Nitaitoa CCM peke yangu tu, kwa njia mbadala

Nitaitoa CCM peke yangu tu, kwa njia mbadala

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Nimeamua kuachana kabisa na harakati za kisiasa kwa nia ya kuitoa CCM. Nimeamua kuachana na njia za kisiasa kama kupiga kura, maandamano ya amani na mikutano ya kisiasa kwa sababu CCM haiheshimu maamuzi ya wananchi wengi kwa njia ya kura,au sauti za walio wengi. CCM wameamua kutumia nguvu za Dola kubaki madarakani.

Sasa nimeamua Mimi peke yangu kutumia njia ya MAOMBI, Mimi peke yangu nitakua namuomba Mungu wa Ibrahimu Isaka na Yakobo
Aitoe CCM madarakani kwa aibu na fedheha kubwa.

Aanze kuwatoa VIONGOZi wa CCM mmoja kila baada ya mwingine kwa muda mfupi Sana bila kuleta madhara kwa Taifa.
Mimi sio mlokole, Wala mtakatifu, lakini Ni Binadamu.

Na Mungu anasikia kila neno litokalo kwa kiumbe wake. Hivyo kwa imani bila kushirikiana na Watanzania wengine mimi peke yangu tu naweza,kwani Mungu katoa nafasi hiyo ya mtu yeyote kuweza kuomba na kujibiwa.

Mungu atajibu tu. Mungu anaona mateso yetu.
 
Jitahidi kabla yakuitoa isije kukutoa wewe na familia yako Mkuu.
 
Nilipoona "title" ya uzi tu, nikafikiri tumepata "Jerry Rawlings" wa Tanzania.

Anyway, kila la kheri mkuu
 
Jitahidi kabla yakuitoa isije kukutoa wewe na familia yako Mkuu.
Mimi naomba tu.
Tena kimyakimya.
Wala sipayuki.
Naomba nikiwa kazini,safarini,nyumbani,nikiwa natembea,kila sehemu.
Wala siombi maombi mareeefu hapa.
Maneno machache tu.
Kaa ukijua Mungu anasikia na anajibu aisee.
Hamta amini.
Mimi sio mchungaji,sio nabii,sio shehe,sio kasisi.ila Mungu hua ananijibu huwa nashangaa Sana.
 
Sasa nimeamua Mimi peke yangu kutumia njia ya MAOMBI,Mimi peke yangu nitakua namuomba Mungu wa Ibrahimu Isaka na Yakobo
Aitoe CCM madarakani kwa aibu na fedheha kubwa.
Wewe mpagani tu hakuna wa kukusikiliza
Unatakiwa umuombe Mungu wako sio wa wenzio wa watu wengine.

Wewe unataka umuombe wa Mungu wa Ibrahim Yakobo na Isaka huna wako wewe

Wa kwako yuko wapi? Kafariki dunia au huna kabisa pagani wewe
 
Wewe mpagani tu hakuna wa kukusikiliza
Unatakiwa umuombe Mungu wako sio wa wenzio wa watu wengine.

Wewe unataka umuombe wa Mungu wa Ibrahim Yakobo na Isaka huna wako wewe

Wa kwako yuko wapi? Kafariki dunia au huna kabisa pagani wewe
Sawa
 
AMINA. Nipo pamoja nawe najua wapo Watanzania wengi wapenda haki tupo pamoja kwa nia hiyo njema.
 
Hivi unajua Mungu ni wa wote wenye mwili eeeh!!!

Maana yake kila mwenye uhai na anapumua hata kama ni mtenda dhambi bado ni wake!!!

Na anawapenda wote, hasa wenye dhambi maana hutamani siku moja wamrudie yeye!!

Ndiyo, yaweza kuwa CCM ni watenda dhambi Sana!! Lakini wakiamua leo hii wamrejee Mungu wanasamehewa kimyakimya huku wakiendelea kukuongoza!!!

Pana tabu yake!! Usimkamie mwenye dhambi ukasema Atapigwa" kumbe mwenzio tayari Kesha tubu na kusamwhewa!!

Hapo ndipo Mungu anapobaki kuwa Mungu!!!!
 
Mkuu maombi yatafua dafu kwa huyu shetani?
39006645.jpg
 
Huyo ni Mungu wa wa Israel wa kwako yuko wapi? ungekuwa naye ungeshinda uchaguzi huna Mungu

una mashetani ya kibelgiji na ya akina Amsterdam
Huyo ni Mungu wa wa Israel wa kwako yuko wapi? ungekuwa naye ungeshinda uchaguzi huna Mungu

una mashetani ya kibelgiji na ya akina Amsterdam
Mimi Lee namfuata Mungu Mkuu,Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo.
Kwa kuwa aliagiza hivi
Enendeni Duniani kote mkafanye mataifa yote kuwa Ni wafuasi wangu.
Huyu Mungu ndiye ambae Kuna watu wanamdhihaki.lakini wanasahau kuwa Huwa hadhihakiwi.
 
Uyo mungu wako, kakuamuru uziheshimu mamlaka zinazo kuongoza.

Maana yake, Mungu kampa baraka zote Mh John Pombe, Magufuli kukuongoza.
 
Back
Top Bottom