Nishati Safi ya Kupikia: Badala ya Kugawa Mitungi ya Gesi, Kwanini tusigawe induction Cookers

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Mtungi mdogo wa Gesi wa Kilo Sita Net bei yake ni elfu 45 mpaka elfu 55
1728838773368.png
Nimecheki hii Induction Cooker direct from Factory huko China
induction cooker.jpg
Hata tukichukilia kwamba dollar moja ni elfu 2600 hii cooker inaweza kuwa na gharama ndogo kuliko hilo jiko tunalogawa bure kwa watu..., LAKINI kabla ya yote ngoja tuangalie matumizi

1kg ya Gesi = 13.6kwh (units)
Kwenye Mtungi wa 6 kgs (
ingawa gesi iliyopo kwenye mtungi sio 6kgs kutokana na uzito wa Mtungi)
Kwahio kwenye Mtungi wa gesi wa 6kgs kuna Units Ngapi

13.6kwh x 6 equals to approx = 81.6 Units
Kwahio Mtungi wa kilo 6 una Units takriban 81.6

Mtungi huu unajazwa kwa Tshs. 25,000/=; Hivyo tunaweza kusema Unit moja unanunua kwa 25,000/81.6 = 306.3
Kumbuka kwa sasa
  • Unit moja mjini unanunua kwa Tshs. 292 /=
  • Vijijini Unit Moja inanunuliwa kwa Tshs. 100/=
Kwahio mpaka dakika hii hilo jiko wanalopewa wanavijiji ni gharama kwa matumizi kuliko hata kupikia umeme

JIKO LA INDUCTION LINA UFANISI ZAIDI YA MARA MBILI MPAKA TATU YA GESI
Kwa mifano hapo juu; mtu wa kijijini atakuwa anatumia kwa bei rahisi zaidi kuliko mtu anayetumia hilo jiko la gesi kwa unit yaani wakati mwenye gesi anatumia Tshs. 306/= kwa unit; wa induction atakuwa anatumia Tshs. 33/= Yaani zaidi ya mara tisa

Nilishauri Tanesco iingie PPP na kampuni za Majiko na badala ya kuagiza wanaweza wakaya-assemble nchini

Soma Pia: Nishati Safi ya Kupikia (PPP tunayohitaji Kuingia)

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichanacho, Tufanye Tunachoweza

Wabongo wanapenda vya bure.

Haya mtugawie na cha kupika sasa.

Unanipa jiko bila sufuria wala unga
Wala hapa hakuna bure..., Huyu Bibi yangu na Babu yangu waliokuwa wanapikia vijikuni vya kuokota okota (bure) sasa hivi wanapewa mitungi na haya majiko bure ambapo wakijaza mara mbili tu ni sawa na bei ya hilo jiko au ni sawa na bei ya kununua induction cooker ambayo itakuwa na gharama ndogo (zaidi ya mara tisa) kuliko huu mkenge wanaoingizwa sasa hivi...

Ni kama drug dealer anakupa drugs bure mara ya kwanza akijua utakuwa teja....

Kumbuka tunapoelekea mkaa utapigwa marufuku
 
iyo jiko mbongo akipika ugali halitoboi zaid ya week
Kwa bei ya sasa hata ukipikia kwa jiko la umeme la coil bado kupikia umeme ni bei rahisi unanunua unit kwa Tshs 100/= wakati mwenye hicho kijiko atakuwa anatumia zaidi ya Tshs. 306/=

Anyway angalia mtu hapa anapikia Induction Cooker (Na kama bei yake ni kama nusu ya mtu anayejaza gesi kila ikiisha hata ukifanya hili jiko liwe disposable bado litakuwa cheaper kuliko hio mitungi

Sufuria za induction cooker wanauza wapi? Nauliza swali hili nikiwa kijijini kwangu Kazuramimba.
Any ferromagnetic pot itafanya kazi, ingawa sio sufuria za aluminium.., kwahio kama tutaweza kuagiza / kuassembly haya majiko sidhani kama tutashindwa kuongeza / kutengeneza masufuria ukizingati hata majembe na koroboi tulikuwa tunatengeneza ije kuwa sufuria ? (Raw Materials tunazo)
 
Mtungi mdogo wa Gesi wa Kilo Sita Net bei yake ni elfu 45 mpaka elfu 55
Nimecheki hii Induction Cooker direct from Factory huko China
Hata tukichukilia kwamba dollar moja ni elfu 2600 hii cooker inaweza kuwa na gharama ndogo kuliko hilo jiko tunalogawa bure kwa watu..., LAKINI kabla ya yote ngoja tuangalie matumizi

1kg ya Gesi = 13.6kwh (units)
Kwenye Mtungi wa 6 kgs (
ingawa gesi iliyopo kwenye mtungi sio 6kgs kutokana na uzito wa Mtungi)
Kwahio kwenye Mtungi wa gesi wa 6kgs kuna Units Ngapi

13.6kwh x 6 equals to approx = 81.6 Units
Kwahio Mtungi wa kilo 6 una Units takriban 81.6

Mtungi huu unajazwa kwa Tshs. 25,000/=; Hivyo tunaweza kusema Unit moja unanunua kwa 25,000/81.6 = 306.3
Kumbuka kwa sasa
  • Unit moja mjini unanunua kwa Tshs. 292 /=
  • Vijijini Unit Moja inanunuliwa kwa Tshs. 100/=
Kwahio mpaka dakika hii hilo jiko wanalopewa wanavijiji ni gharama kwa matumizi kuliko hata kupikia umeme

JIKO LA INDUCTION LINA UFANISI ZAIDI YA MARA MBILI MPAKA TATU YA GESI
Kwa mifano hapo juu; mtu wa kijijini atakuwa anatumia kwa bei rahisi zaidi kuliko mtu anayetumia hilo jiko la gesi kwa unit yaani wakati mwenye gesi anatumia Tshs. 306/= kwa unit; wa induction atakuwa anatumia Tshs. 33/= Yaani zaidi ya mara tisa

Nilishauri Tanesco iingie PPP na kampuni za Majiko na badala ya kuagiza wanaweza wakaya-assemble nchini

Soma Pia: Nishati Safi ya Kupikia (PPP tunayohitaji Kuingia)

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichanacho, Tufanye Tunachoweza

Iwapo viongozi wetu watachukua ushauri huu wako MZURI SANA itakuwa ni Jambo la heri mno.
 
My experience na hiyo induction cooker:
1. Inahitaji sufiria maalumu
2. Inachukua muda kuivisha
3. Inatumia umeme mwingi kuliko inavyosemekana
4. Umeme ulikatika, hamna kupika
5. Ilidumu kwa siku 20, then ikapiga shoti

Nisiwe too conclusive lakini, inawezekana the brand niliyokuwa natumia ndiyo ilikuwa na changamoto. After that first experience with induction cookers, it left a bad impression nikarudi kutumia gas.
 
Ulitumia brand gani?
Inatumia Unit ngapi ?
Kuna inferred cooker na induction cooker zote zinafanana utajuaje tofauti?
 
Mtungi mdogo wa Gesi wa Kilo Sita Net bei yake ni elfu 45 mpaka elfu 55
Nimecheki hii Induction Cooker direct from Factory huko China
Hata tukichukilia kwamba dollar moja ni elfu 2600 hii cooker inaweza kuwa na gharama ndogo kuliko hilo jiko tunalogawa bure kwa watu..., LAKINI kabla ya yote ngoja tuangalie matumizi

Hilo jiko la induction ni bei juu kuliko la gesi
Hadi kulifikisha Kwa mnunuzi sio chini ya 50 000 hapo hujaweka faida ya kuliuza
 
Back
Top Bottom