Nishati Safi ya Kupikia: Badala ya Kugawa Mitungi ya Gesi, Kwanini tusigawe induction Cookers

Nishati Safi ya Kupikia: Badala ya Kugawa Mitungi ya Gesi, Kwanini tusigawe induction Cookers

Unauziwa jiko la gase la elfu 20, gase ikiisha unaenda umbali wa km 40 hadi 70 kujaza tena gase, nauli unatumia kati ya sh. Elfu 5 hadi elfu kumi. je,gharama hizo mwananchi wa kawaida ambae anashindia 1/3 ya milo kwa siku ataziweza?

Serikali iboreshe maisha ya wananchi kwanza kabla ya kuleta hizo nishati mbadala.
Na kuboresha maisha ni kuhakikisha watu wanabaki na disposable income na wanaweza kufanya hivyo huenda kama watahakikisha watu katika kupika hawatumii pesa....
 
Sijakupata mkuu! Unaweza ukaeleza kwa kina unachomaanisha? Je umekubaliana na hoja yangu au?
 
Sijakupata mkuu! Unaweza ukaeleza kwa kina unachomaanisha? Je umekubaliana na hoja yangu au?
Tunaboreshaje maisha ya mwananchi, moja wapo ni kuhakikisha tunampunguzia matumizi, Je tunampungiziaje matumizi kwa kuweza kumfanya akawa mwekezaji na kuweza kupikia chakula kwa gharama ya Tshs 0/= na kuwa mwekezaji wa kuwauzia Tanesco umeme

 
Asilimia kubwa ya maeneo ya vijiji maji ni tatizo kubwa mno ukiwawekea hizo biogas zitakufa ndani ya muda mfupi mnoo! Haiyata kuwa na tija.
Fikiri mtu.anajitwisha maji kichwani km 6-8 ili apate maji ya kunywa tu sasa yakutia katika mtungi au mtambo wa Biogas atatoa wapi.

Labda tumshauri kwanza waziri wa maji aandae bajeti ya kutosha kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Water saving indigenous skills kwa kila kijiji halafu tuvune maji ya mvua yanayo tiririka au kutemebea ardhini pale mvua inaponyesha.
Kwani maji yanayopotea bure ni mengi mnooo yangehifadhiwa mpango wa Biogas ungekuwa rahisi sana kwa kila nyumba.
Mbona tunaambiwa mambo ya kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani ? Au ni swaga
 
Mbona tunaambiwa mambo ya kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani ? Au ni swaga
Sio swaga yaani wanatuliwa lakini baadhi ya maeneo kuna maji yenye chumvi kiasi kwamba hupikii hata mboga za majani zinakacha haziivi,chakula hakiivi Iwe wali au ugali. Na hakuna mashine ya kuyachuja chumvi hivyo ina lazimu kujitwisha tena kichwani kuyafuata yanayofaa umbali mreeefu
 
Back
Top Bottom