Nishati Jadidifu: TotalEnergies yafanya tena kweli, yaongoza njia. Waziri Makamba aipongeza, awataka wengine wafuate

Kabla ya kusifia sana naomba unipe faida ya hicho kiambata excellium kwenye mafuta?? Na mafuta yakikikosa yanakosaje ubora?
Mkuu Gallius , karibu pande hizi

P
 
Mimi ni Mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, nafanya kazi ya uandishi kwa mapenzi tuu, sio kwa kupata chochote, na nafanya bure.

P
Mmmmm ile kampuni yako Ya PPR ni charity organisation kama charity ya mama Teresa inahudumia bure?
 
Mmmmm ile kampuni yako Ya PPR ni charity organisation kama charity ya mama Teresa inahudumia bure?
It's a charity. Hata ukisikia, Leo, kesho, nimetangulia mbele ya haki, usilie, furahi maana nitakuwa nimekwenda straight kuume kwa Baba yangu.
P
 
Pasco ukiwa unaandika makala huchanganyi kingereza na Kiswahili, ila ukiandika humu JF inakuwa bokoboko
 
Kwa hiyo Total ndo wa kwanza kutumia sola!? mbona hadi vijiji vya ndani ndani huku ntimpwindi watu wanatumia sola, au mimi ndo sijaelewa hiki unachojaribu kuaminisha watu kwamba ni innovation kubwa ambayo haijawahi kufanyika hapa bongo.
 
Paa zima ni panel!. Umeona wapi wewe paa zima la nyumba ni panel?.

Hii maana yake Tanzania sasa tuache kuezekea bati, zege na vigae, tuezekee solar panels. Kwenye vituo vya mafuta, TotalEnergies ndio wa kwanza.
P
 
Pasco ukiwa unaandika makala huchanganyi kingereza na Kiswahili, ila ukiandika humu JF inakuwa bokoboko
JF ni social media, tunatumia informal language.
Kuna chakula ni vitamu zaidi vikipikwa kwenye chungu na kwa Mkaa kuliko kwenye gesi na umeme. Vivyo hivyo, kuna maneno ni matamu zaidi yakitamkwa kwa lugha za watu kuliko kwa lugha yako.
P
 
Mimi ni Mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, nafanya kazi ya uandishi kwa mapenzi tuu, sio kwa kupata chochote, na nafanya bure.

P
Sema ukweli bana kampuni yako ya PR umepata tender ya kuipamba Total na sio mbaya kula jasho lako ilihali hujamfanyia mtu fitna.
 
kampuni kimeo, waziri kimeo

umeme wa jua hauko viable in the long-run, muda utasema, labda kama ni kufurahisha genge, au kuna pipoz zinanufaika na 10% za 'periodic maintenance' hapo
 
Kuonyesha - asili ya neno "onya"
Kuonesha - asili ya neno "ona"

Usahihi katika makala yako, Kichwa cha habari kilitakiwa kisomeke KUONESHA na sio KUONYESHA

Acha kuweka wahariri wa Kisukuma
 
Kuonyesha - asili ya neno "onya"
Kuonesha - asili ya neno "ona"

Usahihi katika makala yako, Kichwa cha habari kilitakiwa kisomeke KUONESHA na sio KUONYESHA

Acha kuweka wahariri wa Kisukuma
Asante Sana kwa Ushauri. Umepokelewa.
P
 
Paa zima ni panel!. Umeona wapi wewe paa zima la nyumba ni panel?.

Hii maana yake Tanzania sasa tuache kuezekea bati, zege na vigae, tuezekee solar panels. Kwenye vituo vya mafuta, TotalEnergies ndio wa kwanza.
P
Basi waache kutuuzia fosil fuel waanze kutupimia umeme wa jua kwenye magari.......hapo ndo nitaamini kwamba wameongoza njia.
 
Sema ukweli bana kampuni yako ya PR umepata tender ya kuipamba Total na sio mbaya kula jasho lako ilihali hujamfanyia mtu fitna.
PPR sio kampuni yangu, mimi pale nimeajiriwa kama day waka tuu, kazi ya uandishi wa habari, naifanya bure kwa kujitolea tuu, silipwi chochote na yeyote.
P
 
Happy Valentine's day!.
Totalenegies kama kawaida yao, pita jaza ujazwe!.
Kwa watu wa bagamoyo rd, mambo yote totalenegies Oyster Bay Service Station.
Happy Valentine's
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…