Nisikilizwe nishauriwe ukweli mtupu nisije kujuta maisha yangu yote

kadogo2

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
3,278
Reaction score
5,212
Habari za muda humu

Nitasema ukweli Kama Kuna hukumu Basi nihukumiwe wote tunakosea Hakuna mkamilifu

Nachoitaji ni ukweli mchungu hata kama utaniuma ni sawa ilimradi nisiharibu maisha yangu maana Naona kama shetani amedhamiria kuniharibia maisha

Nimeshaleta story ya Kijana wangu wa kisukuma humu mkanishauri nikashupataza shingo

Huyu mwanaume tuna miaka 3 sasa tangu 2024 na Nina miezi 7 toka nianze kuishi nae..Tulikutana nikiwa na 24 yeye aliniambia ana 27( alinidanganya now ana 35)

Amenitoa nyumbani kwetu kanipeleka mkoa anaoishi yeye(kanda ya ziwa) ndugu zangu wanajua Niko nafanya kazi kumbe nimewekwa kinyumba na msukuma

Amenifungulia Biashara ninayoiendesha mwenyewe kwani aliniambia nitafute wazo la Biashara yeye ataniwezesha ametimiza inaendelea vizuri na yeye hausiki na chochote kwenye hiyo Biashara na ananihudumia vizuri

Changamoto
Tulikuwa na ugomvi mzito tangu mwezi wa 6 baada ya kugundua ana mke (amemlipia mahari wamezaa watoto wawili kwa msukuma ukishalipiwa mahari ni mke tayari)
Ukweli nimeumia sana maana sikutegemea Kama ningekutana na kitu Kama hiki
Lakini mwenzangu yuko kawaida kabisa Kama Hakuna kilichotokea anasema ni kawaida kwao kuoa mitala nitulie Mimi ndio mke mdogo yule atabaki kwenye nafasi yake Kama mke mkubwa na Hakuna anaeachwa

Hii hali inaniumiza Kila nikifikiri mekuaje nimejiingiza humo
Halafu yeye hajali yaani kama Hakuna kilichotokea

Sasa Kuna ex wangu nili soma nae shule tukaachana zamani hiyo kwasababu za umbali amerudi anataka kunioa nawaza nimuache tu huyu nirudi kwa ex au nikae nae tu hivyohivyo

Nishauriwe jamani msianze kunichamba na maneno ya kejeri 🥺🥺
 
IMG-20260613-WA0211.jpg
 
Kama kweli kaamua kukuoa, muambie akakutolee mahari na mfunge ndoa ya serikali au ya kimila.

Suala la kutoshtuka ni kawaida sana kwetu wanaume. Kwanza ukiona hajashtuka ina maana he knew what he is doing, na alikuwa ana hamu ujue ukweli wa mambo ili atue mzigo wa kuwaza.
 
Filisi ilo duka alilokufungulia alafu utembee zako binti wa miaka 24 unakubalije kizembe ivo kuolewa na mme wa mtu unajua ugumu wa uke wenza kweli?Hakuna raha kama kuwa na mume wako tu na sio uke wenza
 
Dah kumbuka ngosha kakupa mtaji lakini ukitaka ukaolewe huko ni sawa uko sahihi ila jitahidi sana muachane kwa amani kwa maridhiano sisi ni pipo, point yako kuu apo mueleze hukutegemea kaoa/ku share na mtu so mbanie hapo hapo mengine watajazia wanasaikolojia nguli humu.
 
Habari za muda humu

Nitasema ukweli Kama Kuna hukumu Basi nihukumiwe wote tunakosea Hakuna mkamilifu

Nachoitaji ni ukweli mchungu hata kama utaniuma ni sawa ilimradi nisiharibu maisha yangu maana Naona kama shetani amedhamiria kuniharibia maisha

Nimeshaleta story ya Kijana wangu wa kisukuma humu mkanishauri nikashupataza shingo

Huyu mwanaume tuna miaka 3 sasa tangu 2024 na Nina miezi 7 toka nianze kuishi nae..Tulikutana nikiwa na 24 yeye aliniambia ana 27( alinidanganya now ana 35)

Amenitoa nyumbani kwetu kanipeleka mkoa anaoishi yeye(kanda ya ziwa) ndugu zangu wanajua Niko nafanya kazi kumbe nimewekwa kinyumba na msukuma

Amenifungulia Biashara ninayoiendesha mwenyewe kwani aliniambia nitafute wazo la Biashara yeye ataniwezesha ametimiza inaendelea vizuri na yeye hausiki na chochote kwenye hiyo Biashara na ananihudumia vizuri

Changamoto
Tulikuwa na ugomvi mzito tangu mwezi wa 6 baada ya kugundua ana mke (amemlipia mahari wamezaa watoto wawili kwa msukuma ukishalipiwa mahari ni mke tayari)
Ukweli nimeumia sana maana sikutegemea Kama ningekutana na kitu Kama hiki
Lakini mwenzangu yuko kawaida kabisa Kama Hakuna kilichotokea anasema ni kawaida kwao kuoa mitala nitulie Mimi ndio mke mdogo yule atabaki kwenye nafasi yake Kama mke mkubwa na Hakuna anaeachwa

Hii hali inaniumiza Kila nikifikiri mekuaje nimejiingiza humo
Halafu yeye hajali yaani kama Hakuna kilichotokea

Sasa Kuna ex wangu nili soma nae shule tukaachana zamani hiyo kwasababu za umbali amerudi anataka kunioa nawaza nimuache tu huyu nirudi kwa ex au nikae nae tu hivyohivyo

Nishauriwe jamani msianze kunichamba na maneno ya kejeri 🥺🥺
Pole sana. Vumilia
 
Changamoto
Tulikuwa na ugomvi mzito tangu mwezi wa 6 baada ya kugundua ana mke (amemlipia mahari wamezaa watoto wawili kwa msukuma ukishalipiwa mahari ni mke tayari)
Ukweli nimeumia sana maana sikutegemea Kama ningekutana na kitu Kama hiki
Lakini mwenzangu yuko kawaida kabisa Kama Hakuna kilichotokea anasema ni kawaida kwao kuoa mitala nitulie Mimi ndio mke mdogo yule atabaki kwenye nafasi yake Kama mke mkubwa na Hakuna anaeachwa
Ulikutana na Tajiri la Katoro, tulia pesa zake si ulikula?
 
Sasa Kuna ex wangu nili soma nae shule tukaachana zamani hiyo kwasababu za umbali amerudi anataka kunioa nawaza nimuache tu huyu nirudi kwa ex au nikae nae tu hivyohivyo
Ila wanawake wa siku hizi, 24 yrs tayari Una Mabwana wawili? Na unataka kurudi kule uliko kuacha Kijana? Kama hapo hapo hata huyo Kijana X wako anataka kukutindua Tu akutupe kule aulize maumivu uliyompa ila ataoa Mwingine.
 
Life haitabiliki inatakiwa wewe utulie ufanye maamuzi ambayo utaona sahihi kwako na huta yajutia kama unampenda msukukua kaanaye tu mbona kwao kuoa wake wawili ni kawaida na hata kama mke wake akijua hatafanya kitu kama ni msukuma mwenye maadili
Na kama unaenda kwa ex wako achana naye kwa amani na mwachie kila kilicho chake hii itakufanya ukaishi kwa amani na ex wako wasikudanganye ety mfilisi then utenane naye ubaya ni akiba
 
Back
Top Bottom