Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari zenu viongozi!
Ni dhahiri Tanzania inakwenda kuwa serikali tajiri. Serikali ambayo haitakuwa tegemezi kwa namna yoyote ile.
Kuna changamoto nyingi nchini katika sekta za afya, elimu, na uchumi.
Nikianzia sekta ya elimu , serikali itoe chakula cha mchana bure mashuleni. Huku msingi na sekondari ndiko wanakoandaliwa watumishi wa umma. Serikali ikizembea huku shule za msingi na sekondari itajikuta ina watumishi wenye uwezo mdogo na wasio wazalendo. Itavuna raia wenye ufahamu mdogo na wenye kukosa uzalendo.
Serikali iende mbali zaidi kwa kuondoa au kuwalipia ada wanafunzi wote wa vyuo vikuu.
Hizi kodi za uzalendo tunazokatwa kwa lazima zitatosha kufanya haya na mengine mengi.