Yes sababu induction inavyofanya kazi ni kupitisha umeme (alternating current) hivyo kutengeneza eddy currents kwenye sufuria ambazo zinatengeneza joto (kwahio sufuria lolote ambalo ni magnetic linafanya kazi)
Hapana hakuna kitu kinachoivisha kwa haraka (kupata joto instantly kama induction cooker), kwahio ukiweka temperature unayotaka unaipata instantly (hakuna device nyingine yoyote inayoweza kufanya hivyo) ingawa ukitaka ichukue muda ofcourse unaweza ukaweka temprature ndogo (kwahio inafanya kazi in all ranges of temperature
Capacity Power ya kitu ni Watts; mfano birika lako la kuchemshia maji linaweza kuwa 1500watts lakini likachukua sekunde kuchemsha maji wakati jiko lako linaweza likawa 100watts likachukua saa kuchemsha maji yaleyale..., kwahio mwisho wa siku umeme ukawa uleule..., Hapo juu mfano hio Induction cooker ina capacity ya 2000watts lakini huenda kupika kwako mchicha ukatumia 100 watts na uzuri zaidi wa kufanya hii kitu iwe na ufanisi wa mpaka 90 percent ni kwamba nishati haipotei, wakati wewe ukiwasha gesi yako kuna nishati inapotea kwa kuchemsha hewa kabla ya kuchemsha hio aluminium induction cooker ni magnetic hence inapiga kwenye chombo unachopikia pekee na ukizima joto linapotea instantly no wastage....
Hapa sijakuelewa kabisa.., ni sawasawa unasema mafuta yakiisha au gesi yako ikiisha hakuna kupika sababu hauna elfu 25,000 ya kujaza mtungi wako ? In short this is mute point..., badala ya kulaumu induction cooker kwa umeme kukatika labda ifike wakati tulaumu shirika kwa kukosa ufanisi (In short badala ya kulaumu tuhakikishe Tanesco inakuwa bora) Point yako ni kama unasema tuache kununua mashine za operation hospitali sababu zinatumie umeme na umeme unaweza kukatika
Kwanini ilipiga shoti (nadhani pa kuanzia ni hapo)
Tena kwa kusema kwako kwamba ilikuwa inatumia muda kupika huenda hata haikuwa induction cooker