Nitajie Rais wa Africa aliyefanikiwa kudhibiti nchi kwa kuwa mlaini/mpole mpole (polite)

Nchi kama China,Russia,Germany hazikuendelea kwa kubembelezana,Josep Stallin,Mao Zedong,Adolf Hitle,huwezi kuacha kuwataja hawa watu ukiongelea maendeleo ya hizo nchi 3 nilizozitaja,

But Dunia imebadilika,kiongozi yeyote yule aongoze kwa mujibu wa sheria na atakayepatikana na hatia ahukumiwe kwa mujibu wa sheria na kusiwe na ile kubembelezana,wahujumu uchumi,wala rushwa,Wezi na makosa mengine makubwa wahukumiwe adhabu kali.
 
Hata Lincoln, A hakuwa mpole. Kwa taarifa yako ndiye aliyeendesha vita dhidi ya waliotaka kuitenga Amerika na akafanikiwa akiwa na Kamanda wake General Grant!
Vita ni uamuzi wa kitaifa dhidi ya waasi wanaotaka kuligawa taifa (uhaini). Usilinganishe na uamuzi binafsi wa kuzuia uhuru wa habari, demokrasia na kuwa na vikundi vya wasiojulikana kuteka, kutesa na kuua wakosoaji nje ya mfumo wa katiba na sheria za nchi.
 
Ramaphosa
 
Una maana gani unaposema mpole?. Maana ukali unaweza kumaanisha ukosefu wa hekima. Ukali unaweza kumaanisha kutaka kuwa juu ya wasaidizi wako muda wote hata katika masuala ya weledi ambayo wameyasomea na wanayafahamu kukuzidi.

Ukali unaweza kumaanisha maamuzi ya pupa tu yanayoitia hasara nchi yako kwa maana ya matumizi mabaya ya kodi ya wananchi yanayoambatana na hicho unachoamua.

Ukali unaweza kukosa hekima na ukataka kila mtu afikirie kama unavyofikiria, Upole ukizidi ni mbaya kwa hao wanaoongozwa lakini ukali unaambatana na dhuluma, udhalimu, uonevu na mabaya mengine ya viwango hivyo.
 
Africa Africa tu hapa mnaleta uzungu tu Africa kumejaa na kunanuka rushwa na ubinafsi utendaji mbooovu inahitajika nguvu kubwa kutawala Africa
 
Pia kufoka ni dalili ya matatizo binafsi ya rais husika. Kutaka kuogopwa kunaambatana na hiyo tabia.

Ni inferiority complex ya tangu utotoni anayokuwa nayo huyo rais. Wengine wanakuwa na unyonge kwa maprofesa na wanajeshi na ni unyonge wa huko walipokulia.
 
Ahahahahah!
 
Kudhibiti uhalifu wa kisiasa na kijamii kunahitaji kuwa na mifumo inayofanya kazi hakuhitaji mtu anayetumia nguvu kubwa na wakati huo huo akiumiza tabaka la watu wa upande mwingine bila ya sababu ya msingi.

Rais ni wa wote na busara ya kawaida tu inapaswa imkumbushe kuwa ni mtumishi wa kila mtu akianza kupendelea kundi fulani kwa makusudi anakuwa analiumiza kundi lingine kwa makusudi hiyo hiyo.
 
Unamaanisha kudhibiti ni kufanyaje, kuua? Kudhulumu watu mali zao, kuwa Rais mkatili kama Magufuli?
 
Ukali unasaidia pale ambapo mhusika anakuwa mtenda haki asiye mwizi. Mf nyerere. Usimlete yule2 jambazi muuaji hapa,. The nightmare of tz
 

Mwingi amewahi ongoza nchi gani Afrika?
 
Hizo ni katiba nzuri kwa jinsi walivyoona wao sio lazima ifae kwetu.ila pia inawezekana kupitia katiba hizo ndizo zilizopelekea wewe kujua kuna huo ufisadi.Ni mjinga peke yake ndiye atakayeogopa nchi kua na katiba bora itakayowajibisha na kujisimamia.
 
Kibaki alikua mkali? Mbona Kenya ilipaa kiuchumi kuliko hata utawala wa dikteta Moi
 
Mbona Bashite na Sabaya hawakutimuliwa kwa aibu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…