walimwengu na njia zao. Wewe unataka ushoga na hapo hapo uwe Nabii. Hapana Hapana.
Kujitofautishaje, kuna maelekezo au utamaduni?.. Wapi ulisikia wakisema wanataja ushoga na unabii?
 
Makenzie unamlinganisha na Passion Java na Lovy?..duuuh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…