Nitaifichaje hii aibu ili niweze kurudisha heshima yangu

Pombe huweka uhalisia wako. Hivyo pombe ilivyokufanya;ndivyo ulivyo.

Kufanya kosa si kosa bali kulirudia.
Iimetokea na huwezi kubadili yaliyopita.

Chakufanya; jitahidi usirudie tena.
 
Pombe huweka uhalisia wako. Hivyo pombe ilivyokufanya;ndivyo ulivyo.

Kufanya.kosa si kosa bali kulirudia.
I.etokea na huwezi kubadili yaliyopita.

Chakufanya; jitahidi usirudie tena.
Kwakweli siwezi kurudia tena
 
Tulishakubaliana kikaoni mnaokunywaga kahawa endeleeni na kahawa zenu msiguze ulanzi wala, kihambule wala wanzuki, hamusikii!

Ona sasa aibu kwa taifa watoto famili na wadada wa kazini kwenu
 
Kunywa Tena pombe alafu Anza jifanye unaanza kuwatopokea Kwa vitu vya akili nyingi.
 
Usifanye kitu kaa kimya kama hakuna kitu kilitokea
 
Inaonekana ulifanya vituko vya kawaida tu kuongea maneno ya hapa na pale ambayo si matusi... Watu wamekuchukulia kwa ukubwa sana kwasababu hawajah kukuona ukilewa au kusikia kama unakunywa pombe...
Chakufanya nakushauri jivike ujasiri, najua mna vikao vya kiofisi au idara basi kikitokea kikao chochote mwishoni wakati boss wako anataka kufunga kikao, muombe dakika 1 mwambie una jambo unataka kuchangia...
Akikuruhusu usiongee maneno mengi wewe sema "ndug zangu nashukuru kwa nafasi hii nipo mbele zenu kuwaomba radhi wale wote niliwakosea siku ile ambayo nilionja pombe nikajikuta naleta masihara yasiyo mazuri kwenu, naombeni mnisamehe sana, Asanteni..."
Baada ya kusema maneno hayo kaa chini na ukae kimya, ukitoka hapo endelea na maisha yako kama vile hakuna kitu umewah kufanya na kama vile hujawah ongea chochote ktk kikao... Na ikitokea mtu anakutania kuhusu siku uliyokunywa wewe kaa kimya usimbishie wala kukataa sana sana mwambie yalipita haina haja kuyarudia...
All in all Mungu akusaidie sana usirudie pombe...
 
Sisi walevi tuna kamsemo ketu "What happens in Vegas, stays in Vegas"🍻
 
Kausha, endelea na maisha kama hamna kilichotokea, yalinikuta sana hayo enzi nilikuwa nalewa
 
Ahsante mkuu kwa kunipa ujasiri angalau sasa naona ahueni and
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…