Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
Kampuni namba 2 na namba 3 kwa utengenezaji wa magari nchini Japan baada ya Toyota, Honda na Nissan zinafikiria kuunganisha mitaji yao ili kuziunganisha na kuwa kampuni moja.
Lengo ni kuwasaidia kushindana dhidi ya watengenezaji wa magari ya umeme (EV), hasa nchini China. Huu utakuwa ushirikiano wa kimkakati kwa kampuni hizo mbili.
Mwaka huu mwezi Machi, Honda na Nissan walikubaliana kushirikiana katika EV, na Agosti wakikubali kufanya kazi pamoja kwenye teknolojia ya betri za EVs na teknolojia zingine.
Jarida la Nikkei la Japan pia iliripoti kwamba Nissan na Honda wanafikiria pia kuishirikisha Mitsubishi katika ushirikiano wowote unaowezekana. Mitsubishi bado haijajibu maombi yao.
Honda, Nissan na labda Mitsubishi zinafikiria kuunganishwa chini ya kampuni mpya baada ya kukabiliwa na kupungua kwa mauzo na ongezeko la gharama za uzalishaji.
Kampuni zote mbili, kama vile watengenezaji magari wengine duniani wasio Wachina, wametatizika katika soko la China lililokuwa kubwa zaidi duniani la magari. Wateja wa China waliokuwa wanunuaji wakubwa wa bidhaa za kigeni lakini kwa kiasi kikubwa wamehamia kwenye brands za ndani, ambazo zimeonekana kuwa na thamani zaidi nchini.

- Honda na Nissan wamepoteza 70% ya sehemu ya soko kubwa la magari duniani yaani China katika EVs kwa mwezi November peke yake
- Nissan ilisema kuwa mapato yake ya uendeshaji kati ya March na September yalipungua kwa 90% kutoka kipindi kama hicho mwaka uliopita
- Kuongezeka kwa matatizo ya kifedha na kimkakati ya Nissan katika miezi ya hivi karibuni kumeongeza uharaka zaidi wa ushirikiano wa karibu na Honda. Nissan ilitangaza mpango wa kuokoa gharama ya dola bilioni 2.6 mwezi uliopita kwa kupunguza nafasi za kazi 9,000 na 20% ya uwezo wake wa uzalishaji wa kimataifa, huku mauzo duni nchini China na Marekani yakisababisha kushuka kwa faida ya robo ya pili kwa 85%
Brands hizo mbili Honda na Nissan kwa pamoja mwaka 2023 ziliuza magari milioni 7.4 katika soko la dunia lakini zinakabili ushindani mkubwa kutoka kwa watengenezaji wa bei nafuu wa EV kama vile BYD, ambayo mapato yake ya robo mwaka yameongezeka, na kuwashinda Tesla kwa mara ya kwanza October 2024.
- Katika mwaka uliopita, vita vya bei ya EVs kati ya Tesla na BYD imeongeza shinikizo kwa kampuni kama Honda na Nissan kutafuta njia za kupunguza gharama na kuunganishwa ili kushindana nazo
"Mzunguko wa pesa za Honda unatarajiwa kuzorota mwaka ujao na EV zake hazijakuwa zikienda vizuri."
–Sanshiro Fukao (Executive fellow at Itochu Research Institute)
Japan auto industry ambayo ilionekana kutoweza kushindwa "unbeatable" inarudishwa nyuma kufuatia ushindani kutoka kwa China auto industry.
CREDIT: https://www.cnn.com/2024/12/17/business/honda-nissan-merger-talks/index.html
CREDIT: https://www.cnn.com/2024/12/17/business/honda-nissan-merger-talks/index.html