Nitajibu swali lolote linalohusu ujenzi kasoro neno bei gani. Technical tu

Nitajibu swali lolote linalohusu ujenzi kasoro neno bei gani. Technical tu

Nitumie rangi gani nje kupaka ukuta ikiwa nimepaua kwa bati la kijani. Naona bati liko selective sana ku match na rangi ili nipate nyumba inayovutia?
 
Mkuu ni namna gani ya kudhibiti paa la mficho ie hiden roof lisivuje au maji yasishuke na kuta
Nikuwa na ditch nyingi....(contemporary roofing), au hiden roof kuna Aina mbili ya zege au ya bati. Ile ya zege haina shida kwasababu ukitumia recommended ratio M20 na ukingo wa 15-20mm nakuweka scheme za kupitisha maji na pipe zikakaa vizur au ukioona ngumu pia ongeza na tiles tatizo limeisha, kwenye PAA sasa imekuwa changamoto au zimekuwepo cases nyingi za kuvuja na ukwel kwamba tatizo liko kwenye SLOPE ( 30°) au arctan RISE/Run kuwa hamna au halipo. Cha kufanya :
1.weka slope towards short span,
2Weka matoleo ya maji piping (ditch) kwenye kuta angalau kila penye uwezekano wa kupokea maji.
3.Pembeni weka waterproof na hapa kuwa makini kuchagua nzur na ipo tech imeboreshwa Sana.
4.Hakikisha misumari ya bati hufanyi makosa na ikibidi seal it kwa grouting pia.
5.Paa liwe linafanyiwa usafi kila mara mvua zikinyesha ili kuondoka takataka (banking).
6.pia wakati wa kupigilia mbao (purlins), weka karasi ya nailon au kuna material sijuh kama huko yanapatikana hayapitishi maji. Basi utakuwa na uhakika wa kushinda tatizo Hilo. Hakikisha unaitumia vizuri hii kanuni A2+B2=C2 (2 ni exponent). Ili upate hypotenus sahii. Picha zinagoma kuwa attached..sor
 
Nitumie rangi gani nje kupaka ukuta ikiwa nimepaua kwa bati la kijani. Naona bati liko selective sana ku match na rangi ili nipate nyumba inayovutia?
Kwenye PHYSICS ya RANGI itategemea colour blind level ya mteja, (mapenz yake) Ila ktk matching naweza kuwa siko sahii kabisa ila kumbuka kuna RANGI ya kijani pia kama unataka chemistry nzur japo nikiangalia hizo (RANGI za wasanii hizo na njano), Ila unaweza kwenda kwa wazalisha RANGI wakakutengeneza unayotaka (CUSTOMIZED PAINT) . japo kwa TZ broken white ya KIBOKO inaonyesha kumatch na MAPAA mengi.
Kumbuka kusoma mazingira ya nyumba yako ndo uchague na RANGI pia.. NYEUPE ina dharau Sana..ukiwa mchafu basi.
 
Nitajibu swali lolote linalohusu ujenzi kasoro neno bei gani. Technical tu

Structure, design and building economic.

Kuna nafasi ndogo ya kujenga ukuta, lakini pia umahitaji mtaro kupitisha maji ya mvua hadi kwenye mitaro ya jiji? Ukuta wa aina gani utafaa hapa?
 
Kuna nafasi ndogo ya kujenga ukuta, lakini pia umahitaji mtaro kupitisha maji ya mvua hadi kwenye mitaro ya jiji? Ukuta wa aina gani utafaa hapa?
Ingawa hili linaitaji "kuona site nature", pia naitaji kujua hayo maji ya mvua yanatokana na Paa kukusanya maji pamoja na mvua yenyewe (kama ndio), je pia kuna slope/mtelemko au nikulazimisha Chanel?. Hapa zingatia hivi:
1.Msingi wa ukuta ni Bora zaidi ukitumia zege na si tofari au tumia mawe kama yanapatikana na uwe angalau 230mm. (Msingi, hafu hakikisha unakuwa juu ya level ya ardhi.(ground level).60cm.
2.Weke matundu kwenye msingi (Bomba ili kupitisha maji ya chini ya ardh(rain water)
3.weka GUTTER (zile bomba za kukusanya maji kwenye PAA ili yawe na uelekeo mmoja unaweza yavuna au unaweza yaelekeza uelekeo mmoja.
4. Weka mtaro ( excavate trench),V-shape au trapezoidal shape ili maji yasiwe yanatuama kwa muda ili iwe inapeleka maji nje ya ukuta.
5.Weka ukuta tofari 150mm au 6" na unaweza kwenda hata urefu wa 2m.
NOTE: ukuta kazi yake sio usalama bali kizuizi (obstraction not for security).
 
Je, white cement inaweza tumika Kama water proofing kwenye uezekaji(contemporary roofing)?
 

Nitajibu swali lolote linalohusu ujenzi kasoro neno bei gani. Technical tu

Structure, design and building economic.
conductor latika ujenzi nyumba ya kuishi ghorofa moja nimeona kuna mafundi wanamwaga jamvi, wengine hawamwagi jamvi kitaalam hii imekaaji?
Vilevile kwenye nguzo za jengo hilohilo la ghorofa moja kwenye nguzo huweka nondo 4 za 16mm. Na wengine huweka 6 za mm 12 kitaalam hii imekaaje pia?
 
labda km upo Ktk Majiji ama Miji mikubwa, lkn ktk Halmashauri zetu hz, kila kata inakuwa na Mtu wa Idara ya Ujenzi wa Halmashauri husika... huyu ndo "SNITCH" wa yale Maandishi "BOMOA" ... "SIMAMISHA UJENZI" ... mtafute huyu Bwana mapema kisha MALIZANA NAE... Anza ujenzi wako, hutaona Mtu wa Halmashauri wala Idara ya Ujenzi
Ahsant kwa ushaur
 
Chumba kimoja na choo mkuu Cha kisasa. Vyenye ukubwa wa wastani wa vyumba vya kawaida kabisa, huwa unakula kias Cha tofali ngapi -MSINGI?
 
Kwa Nyumba ya contemporary ili isiwe na joto natakiwa kujenga tofali ngapi (kozi ngapi) toka kwenye msingi mpaka kwenye Lenta(bim)?
 
Je, white cement inaweza tumika Kama water proofing kwenye uezekaji(contemporary roofing)?
Sishauri Sana, Kwan hazitofautiana Sana na ORDINARY CEMENT..kwa uwezo wa kustahilimili kuvuja, Ila ipo special cement au tafuta grouting type ingine ziko kwenye maduka
 

Attachments

  • FB_IMG_1695995797967.jpg
    FB_IMG_1695995797967.jpg
    105 KB · Views: 25
conductor latika ujenzi nyumba ya kuishi ghorofa moja nimeona kuna mafundi wanamwaga jamvi, wengine hawamwagi jamvi kitaalam hii imekaaji?
Vilevile kwenye nguzo za jengo hilohilo la ghorofa moja kwenye nguzo huweka nondo 4 za 16mm. Na wengine huweka 6 za mm 12 kitaalam hii imekaaje pia?
1.nyumba inajengwa kwa hatua,hivyo hatua ya jamvi mwaga jamvi, nenda hatua ya pili...Ila kwenye gorofa kuna njia mbili za kujenga, unaweza kuanza na frame(only column)au ukajenga kwa whole structure.
B. 4@16mm au 6@12mm nondo
Wote wanaweza kuwa sawa au hapana, (endapo nitaona structural design). Ila nitaka vizuri hapa, sifa kubwa ya NONDO nikwamba ni imara kupambana na kupanuka/kurefuka (strong in tension and weak in compression). Ndo maana inaongezewa materials yaliyo imara katika compresion katiko joto flani), i.e penye nondo kuna uimara kuliko pasipo na nondo(Nondo ina tabia ya buckling na sio expansion), na jengo lolote uzito wa mzigo upimwa kwa N/mm2 (yaani kwenye milimita za mraba /ujazo kiasi gani nondo itaweza kuvumilia KUBEBEA MZIGO, hivyo nondo upimwa kwa kilo inazokwenda KUBEBA katika mzingo flan, Kuna percentage inavyotakiwa kwa kiwango cha chini 0.8% cho CHUMA kwenye Mzingo mmoja ya eneo la NGUZO.yaan Kama NGUZO inakuwa na ujazo 500kg/m 3 basi 0.8% iwe CHUMA, (hapa panaitaji nguvu kiasi kuelewa), nondo inanunuliwa kwa kilo sio kwa urefu au unene...japo unene unachangia kilo kuwa nyingi na mzigo kuwa mchache...hivyo ukutumia 16mm basi na nondo unaweza tumia bar bending schedule tofauti na ukitumia 12mm. Cha msingi eneo limechukua kilo ngapi za CHUMA .
 
Kwa TZ, kibari cha ujenz kinatolewa na ALMASHAURI huska, kwenye IDARA ya ujenz, KAZI kubwa ya IDARA ya ujenzi inayokuwa na watu 2 muhimu ni msanifu majengo (architecture) na mhandisi majengo (structure engineer). cha Kwanza wataomba uonyeshe yafuatayo:
1. Hati ya kiwanja /mmiliki
2. Mchoro wa jengo(structural design)
3.Usanifu wa jengo(architectural design)
Na michoro hiyo lazma iwe na mhuri wa aliyepitisha ubora,
Baada ya hapo watapanga kuja kutembelea eneo na QS wao au afisa mipango miji
badae utapata kibari cha sasa unaweza kujenga na watakwambia ulipie gharama za kibar cha ujenz, nadhan huwa unalipa kwa eneo linalokwenda kusimama jengo (, Square metre).BAADA YA HAPO UNAWEZA KUTAFUTA MTAALUM WAKO NA UWEKE KIBAO CHA KUONYESHA KUNA UJENZI.
Na itakulazimu sasa kwasababu ni orofa kibao kinachoo yesha :
1. Aina ya jengo
2.Mteja
3.mkandrasi wa jengo
4.mkandras wa umeme
5.mkandras wa mifumo mingine kama ipo .
Kazi kwako...

1. Msanifu majengo anaitwa "architect" na sio "architecture".

2. Una kitu lakini uandishi wako sio mzuri. Andika kama mtaalamu na sio kama unachat na mtu facebook/whatsapp.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
1. Msanifu majengo anaitwa "architect" na sio "architecture".

2. Una kitu lakini uandishi wako sio mzuri. Andika kama mtaalamu na sio kama unachat na mtu facebook/whatsapp.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
Nashukuru kwa USHAURI, kiswahili kigumu, ninayo andika we umeyasoma kwa Kiswahili ulipokuja kugundua nina kitu?. Be more positive acha tabia za ualimu..Anza uzi wako tutajifunza pia boss
 
Mkuu ili kuepuka kuta kupata fungus ni kipi cha kuzingatia wakati wakuanza ujenzi...!?
Na kipi hupelekea kuta za block kupata crack wakati mwingine hata jengo halijaisha...!?.
 
Mkuu ili kuepuka kuta kupata fungus ni kipi cha kuzingatia wakati wakuanza ujenzi...!?
Na kipi hupelekea kuta za block kupata crack wakati mwingine hata jengo halijaisha...!?.
A.Mara nyingi fungus husababishwa na vitu Zaid ya KIMOJA, ikiwa pamoja na asili ya ardh (kama maji yanatuama eneo hilo kwa masika tofauti, au ubora wa material unayotumia cement (manufacturing date and quality, au mchanga unaiotumia (kama sio river sand), unachumvi chunvi , au Uhahi wa tofari kufika mwisho na endapo hutafanya plastering kubufasaha.
Pia kingine cha msingi hakikisha tofari limekomaa (cure). na Lina ratio mzuri.

B.Crake ni Somo Pana kwenye ujenz Kaka (Mpaka wasomi wanatengeneza thesis za PhD kugundua Sabab). kuna Aina nyingi za crake (Hairline,shrinkage, settlement and structural) Ila moja ina sababu za kutokea, Ila Kwa mujibu wa SWALI lako kiko chanzo linawesa anzia mmojawapo ya hizo Aina za crake,ama msingi haukuwa imara na haukupewa muda wa kufanyiwa analysis au fundi katika "bonding" (jinsi amavyopanga tofari) akawa amekosea, materials ubora ..lakini pia wakati mwingine ni natura factor eneo huska kama lina pitiwa na tetemeko, au kuna Miti imesambaza miziz eneo hilo mfano Mharobaini ni mimea mbaya Sana kusababisha crake..nk
 

Attachments

  • Screenshot_20240206-105030.png
    Screenshot_20240206-105030.png
    232.9 KB · Views: 17
Nitajibu swali lolote linalohusu ujenzi kasoro neno bei gani. Technical tu

Structure, design and building economic.
Mkuu mimi Napenda nyumba yangu niezeke bati za vigae,lkn jamaa zangu wananishauri kuwa nisizitumie hizo Kwasababu eti ni rahisi kuvuja.Vipi kuna Ukweli hapo?.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Asante, mfano ninaplan ya kujenga nyumba ya vyumba vinne vya kulala ila sina huo uwezo kwa sasa, sasa nataka kujenga vyumba viwili vya kulala, jiko na toilet, je itawezekana hapo baadae kuunganisha vyumba vingine katika nyumba ya kwanza? ubora wake utakuwaje?
Inawezekana Hamna shida.. fundi wako Aache matoleo.
 
Back
Top Bottom