Nishati Safi ya Kupikia: Badala ya Kugawa Mitungi ya Gesi, Kwanini tusigawe induction Cookers

Wewe ndio huekew8

Sawa wako wa bidhaa zote iwe sukari,Vipuri,mafuta ,majiko ya gesi nk sector binafsi wafanyabiashara binafsi ndio hununua huko factory price na kuleta tena meli na meli kama ni sugari wanaagiza Brazil ya kutosha nchi nzima kama ni mafuta ya magari wananunua ya kutosha nchi nzima kama ni majiko ya gesi wananunua ya kutosha nchi nzima
Hivi hata unajua unachoongea Sukari wala sijaongelea kutoka nje ndani ya nchi kuna watu wanavibali vya kusambaza (authorized dealers) kuna watu kama Mwanza Huduma ndio wasambazaji unakuta wanaleta cement Mwanza ndio kusambazia watu..., Sukari kuagiza nje mpaka vibali ndio maana hata kuna kesi ya Luhaga Mpina kuhusu watu wasiokuwa na experience ya hio kazi walipewa vibali..., kwahio kwenye hili tu umeonesha jinsi uelewa wako ulivyo limited..., Kuna watu ni authorized dealers wa kitu fulani katika nchi fulani wameshaingia mikataba kwamba hilo soko ni la mtu huyo wala hicho kiwanda hakitasumbuka kumuuzia mwingine, narudia tena hii ni karne ya information at your fingertips tumia muda kujielimisha

Hapo tu kwenye Picha ya huu uzi umeshaona kwamba minimum order ya kupewa kwa dollar sita ni units 1,000 sasa bila taasisi yenye uhakika wa consumption hii itakuwa a risky business....
nk

Usituletee ngonjera hapa za kijinga kanunue wewe lete kama hao wengine wanavyonunua factory price huko nje na kuleta hujazuiwa
Wengine ni kina nani ? Hivi hata unajua maana ya factory price ? Ngoja nikupe mfano hivi unadhani mfano Dangote na kiwanda chake cha Cement kuna wale wasambazaji ambao wamepewa contract unadhani kila mtu anaweza kutoa order kiwandani au watambwambia kamuone agent wetu sehemu fulani;
Kuna magenta wa majampuni ya kimataifa hata hapa Tanzania kibao wananunua bidhaa at ex factory price huko nje za kutosha nchi nzima na kutuletea
magenta na ex factory unamaanisha nini ? Na ukishasema agent ndio hivyo hao wana mkataba wa kusambaza sehemu husika hivyo tayari wameshaingia contract na wamepewa minimum order ya kusambaza kwahio huwezi tu kuwa agent bila kukidhi baadhi ya vigezo hususan kama kampuni ni kubwa...
Sio Big deal hiyo kalete sio wazo jipya waka kitu kipya labda uone kama umetoa bonge la Idea!!! Hamna kitu

Nenda kalete wewe kama unaona hiyo business ni viable na rate of return iko OK kwa vigezi vyote vya rate of Return iwe internal rate of return, capital etc sio Big deal
Narudia tena uelewa wako ni mdogo sana na hapa wala siongelei kwa manufaa ya mtu kupata faida kama mfanyabiashara bali kwa nchi kwa ujumla na wananchi kuweza kusave pesa zao na Kodi zao sababu kitu wanachopewa kina gharama zaidi wakati wangeweza kupewa kitu cha gharama kwa gharama nafuu na chenye ufanisi wa kutosha...

Kabla sijafika mbali nenda kaangalie ni nini maana ya Economy of Scale au ni jinsi gani Volkswagen (The Peoples Car waliweza kufanikiwa kutengeneza gari na kuuzia watu bei ambayo kwa kipindi hicho ilionekena haiwezekani....

Ukiwa na volume kubwa / wahitaji wengi na bei inapungua....
 
AGIZA GESI YA KUPIKIA HAPOHAPO ULIPO USIONDOKE KAA HAPOHAPO MTAANI KWAKO
Gesi zote zipo: Oryx Gas, Taifa Gas, Manjis Gas, O-Gas, Total Gas, Mihan Gas, na Puma Gas: zote zinapatikana hapo
 
Kwahio unanishauri mimi mwanakijiji nitumie hii badala ya Umeme ?

Ofcourse ki biashara na wewe kupata mkate wako upo sawa... lakini wewe kama daktari ambaye umejinasibu kwamba mambo ya Nishati unayafahamu..., Je unaona ni sawa umshauri mtu huyu wa kijijini (approx. 100/= kwa unit) atumie huo Mtungi

Mtungi mdogo wa Gesi wa Kilo Sita Net bei yake ni elfu 45 mpaka elfu 55
Nimecheki hii Induction Cooker direct from Factory huko China
Hata tukichukilia kwamba dollar moja ni elfu 2600 hii cooker inaweza kuwa na gharama ndogo kuliko hilo jiko tunalogawa bure kwa watu..., LAKINI kabla ya yote ngoja tuangalie matumizi

1kg ya Gesi = 13.6kwh (units)
Kwenye Mtungi wa 6 kgs (
ingawa gesi iliyopo kwenye mtungi sio 6kgs kutokana na uzito wa Mtungi)
Kwahio kwenye Mtungi wa gesi wa 6kgs kuna Units Ngapi

13.6kwh x 6 equals to approx = 81.6 Units
Kwahio Mtungi wa kilo 6 una Units takriban 81.6

Mtungi huu unajazwa kwa Tshs. 25,000/=; Hivyo tunaweza kusema Unit moja unanunua kwa 25,000/81.6 = 306.3
Kumbuka kwa sasa
  • Unit moja mjini unanunua kwa Tshs. 292 /=
  • Vijijini Unit Moja inanunuliwa kwa Tshs. 100/=
Kwahio mpaka dakika hii hilo jiko wanalopewa wanavijiji ni gharama kwa matumizi kuliko hata kupikia umeme

JIKO LA INDUCTION LINA UFANISI ZAIDI YA MARA MBILI MPAKA TATU YA GESI
Kwa mifano hapo juu; mtu wa kijijini atakuwa anatumia kwa bei rahisi zaidi kuliko mtu anayetumia hilo jiko la gesi kwa unit yaani wakati mwenye gesi anatumia Tshs. 306/= kwa unit; wa induction atakuwa anatumia Tshs. 33/= Yaani zaidi ya mara tisa

Nilishauri Tanesco iingie PPP na kampuni za Majiko na badala ya kuagiza wanaweza wakaya-assemble nchini

Soma Pia: Nishati Safi ya Kupikia (PPP tunayohitaji Kuingia)

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichanacho, Tufanye Tunachoweza

ALRIGHT

Maendeleo ya Kisasa ya Kitekinolojia na Utengenezaji wa vifaa vitumiavyo umeme, kama majiko umeme yenyewe --khasa haya ya Uambukizaji Moto-Umeme, ni mfumo ya ki-'uelektronishi mchangamano' zaidi kuliko ile namna ya 'Mfumo wa KiUmeme wa Kunyookea Njia tu'; yaani tuseme: si 'Linear System' kwa sehemu kubwa, utendaji wake unahusisha kujisoma na kujitathmini kwa ajili ya ufanisi na ubora wa kazi/fanusi yake .

Hili kiufundi, linatengeneza nasibu ya kuweza kujumuisha ndani ya mifumo ya umeme wa Jiko Ambukizaji Moto-Umeme, Induction Cooker, namna ya mifumo zaidi ya 'kujisoma', 'kutengeneza/jinereti data/code' na 'kutengeneza teminali' ya 'kiungo cha mawasiliano'.

Jiko Ambukizaji Moto-Umeme, hufanyakazi kwa kunururisha mawimbi sumaku-umeme kutoka kwenye kitako cha kupikia, jikoni; ambavyo chombo cha kupikia kinakuwa na kitako ambacho hugeuza mnururisho huo kuwa joto... Kanuni ni ile ile ya kama transfoma ya umeme inavyopata joto kutokana na vibati vyake 'kuchoma' kwa 'eddy currents'...

View: https://www.youtube.com/watch?v=pbwr73R6Ay8

SASA, mfumo wa sakiti ya J-I-M-U, kwa asili kabisa, unayonamna ya kujitathmini 'pumzi ya umeme-Voltage', na 'kasi ya kutiririka kwa mkondo wa umeme wenyewe-Current'; hivi viwili, kiufundi, vinatosha kujinereti 'data/code' kwa kuwa kizio ya ukubwa wa umeme--umeme unaonunuliwa tuseme kwa 'LUKU' ni zao la 'Pumzi (V) na Mkondo(I) na Wakati(T)' ambavyo 'Unit/Kizio' ni tumizi la 'Uelfu wa Zao la Pumzi na Mkondo kwa (Li)saa--KWh'.

Kwa kuzingatia, siku hizi utekinolojia Janja ni jambo linaelekea kuwa 'Standard/Kiwango cha Sifa ya Kukubalika kote kimanufaa'; kujumuisha mifumo ya hesabu na mawasiliano, computation&communication - ungamuzi na mawasiliano, si jambo gumu kwa chombo chochote... Vifaa vingi siku hizi iwe simu, iwe visikilizio vya kichwani, spika za bluetooth n.k huwa na mfumo wa kujisoma na kujitathmini matumizi yake ya umeme ili 'kutoa taarifa kwa mtumiaji'--khasa inapokuja suala la kumeneji 'chaji ya umeme' iliyobaki/iliyomo kwenye betri...

Jambo hili ni kitu kile kile kinachoweza kujumuishwa kwenye J-I-M-U basi ikaweza 'kuonana na LUKU' za majumbani kwa madhumuni ya kusawazishia 'reti/Kasi' ya kukatika/kuishia kwa kwa 'units'...

Ikiwa tunaweza kurekebisha mfumo wa LUKU kuhesabu na kuzipungumza 'units' za LUKU, kubuni/kujumuisha tekinolojia-janja, basi tunaweza kupangilia Mfumo wa LUKU uwe una 'viingizi viwili tofauti vya data za matumizi' ya umeme katika kaya ambavyo signali kutokea kwenye teminali ya J-I-M-U inachakatwa kwa reti ya makato iliyo ni tofauti na ile ya kawaida... Hii ina maana, kwa mfano, tunaweza kufanya kwenye kupikia 'Unit 1' iwe inakata/uthamani wa 'shilingi 10' na huku ya kawaida inakata 'shilingi 300'... Kwa dhana hii mtu/wanajamii wanaweza kutumia jiko la J-I-M-U kwa manufaa zaidi ya Kimazingira, Jamii na Uchumi huku wakinufaika na umeme unaozalishwa kiasi cha kutosha na vyanzo vyetu vya Nishati hii...

SASA, hili linaweza kushangaza kama si kuchekesha... Dhana yoyote inayofikiria kusambaza 'miundo mbinu kama mabomba ya gesi kote mjini na vijijini' haina chochote na kupambanishwa, ki-ugharimu wa manufaa, na hii 'Smart Technology--Tekinolojia Janja'... Sana sana watundu wa 'upembuzi yakinifu' wanaweza kuutumia mwanya wa 'jambo lililobado kufahamika' kupigia chepua 'conventional appliances--vifaa vya matumizi vyenye kutumika kwa makusudi hayo hayo'... Mambo ya gesi, na nishati jadidifu na 'utundu wote wa mashauri ya kitaalam/wataalam wanaoweza kurubunika'...

Majiko ya J-I-M-U yanaweza kutengenezewa muongozo wa viwango na basi vijana hata wa Kitanzania wakayatengeneza kwa kuyaunganisha na kuyauza--wakapata vipato na huku wakaiimarisha kada ya ufundi na tekinolojia. Hata namna ya LUKU za 'Smart Technology' daima ni uwezekano, ipo namna hata vijana wa kitanzania wakitengenezewa mazingira wanaweza kuziunda kwa kuziunganisha...

Fikiri tu kwa mfano, ikiwa simu yako Janja, wakati wowote inaweza kujisoma na basi ikakupa taarifa tuseme: kwa wakati huu, ni kioo chako kinatumia umeme mwingi kuliko 'app' yoyote ndani ya simu... Siri ya kujisoma hivi ni suluhu ya kimsingi ya karibia vifaa vyote vya kisasa--sembuse LUKU?​
 
Mfumo wa Smart Meter na Direct to Grid tayari upo kwahio tunaweza kununua tu huko na kuja kufunga wala hatuhitaji kubuni upya ndio maana nilishauri kila raia awe mzalishaji wa Nishati ya Umeme na kuawuzia Tanesco kwa yeye kupewa Credit...

Induction cooker ni nzuri sana, magnetic ni ajabu sana ukibandika sufuria zake ukiwasha tu maji yanaanza kuchemka😂😂 na ukiepua kile kitako joto limepotea
blood of jesus..haya ni majabu
 
Ni sawa tuu kwani gas ikiisha jiko ka gas unaweza kupika?
Tena hata kama jirani yako anauza gesi na ni mchana unaweza kuchukua mtungi huenda hauna hio 56 au 25 ya kununua mtungi wa gesi na ukizingatia gesi ni gharama ukilinganisha na umeme per unit hata kwa bei za dakika hii

Changamoto yake ni huu umeme wa mgao. Kuna siku wanaweza kukulaza njaa
 
Unakuwa na alternative zamani watu walipikia hata majiko ya mafuta ya taa yanaitwa ya mchina kama alternative lakini main cooking energy ilikuwa ni umeme
1734850453076.png

Cha maana ni kuhakikisha wasikate umeme na kuwekeza kwenye umeme uwe wa uhakika na sio kuendelea kutajirisha wengine kwa kununua Gesi / LPG kutoka kwao..., na hata ukisema mbona mafuta ya taa tunaagiza basi takwambia tunaweza kuanza kupikia gongo ambayo tunaweza kuzalisha (Ethanol) kama insurance wakikata umeme (lakini kwanini wakate, tuwape vigezo kwamba umeme ukikatika zaidi ya percent 2 kwa mwaka viongozi wote Tanesco Hawana kazi na wanakatwa mishahara...)
 
Niliwahi kutoa maoni na andiko zuri la kuimplement hii idea ya nishati safi kwa serikali kuwasaidia wananchi kwa kutengeneza mtambo wa biogesi . 1. Kushawishi kila familia kuwa na mifugo ya wastani kama kuku,ngombe ,nguruwe ambacho kinyesi kitatumika kutengeneza gesi ya kupikia , kisha familia itapata maziwa, mayai na kitoweo na end product itaenda kutumika kwenye bustani za mboga na familia itapata mboga ya majani .
Hivyo hapa tayari mwananchi anaweza kuwa amepata nishati safi isiyokuwa na ghalama za mara kwa mara labda marekebisho kidogo ha mfumo, mbili upatikanaji wa mboga na kupunguza udumavu kwa sera hii ingeleta tija zaidi
 
Hii inaweza ikawa best scenario kwa wakulima na wazalishaji ambao wana mabaki au muda na sehemu ya kufuga..., sababu ni sustainable na itachukua mabaki ambayo ni uchafu na unaweza kuharibu mazingira na kuubadilisha kuwa mbolea na nishati (perfect and sustainable) ila ile convinience na uzembe na uvuvi wa wanajamii as well as urbanization sio kila mtu atakuwa na sehemu ya kufugia wala sio kila mtu ataishi kijijini tunapoelekea hata maeneo yanaanza kuwa issue inabidi tuanze kujenga kwa kwenda juu..., Na katika andiko hili nimejaribu kuanisha njia tofauti za Nishati na Biogas ikiwemo

Ndio maana nikasema hata kwa wanaopanga chumba kimoja na hawa muda wa kufuga wao pia wanaweza kuingia katika usaidizi wa nishati safi na umeme ni convinient kabisa hata kwa mvivu ni kiasi cha kuwasha tu switch....

Wala hapa hakuna bure..., Huyu Bibi yangu na Babu yangu waliokuwa wanapikia vijikuni vya kuokota okota (bure) sasa hivi wanapewa mitungi na haya majiko bure ambapo wakijaza mara mbili tu ni sawa na bei ya hilo jiko au ni sawa na bei ya kununua induction cooker ambayo itakuwa na gharama ndogo (zaidi ya mara tisa) kuliko huu mkenge wanaoingizwa sasa hivi...

Ni kama drug dealer anakupa drugs bure mara ya kwanza akijua utakuwa teja....

Kumbuka tunapoelekea mkaa utapigwa marufuku
Sio tunapoelekea mkuu Mkaa tayari ni kama nyara maana hapa Dom nenda yadi ya Halmashauri wamkamata na kuyajaza kibao hadi wale wa vi soksi vya mkaa vimedakwa .
 
Niliwahi kutoa maoni na andiko zuri la kuimplement hii idea ya nishati safi kwa serikali kuwasaidia wananchi kwa kutengeneza mtambo wa biogesi . 1. Kushawishi kila familia kuwa na mifugo ya wastani kama kuku,ngombe ,nguruwe ambacho kinyesi kitatumika kutengeneza gesi ya kupikia , kisha familia itapata maziwa, mayai na kitoweo na end product itaenda kutumika kwenye bustani za mboga na familia itapata mboga ya majani .
Hivyo hapa tayari mwananchi anaweza kuwa amepata nishati safi isiyokuwa na ghalama za mara kwa mara labda marekebisho kidogo ha mfumo, mbili upatikanaji wa mboga na kupunguza udumavu kwa sera hii ingeleta tija zaidi
Asilimia kubwa ya maeneo ya vijiji maji ni tatizo kubwa mno ukiwawekea hizo biogas zitakufa ndani ya muda mfupi mnoo! Haiyata kuwa na tija.
Fikiri mtu.anajitwisha maji kichwani km 6-8 ili apate maji ya kunywa tu sasa yakutia katika mtungi au mtambo wa Biogas atatoa wapi.

Labda tumshauri kwanza waziri wa maji aandae bajeti ya kutosha kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Water saving indigenous skills kwa kila kijiji halafu tuvune maji ya mvua yanayo tiririka au kutemebea ardhini pale mvua inaponyesha.
Kwani maji yanayopotea bure ni mengi mnooo yangehifadhiwa mpango wa Biogas ungekuwa rahisi sana kwa kila nyumba.
 
Unauziwa jiko la gase la elfu 20, gase ikiisha unaenda umbali wa km 40 hadi 70 kujaza tena gase, nauli unatumia kati ya sh. Elfu 5 hadi elfu kumi. je,gharama hizo mwananchi wa kawaida ambae anashindia 1/3 ya milo kwa siku ataziweza?

Serikali iboreshe maisha ya wananchi kwanza kabla ya kuleta hizo nishati mbadala.
 
Wala hapa hakuna bure..., Huyu Bibi yangu na Babu yangu waliokuwa wanapikia vijikuni vya kuokota okota (bure) sasa hivi wanapewa mitungi na haya majiko bure ambapo wakijaza mara mbili tu ni sawa na bei ya hilo jiko au ni sawa na bei ya kununua induction cooker ambayo itakuwa na gharama ndogo (zaidi ya mara tisa) kuliko huu mkenge wanaoingizwa sasa hivi...

Ni kama drug dealer anakupa drugs bure mara ya kwanza akijua utakuwa teja....

Kumbuka tunapoelekea mkaa utapigwa marufuku
hili wimbi la ku-promote na kugawa majiko ya gas, naona ni vita vya makampuni ya gas, ni mapambano ya kuhodhi market share, kwa kisingizio cha envirnmental protection, na kuwapambania wanawake
 
Mtungi mdogo wa Gesi wa Kilo Sita Net bei yake ni elfu 45 mpaka elfu 55
Nimecheki hii Induction Cooker direct from Factory huko China
Hata tukichukilia kwamba dollar moja ni elfu 2600 hii cooker inaweza kuwa na gharama ndogo kuliko hilo jiko tunalogawa bure kwa watu..., LAKINI kabla ya yote ngoja tuangalie matumizi

1kg ya Gesi = 13.6kwh (units)
Kwenye Mtungi wa 6 kgs (
ingawa gesi iliyopo kwenye mtungi sio 6kgs kutokana na uzito wa Mtungi)
Kwahio kwenye Mtungi wa gesi wa 6kgs kuna Units Ngapi

13.6kwh x 6 equals to approx = 81.6 Units
Kwahio Mtungi wa kilo 6 una Units takriban 81.6

Mtungi huu unajazwa kwa Tshs. 25,000/=; Hivyo tunaweza kusema Unit moja unanunua kwa 25,000/81.6 = 306.3
Kumbuka kwa sasa
  • Unit moja mjini unanunua kwa Tshs. 292 /=
  • Vijijini Unit Moja inanunuliwa kwa Tshs. 100/=
Kwahio mpaka dakika hii hilo jiko wanalopewa wanavijiji ni gharama kwa matumizi kuliko hata kupikia umeme

JIKO LA INDUCTION LINA UFANISI ZAIDI YA MARA MBILI MPAKA TATU YA GESI
Kwa mifano hapo juu; mtu wa kijijini atakuwa anatumia kwa bei rahisi zaidi kuliko mtu anayetumia hilo jiko la gesi kwa unit yaani wakati mwenye gesi anatumia Tshs. 306/= kwa unit; wa induction atakuwa anatumia Tshs. 33/= Yaani zaidi ya mara tisa

Nilishauri Tanesco iingie PPP na kampuni za Majiko na badala ya kuagiza wanaweza wakaya-assemble nchini

Soma Pia: Nishati Safi ya Kupikia (PPP tunayohitaji Kuingia)

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichanacho, Tufanye Tunachoweza

Si kila mahali pana umeme, lazima uangalie cost comparison , availability na gharama za uendeshaji
 
Kwanini kila mahali hakuna umeme ?

Which is easier kutumia Kodi kununua fedha za kigeni ili kuagiza gesi nje ya nchi au kutumia Kodi zetu na misaada ya Nishati safi kuhakikisha kila mahali kuna umeme ?

Na JPM alivyosema kuunganisha elfu 27 wengi waliunganisha umeme je hilo ni bora au kufanya Laki tatu na ushee wengi wakose Umeme wakati tuna mpango wa kudouble capacity baada ya Bwawa ? ili nani atumie ?

Back
Top Bottom