Nissan na Honda kuungana kufuatia ushindani mkubwa kutoka China katika utengenezaji wa magari

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
Kampuni namba 2 na namba 3 kwa utengenezaji wa magari nchini Japan baada ya Toyota, Honda na Nissan zinafikiria kuunganisha mitaji yao ili kuziunganisha na kuwa kampuni moja.

Lengo ni kuwasaidia kushindana dhidi ya watengenezaji wa magari ya umeme (EV), hasa nchini China. Huu utakuwa ushirikiano wa kimkakati kwa kampuni hizo mbili.

Mwaka huu mwezi Machi, Honda na Nissan walikubaliana kushirikiana katika EV, na Agosti wakikubali kufanya kazi pamoja kwenye teknolojia ya betri za EVs na teknolojia zingine.

Jarida la Nikkei la Japan pia iliripoti kwamba Nissan na Honda wanafikiria pia kuishirikisha Mitsubishi katika ushirikiano wowote unaowezekana. Mitsubishi bado haijajibu maombi yao.

Honda, Nissan na labda Mitsubishi zinafikiria kuunganishwa chini ya kampuni mpya baada ya kukabiliwa na kupungua kwa mauzo na ongezeko la gharama za uzalishaji.

Kampuni zote mbili, kama vile watengenezaji magari wengine duniani wasio Wachina, wametatizika katika soko la China lililokuwa kubwa zaidi duniani la magari. Wateja wa China waliokuwa wanunuaji wakubwa wa bidhaa za kigeni lakini kwa kiasi kikubwa wamehamia kwenye brands za ndani, ambazo zimeonekana kuwa na thamani zaidi nchini.

  • Honda na Nissan wamepoteza 70% ya sehemu ya soko kubwa la magari duniani yaani China katika EVs kwa mwezi November peke yake​
  • Nissan ilisema kuwa mapato yake ya uendeshaji kati ya March na September yalipungua kwa 90% kutoka kipindi kama hicho mwaka uliopita​
  • Kuongezeka kwa matatizo ya kifedha na kimkakati ya Nissan katika miezi ya hivi karibuni kumeongeza uharaka zaidi wa ushirikiano wa karibu na Honda. Nissan ilitangaza mpango wa kuokoa gharama ya dola bilioni 2.6 mwezi uliopita kwa kupunguza nafasi za kazi 9,000 na 20% ya uwezo wake wa uzalishaji wa kimataifa, huku mauzo duni nchini China na Marekani yakisababisha kushuka kwa faida ya robo ya pili kwa 85%​

Brands hizo mbili Honda na Nissan kwa pamoja mwaka 2023 ziliuza magari milioni 7.4 katika soko la dunia lakini zinakabili ushindani mkubwa kutoka kwa watengenezaji wa bei nafuu wa EV kama vile BYD, ambayo mapato yake ya robo mwaka yameongezeka, na kuwashinda Tesla kwa mara ya kwanza October 2024.
  • Katika mwaka uliopita, vita vya bei ya EVs kati ya Tesla na BYD imeongeza shinikizo kwa kampuni kama Honda na Nissan kutafuta njia za kupunguza gharama na kuunganishwa ili kushindana nazo​

"Mzunguko wa pesa za Honda unatarajiwa kuzorota mwaka ujao na EV zake hazijakuwa zikienda vizuri."
–Sanshiro Fukao (Executive fellow at Itochu Research Institute)

Japan auto industry ambayo ilionekana kutoweza kushindwa "unbeatable" inarudishwa nyuma kufuatia ushindani kutoka kwa China auto industry.

CREDIT: https://www.cnn.com/2024/12/17/business/honda-nissan-merger-talks/index.html
 
Waungane tu, biashara ni vita siku zote. Ila nawaona ni wapuuzi kama lengo/dhamira kuu ni kuunda EV, teknolojia ambayo wenzao wameshaanza nayo,

Ningekuwa mimi ndio mshauri wao basi ningewashauri EV iwe ni kama extra tu kwenye muundo mpya wa magari, ila kikubwa ni kuangalia/kubuni teknolojia mpya ambayo wengine hawana kabisa, maana kufanya kitu kipya ndio njia pekee ya kuteka soko na siyo kuunda kitu ambacho tayari kishakuwa exist
 
Kwa sasa huwezi kusema EV ni extra lazima kampuni zitengeneze demand yake inazidi kuongezeka si umeona Mchina anavyoexport

Ukitaka ujue hilo angalia mataifa ya Ulaya na Marekani wanajitahidi kuzipa ruzuku kampuni zao za ndani ili ziwekeze kwenye EV na kuzipa nafasi kampuni za Japan na South Korea kuinvest kwenye mataifa yao hasa upande wa EV batteries tech kucompete na Mchina

Tatizo la Wajapan ni very conservative wakishikilia kitu. Waliamini sana kwenye gari za ICE (Internal Combustion Engine) wakati Mchina alikuwa busy na purely electric na plug-in hybrid, finally Mchina kapindua meza

Hebu mfano angalia kampuni kama Toyota badala ya kuwekeza capital zaidi kwenye EV wao wako interested zaidi na Hydrogen engines huku akiweka nguvu kidogo kwenye electric.

Toyota asipokuwa makini hili litamcost kwenye long run, dunia inaenda kwenye purely electric na plug-in hybrid engines yeye anakomaa na hydrogen engines
 
Kampuni namba 2 na namba 3 kwa utengenezaji wa magari nchini Japan baada ya Toyota, Honda na Nissan zinafikiria kuunganisha mitaji yao ili kuziunganisha na kuwa kampuni moja.

Lengo ni kuwasaidia kushindana dhidi ya watengenezaji wa magari ya umeme (EV), hasa nchini China. Huu utakuwa ushirikiano wa kimkakati kwa kampuni hizo mbili.

Mwaka huu mwezi Machi, Honda na Nissan walikubaliana kushirikiana katika EV, na Agosti wakikubali kufanya kazi pamoja kwenye teknolojia ya betri za EVs na teknolojia zingine.

Jarida la Nikkei la Japan pia iliripoti kwamba Nissan na Honda wanafikiria pia kuishirikisha Mitsubishi katika ushirikiano wowote unaowezekana. Mitsubishi bado haijajibu maombi yao.

Honda, Nissan na labda Mitsubishi zinafikiria kuunganishwa chini ya kampuni mpya baada ya kukabiliwa na kupungua kwa mauzo na ongezeko la gharama za uzalishaji.

Kampuni zote mbili, kama vile watengenezaji magari wengine duniani wasio Wachina, wametatizika katika soko la China lililokuwa kubwa zaidi duniani la magari. Wateja wa China waliokuwa wanunuaji wakubwa wa bidhaa za kigeni lakini kwa kiasi kikubwa wamehamia kwenye brands za ndani, ambazo zimeonekana kuwa na thamani zaidi nchini.

  • Honda na Nissan wamepoteza 70% ya sehemu ya soko kubwa la magari duniani yaani China katika EVs kwa mwezi November peke yake​
  • Nissan ilisema kuwa mapato yake ya uendeshaji kati ya March na September yalipungua kwa 90% kutoka kipindi kama hicho mwaka uliopita​
  • Kuongezeka kwa matatizo ya kifedha na kimkakati ya Nissan katika miezi ya hivi karibuni kumeongeza uharaka zaidi wa ushirikiano wa karibu na Honda. Nissan ilitangaza mpango wa kuokoa gharama ya dola bilioni 2.6 mwezi uliopita kwa kupunguza nafasi za kazi 9,000 na 20% ya uwezo wake wa uzalishaji wa kimataifa, huku mauzo duni nchini China na Marekani yakisababisha kushuka kwa faida ya robo ya pili kwa 85%​

Brands hizo mbili Honda na Nissan kwa pamoja mwaka 2023 ziliuza magari milioni 7.4 katika soko la dunia lakini zinakabili ushindani mkubwa kutoka kwa watengenezaji wa bei nafuu wa EV kama vile BYD, ambayo mapato yake ya robo mwaka yameongezeka, na kuwashinda Tesla kwa mara ya kwanza October 2024.
  • Katika mwaka uliopita, vita vya bei ya EVs kati ya Tesla na BYD imeongeza shinikizo kwa kampuni kama Honda na Nissan kutafuta njia za kupunguza gharama na kuunganishwa ili kushindana nazo​

"Mzunguko wa pesa za Honda unatarajiwa kuzorota mwaka ujao na EV zake hazijakuwa zikienda vizuri."
–Sanshiro Fukao (Executive fellow at Itochu Research Institute)

Japan auto industry ambayo ilionekana kutoweza kushindwa "unbeatable" inarudishwa nyuma kufuatia ushindani kutoka kwa China auto industry.

CREDIT: https://www.cnn.com/2024/12/17/business/honda-nissan-merger-talks/index.html
Hata wa kiungana na toyota amna kitu
 
Nasubiria Mwigulu kwenye hotuba ya bajeti aseme, "serikali imeamua kuongeza Kodi kwenye Magari ya umeme ili kulinda viwanda vyetu vya ndani hasa gesi asili" makofi pwah, pwah, pwah kutoka kwa wabunge akina Musukuma, Mjagama, Shigongo, nk
 
Nimeona hii habari nimecheka sana. Hali mbaya. Japan wamechelewa EV, Toyota na Subaru muungano wao unasuasua.

Akili kaifanya Mazda kuungana na Mchina.
Mjapan Mazda kacheza kama Mjerumani Volkswagen naye ameamua kufanya joint venture na kampuni za Kichina FAW na XPeng kwenye Chinese EV tech
 
Kwa sasa huwezi kusema EV ni extra lazima kampuni zitengeneze demand yake inazidi kuongezeka si umeona Mchina anavyoexport

Ukitaka ujue hilo angalia mataifa ya Ulaya na Marekani wanajitahidi kuzipa ruzuku kampuni zao za ndani ili ziwekeze kwenye EV na kuzipa nafasi kampuni za Japan na South Korea kuinvest kwenye mataifa yao hasa upande wa EV batteries tech kucompete na Mchina

Tatizo la Wajapan ni very conservative wakishikilia kitu. Waliamini sana kwenye gari za ICE (Internal Combustion Engine) wakati Mchina alikuwa busy na purely electric na plug-in hybrid, finally Mchina kapindua meza

Hebu mfano angalia kampuni kama Toyota badala ya kuwekeza capital zaidi kwenye EV wao wako interested zaidi na Hydrogen engines huku akiweka nguvu kidogo kwenye electric.

Toyota asipokuwa makini hili litamcost kwenye long run, dunia inaenda kwenye purely electric na plug-in hybrid engines yeye anakomaa na hydrogen engines
Ila kama watafanikiwa kwenye hydrogen watatoboa. Materials za kutengeneza EV battery ni adimu na itafika muda zitakuwa ghali zaidi.
 
Miundombinu ya hydrogen ni ghali zaidi na safety ni ndogo

Hasa upande wa hydrogen leak inaweza kusababisha moto ni sawa na kucheza na bomu maana storage tanks, pipeline na valves zikivujisha tu tunazungumzia mengine au ikila mzinga

Hydrogen ilishafeli kitambo EVs won a long time ago

Toyota wabadilike waingie mazima kwenye EV na aendelee na ICE, najua Mjapan huwa anachukia kubadilika

Kila mwaka tangu 2010s Toyota kwenye media they say all types of things to keep the masses entertained kuhusu magari yao ya hydrogen na wamezindua matoleo kadhaa ya hydrogen lakini hayahuziki
 
Back
Top Bottom