Nishati Safi ya Kupikia: Badala ya Kugawa Mitungi ya Gesi, Kwanini tusigawe induction Cookers

Nishati Safi ya Kupikia: Badala ya Kugawa Mitungi ya Gesi, Kwanini tusigawe induction Cookers

Hapo ndipo jiko gesi linapoizidi jiko la induction
Gesi ikikata (kuisha)?😂😂

Mkaa/ndo mpango mzima wasituzuie kikubwa watuhamasishe kupanda miti Kwa wingi. Bado tuna ardhi kubwa mno isiyo limwa asee. Na miti Kila muda huchipua ikikatwa!!
 
Mtungi mdogo wa Gesi wa Kilo Sita Net bei yake ni elfu 45 mpaka elfu 55
Nimecheki hii Induction Cooker direct from Factory huko China
Hata tukichukilia kwamba dollar moja ni elfu 2600 hii cooker inaweza kuwa na gharama ndogo kuliko hilo jiko tunalogawa bure kwa watu..., LAKINI kabla ya yote ngoja tuangalie matumizi

1kg ya Gesi = 13.6kwh (units)
Kwenye Mtungi wa 6 kgs (
ingawa gesi iliyopo kwenye mtungi sio 6kgs kutokana na uzito wa Mtungi)
Kwahio kwenye Mtungi wa gesi wa 6kgs kuna Units Ngapi

13.6kwh x 6 equals to approx = 81.6 Units
Kwahio Mtungi wa kilo 6 una Units takriban 81.6

Mtungi huu unajazwa kwa Tshs. 25,000/=; Hivyo tunaweza kusema Unit moja unanunua kwa 25,000/81.6 = 306.3
Kumbuka kwa sasa
  • Unit moja mjini unanunua kwa Tshs. 292 /=
  • Vijijini Unit Moja inanunuliwa kwa Tshs. 100/=
Kwahio mpaka dakika hii hilo jiko wanalopewa wanavijiji ni gharama kwa matumizi kuliko hata kupikia umeme

JIKO LA INDUCTION LINA UFANISI ZAIDI YA MARA MBILI MPAKA TATU YA GESI
Kwa mifano hapo juu; mtu wa kijijini atakuwa anatumia kwa bei rahisi zaidi kuliko mtu anayetumia hilo jiko la gesi kwa unit yaani wakati mwenye gesi anatumia Tshs. 306/= kwa unit; wa induction atakuwa anatumia Tshs. 33/= Yaani zaidi ya mara tisa

Nilishauri Tanesco iingie PPP na kampuni za Majiko na badala ya kuagiza wanaweza wakaya-assemble nchini

Soma Pia: Nishati Safi ya Kupikia (PPP tunayohitaji Kuingia)

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichanacho, Tufanye Tunachoweza

Wanagawa upuuzi huo as RUSHWA...BRIBES KWA AJILI YA UCHAGUZI
 
My experience na hiyo induction cooker:
1. Inahitaji sufiria maalumu
Yes sababu induction inavyofanya kazi ni kupitisha umeme (alternating current) hivyo kutengeneza eddy currents kwenye sufuria ambazo zinatengeneza joto (kwahio sufuria lolote ambalo ni magnetic linafanya kazi)
2. Inachukua muda kuivisha
Hapana hakuna kitu kinachoivisha kwa haraka (kupata joto instantly kama induction cooker), kwahio ukiweka temperature unayotaka unaipata instantly (hakuna device nyingine yoyote inayoweza kufanya hivyo) ingawa ukitaka ichukue muda ofcourse unaweza ukaweka temprature ndogo (kwahio inafanya kazi in all ranges of temperature

3. Inatumia umeme mwingi kuliko inavyosemekana
Capacity Power ya kitu ni Watts; mfano birika lako la kuchemshia maji linaweza kuwa 1500watts lakini likachukua sekunde kuchemsha maji wakati jiko lako linaweza likawa 100watts likachukua saa kuchemsha maji yaleyale..., kwahio mwisho wa siku umeme ukawa uleule..., Hapo juu mfano hio Induction cooker ina capacity ya 2000watts lakini huenda kupika kwako mchicha ukatumia 100 watts na uzuri zaidi wa kufanya hii kitu iwe na ufanisi wa mpaka 90 percent ni kwamba nishati haipotei, wakati wewe ukiwasha gesi yako kuna nishati inapotea kwa kuchemsha hewa kabla ya kuchemsha hio aluminium induction cooker ni magnetic hence inapiga kwenye chombo unachopikia pekee na ukizima joto linapotea instantly no wastage....
4. Umeme ulikatika, hamna kupika
Hapa sijakuelewa kabisa.., ni sawasawa unasema mafuta yakiisha au gesi yako ikiisha hakuna kupika sababu hauna elfu 25,000 ya kujaza mtungi wako ? In short this is moot point..., badala ya kulaumu induction cooker kwa umeme kukatika labda ifike wakati tulaumu shirika kwa kukosa ufanisi (In short badala ya kulaumu tuhakikishe Tanesco inakuwa bora) Point yako ni kama unasema tuache kununua mashine za operation hospitali sababu zinatumie umeme na umeme unaweza kukatika
5. Ilidumu kwa siku 20, then ikapiga shoti
Kwanini ilipiga shoti (nadhani pa kuanzia ni hapo)
Nisiwe too conclusive lakini, inawezekana the brand niliyokuwa natumia ndiyo ilikuwa na changamoto. After that first experience with induction cookers, it left a bad impression nikarudi kutumia gas.
Tena kwa kusema kwako kwamba ilikuwa inatumia muda kupika huenda hata haikuwa induction cooker
 
Hilo jiko la induction ni bei juu kuliko la gesi
Hadi kulifikisha Kwa mnunuzi sio chini ya 50 000 hapo hujaweka faida ya kuliuza
Ndio maana nimeweka points kuu tatu:
  1. Hio ni direct from factory ambapo ni dollar sita kwa pcs elfu moja nina uhakika ukiweka pcs 500 bei itashuka
  2. Mbili kuna kitu kinaitwa economy of scale kupata shilingi moja kwa watu milioni moja ni nyingi kulika kupata laki moja kwa watu wanne..; hence ndio maana nikatoa ushauri kwa kampuni kama Tanesco kuingia Ubia na watengenezaji wa haya majiko either buying in bulk au kuweka assembly plant huku, tena ikiwa hivyo hata wakiuza kwa bei ya hasara au ku beak even wanaweza wakawa wanapata pesa kwa kuuza accessories na vifaa vya repair.
  3. Nne kama tunatoa Ruzuku kwa kuuza mitungi ya gesi (ruzuku ni kodi zetu) kwa kuwapa wanakijiji chombo ambacho kinazidi kuwatoboa mifuko ni bora kutoa ruzuku hio kwa jambo kweli linalosaidia na vilevile Tanesco wakichukua hili wanaweza wakapata faida kwenye carbon credit (kwanba wanauza vifaa vya clean cooking)
 
Usisahau gesi ya muhimu kuwa nayo kama umeme utakatika
Unaweza hata ukawa na jiko la mchina / la mafuta ya taa watu wa zamani wanajua haya, sababu zamani umeme ndio ulikuwa nishati ya kupikia kabla ya kuleta hizi lobbying na huenda kweli kipindi hicho jiko la coil halikuwa efficient lakini sasa hivi hili jiko ni zaidi ya mara tisa kwa ufanisi ukilinganisha na gesi...

Kwanza kabisa kwanini Umeme ukatike (labda tuanzie hapo) sababu kwenye gesi naona hasara zifuatazo tena ni hasara za muda mrefu
  1. Gesi tunaagiza kutoka nje kwahio Nishati hii tutakuwa tunasema tutumie nishati tegemezi (tunategemea); ingawa hakuna shida kutegemea kama hauna alternative, ingawa alternative ipo (UMEME) ambayo ni Safi na gharama ya chini ; Nishati Safi ya Kupikia, Mwarobaini tunao na ni Bora kuliko Gesi
  2. Gesi hii LPG ni gharama kuliko umeme tena kwa mtu wa kijijini akinunua hivi vimitungi vidogo anapata units kwa zaidi ya mia tatu wakati umeme ni 100/=
  3. Kwanini tutumie cha jirani (LPG) hata kingekuwa bora wakati tunacho chetu tena kingine kila siku kinapotea (Solar Power); Wazo huru: PPP's ya Tanesco na wamiliki wa nyumba Tanzania (133.2 gigawatts)
Am all for Free Market na ninaamini Adam Smith alisema kweli....;

It is the maxim of every prudent master of a family, never to attempt to make at home what it will cost him more to make than to buy...What is prudence in the conduct of every private family, can scarce be folly in that of a great kingdom.

Ni kweli kabisa kujaribu kutengeneza kitu kwa gharama zaidi kwako wakati ungeweza kununua kwa jirani ni Ujuha..., lakini ni Jambo la ajabu kabisa kwenda kununua kwa jirani kitu ambacho ni gharama kwako na ungeweza kukipata nyumbani kwa gharama nafuu....

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichonacho, Tufanye Tunachoweza
 
Yes Induction cookers powered by solar is the way forward
 
Attachments

  • IMG_0665.jpeg
    IMG_0665.jpeg
    20.9 KB · Views: 5
  • IMG_0664.jpeg
    IMG_0664.jpeg
    19.5 KB · Views: 5
  • IMG_0661.png
    IMG_0661.png
    96.6 KB · Views: 5
  • IMG_0660.png
    IMG_0660.png
    61.1 KB · Views: 5
  • IMG_0663.jpeg
    IMG_0663.jpeg
    16.8 KB · Views: 5
Wanagawa upuuzi huo as RUSHWA...BRIBES KWA AJILI YA UCHAGUZI
Bora wagawe TShirts watu wanajisitiri kwa baridi na watapendeza..., hii kitu ni kama Drug Dealer anakupa drugs bure alafu unakuwa teja na kutumia kila ulichonacho kwa kuendelea kununua kwake..., Hii gesi anayopewa mwanakijiji inacost equivalent ya zaidi ya Tshs 300/= tofauti na mtu huyu angetumia umeme ni Tshs 100/= kwa unit..., Ingawa nadhani kuna watu wanafanya lobbying ili mtungi huo na gesi ishuke bei..., Ila pesa hio itatoka wapi ni kwa huyu huyu mwananchi atakatwa kama Kodi na badala kodi hio imletee panadol itakwenda kwenye mifuko binafsi ya wauza gesi (mbaya zaidi wauzaji hawa wengine ni Ughaibuni tunapoagiza LPG)
 
Gesi ikikata (kuisha)?😂😂

Mkaa/ndo mpango mzima wasituzuie kikubwa watuhamasishe kupanda miti Kwa wingi. Bado tuna ardhi kubwa mno isiyo limwa asee. Na miti Kila muda huchipua ikikatwa!!
Kufanya Mkaa kama nishati kuu huenda isiwe sustainable lakini mtu mmoja mmoja yaani mtu binafsi anaweza akawa na misitu yake kwahio Kuni anaokota moja moja na kupika (mwanakijiji huyu atakuwa anatumia / anapata hizi kuni bure kabisa) na kuni hizo zikifanyiwa carbonization wala hazileti madhara kwake kiafya..., ila tukiongelea Jamii kwa ujumla Tanzania nzima hatuwezi tukaamua kutumia mkaa kama Nishati kuu na Miti ikapota (consumption ni kubwa kuliko uzalishaji) ; Ingawa kwanini nchi ya kitropiki yenye kila aina ya vyanzo vya nishati inayoweza kubadilishwa kuwa umeme Nishati iwe Tatizo ?; Fanya leo bei ya Unit Tshs 20/= uone kama kuna mtu atasumbuka na mkaa au nishati ya aina yoyote ile nyingine...
 
Mawazo Yako ni chana sana Wala sikupingi. Cha msingi pamoja na hayo yote kuihamsisha jamii kupanda miti itasaidia sana pia si kupikia tu Hali hewa pia
 
Mawazo Yako ni chana sana Wala sikupingi. Cha msingi pamoja na hayo yote kuihamsisha jamii kupanda miti itasaidia sana pia si kupikia tu Hali hewa pia
Naam kupanda miti na mazingira ni jambo muhimu sana tena sana wala hilo silipingi kabisa na ndio maana nasema huenda hata yule bibi anayekusanya vijimiti vikianguka ndio anapikia yeye ni champion wa mazingira kuliko sisi huku mijini wenye ma V8 yetu tunaofanya pollution lakini bado tunamshutumu yeye...
 
Mtungi mdogo wa Gesi wa Kilo Sita Net bei yake ni elfu 45 mpaka elfu 55
Nimecheki hii Induction Cooker direct from Factory huko China
Hata tukichukilia kwamba dollar moja ni elfu 2600 hii cooker inaweza kuwa na gharama ndogo kuliko hilo jiko tunalogawa bure kwa watu..., LAKINI kabla ya yote ngoja tuangalie matumizi

1kg ya Gesi = 13.6kwh (units)
Kwenye Mtungi wa 6 kgs (
ingawa gesi iliyopo kwenye mtungi sio 6kgs kutokana na uzito wa Mtungi)
Kwahio kwenye Mtungi wa gesi wa 6kgs kuna Units Ngapi

13.6kwh x 6 equals to approx = 81.6 Units
Kwahio Mtungi wa kilo 6 una Units takriban 81.6

Mtungi huu unajazwa kwa Tshs. 25,000/=; Hivyo tunaweza kusema Unit moja unanunua kwa 25,000/81.6 = 306.3
Kumbuka kwa sasa
  • Unit moja mjini unanunua kwa Tshs. 292 /=
  • Vijijini Unit Moja inanunuliwa kwa Tshs. 100/=
Kwahio mpaka dakika hii hilo jiko wanalopewa wanavijiji ni gharama kwa matumizi kuliko hata kupikia umeme

JIKO LA INDUCTION LINA UFANISI ZAIDI YA MARA MBILI MPAKA TATU YA GESI
Kwa mifano hapo juu; mtu wa kijijini atakuwa anatumia kwa bei rahisi zaidi kuliko mtu anayetumia hilo jiko la gesi kwa unit yaani wakati mwenye gesi anatumia Tshs. 306/= kwa unit; wa induction atakuwa anatumia Tshs. 33/= Yaani zaidi ya mara tisa

Nilishauri Tanesco iingie PPP na kampuni za Majiko na badala ya kuagiza wanaweza wakaya-assemble nchini

Soma Pia: Nishati Safi ya Kupikia (PPP tunayohitaji Kuingia)

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichanacho, Tufanye Tunachoweza

Unadhani viongozi hawajui hayo unayosema au uliyoandika tatizo wameshakula ten percent za watu na walipaji sasa ndio hao wanaoitwa wanyonge.

Viongozi wetu wanajua kabisa hakuna mtanzania wa kijijini atayemudu kununua gas ata kale kamtungi kadogo kijijini hawamudu..
 
Huku kugawa mitungi ya gesi kunachagizwa zaidi na wanasiasa, na hasa kipindi hiki tukielekea uchaguzi. Lakini kwa utafiti niliofanya mitungi mingi ipo nyumbani kama pambo, maana kujaza tena gesi kwa Tsh. 25,000/- kwa wengi imekuwa mtihani..!
 
Unadhani viongozi hawajui hayo unayosema au uliyoandika tatizo wameshakula ten percent za watu na walipaji sasa ndio hao wanaoitwa wanyonge.

Viongozi wetu wanajua kabisa hakuna mtanzania wa kijijini atayemudu kununua gas ata kale kamtungi kadogo kijijini hawamudu..
Viongozi ni wachache wananchi ndio wengi, kwahio viongozi wanatumia propaganda na kutokujua kwa wananchi ili kuweza kufanya na kupitisha mambo yao..., hivyo nachofanya ni kujaribu kuweka wazi nini ni nini..., mfano watu wengi wadhani yafuatayo:
  1. Gesi ina gharama nafuu kuliko umeme
  2. Ile Gesi ya mtwara (ambayo huenda ikawa ya kwetu) ndio hii gesi ya majumbani hence tunapohimiza matumizi ya gesi tunahimiza kutumia chetu
  3. Umeme hautoshi hivyo watu hawawezi kupikia (wakati Bwawa likiisha tutakuwa na double the capacity)
 
Induction cooker ni nzuri sana, magnetic ni ajabu sana ukibandika sufuria zake ukiwasha tu maji yanaanza kuchemka😂😂 na ukiepua kile kitako joto limepotea
fake P/pastor etii,magnetic induction cooker inafanyaje kazi?
 
Kuhimiza kupanda miti ni jambo lenye tija kuliko kuwaza juu ya mitungi ya gesi.
Ikumbukwe kuwa gesi ikiisha kwenye mtungi inabidi kupelekwa kwa wakala kujazwa upya. Hapa kuna gharama nyingine ambayo ni ama kwa kubeba kichwani ukitembea kwa miguu au kulioia boda boda.
Vile vile, kuna nyakati kule kwa mawakala wanakuwa hawana mitungi yenye gesi. Yaani hawana gesi. Pia inatokea wakala ameishiwa gesi ya kampuni ya mtungi ulionao.
Umeme ukidhibitiwa usikatike ni bora sana.kuliko gesi.
Hata hivyo, kwa maisha ya vijijini yalivyo kwa wananchi wengi, bado naamini kuwa kuni na mkaa bado ni bora zaidi.
Pia, bado gesi na mkaa havitumiki kwa kuchoma nyama, mahindi, mihogo nk.
Viongozi wapite vijijini waone maisha yetu.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Kijijini kupika wengi wala hawahitaji kutoa hata shilingi moja..., ni mwendo wa kuzunguka na kuokota kuni zake mtu anapika, mtu huyu mzunguko wake wa pesa huende mwezi mzima hajashika hata elfu kumi..., ndio maana nikasema mtu huyu badala ya kuvuna kuni anaweza akavuna jua akawauzia Tanesco akapewa credit za kupika.

Mtungi mdogo wa Gesi wa Kilo Sita Net bei yake ni elfu 45 mpaka elfu 55
Nimecheki hii Induction Cooker direct from Factory huko China
Hata tukichukilia kwamba dollar moja ni elfu 2600 hii cooker inaweza kuwa na gharama ndogo kuliko hilo jiko tunalogawa bure kwa watu..., LAKINI kabla ya yote ngoja tuangalie matumizi

1kg ya Gesi = 13.6kwh (units)
Kwenye Mtungi wa 6 kgs (
ingawa gesi iliyopo kwenye mtungi sio 6kgs kutokana na uzito wa Mtungi)
Kwahio kwenye Mtungi wa gesi wa 6kgs kuna Units Ngapi

13.6kwh x 6 equals to approx = 81.6 Units
Kwahio Mtungi wa kilo 6 una Units takriban 81.6

Mtungi huu unajazwa kwa Tshs. 25,000/=; Hivyo tunaweza kusema Unit moja unanunua kwa 25,000/81.6 = 306.3
Kumbuka kwa sasa
  • Unit moja mjini unanunua kwa Tshs. 292 /=
  • Vijijini Unit Moja inanunuliwa kwa Tshs. 100/=
Kwahio mpaka dakika hii hilo jiko wanalopewa wanavijiji ni gharama kwa matumizi kuliko hata kupikia umeme

JIKO LA INDUCTION LINA UFANISI ZAIDI YA MARA MBILI MPAKA TATU YA GESI
Kwa mifano hapo juu; mtu wa kijijini atakuwa anatumia kwa bei rahisi zaidi kuliko mtu anayetumia hilo jiko la gesi kwa unit yaani wakati mwenye gesi anatumia Tshs. 306/= kwa unit; wa induction atakuwa anatumia Tshs. 33/= Yaani zaidi ya mara tisa

Nilishauri Tanesco iingie PPP na kampuni za Majiko na badala ya kuagiza wanaweza wakaya-assemble nchini

Soma Pia: Nishati Safi ya Kupikia (PPP tunayohitaji Kuingia)

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichanacho, Tufanye Tunachoweza

Unaweza wewe kufanya hivyo
 
Wastage of time, bila vipato vya watu kukua bado mamilioni ya watu hawataweza kutumia iwe hiyo induction cooker au gesi. Hata uwape majiko kumi bado hawataweza kumudu gharama za matumizi. Ni sawa na umpe gari jobless, atakua na gari Ila mafuta kuweka atembelee ndio haitawezekana
 
Back
Top Bottom