Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Me ......jina "Y" .....25/11

Ke ...... jina "A" ......16/8 ...

Status : uchumba sugu
Rakims
 
Mi ni mwanaume herufi I tarehe 26/06 na mke Ni heruf M tarehe 15/08
 
Uwongo tu,hii ni aina nyingine ya kupiga ramli au Mazingaombwe,Anayejua hatima yangu na mke wangu ni MUNGU tu,lkn sio huu usanii.
Yani Astrology ni wasanii? huna ulijuwalo hapa duniani.

Hivi kila kitu mpaka uambiwe na paroko wako aliyekushika akili?

Unaelewa wale mamajusi walikuwa ni watu gani? Waliiona nyota ya mashariki masiha amezaliwa wakaenda kumsujudia na kumpa zawadi ya mavumba, dhahabu ubani na manemane.

Swali unawajuwa mamajusi ni watu gani? Kwa kukusaidia anzia Google kabisa halafu ndio urudi hapa.
 
Me 17 January herufi C
Ke 21 April herufi E

Mimi ndio Me
Kwa mtizamo hapa unaonekana wewe na yeye mnaendana kwa asilimia 90 kwa maana ni watu wenye kuendana kiasili ya nyota zenu nyote ni udongo ambapo wewe ni udongo wa pwani na yeye ni mchanga wa fungu hivyo ni watu mnaendana vizuri na pia kindoa mnaingia katika mlango wa 12 yaani ni mlango uliojaa fungo na siri kwako utanufaika sana ukiwa nae na ufuatao ni uchambuzi wenu:

Yeye anaonekana kuvutiwa na makusudio yako katika mahusiano yenu na wewe unafurahia zaidi utulivu wake na upendo kwa ujumla anapokuwa na wewe hujihisi yupo juu na kufarijika zaidi na huvutiwa zaidi na mutikio wako wa mambo yake jinsi unavyokuwa unamakinika nae anajihisi kwako wewe kapata na hata kama bado hajaanza kuonyesha hilo.
Nyote mnashauku sawa za kiardhi na asilia kimwili hisia za pamoja mnakuwa mnaenda vema. Yeye kwako anakuwa kakamatika zaidi kihisia na hujihisi muda wote kwenye mapenzi yeye ni mgeni na wewe ni mwenye kumpokea vema. Pia wivu kati yenu sio tatizo sana kuoneana wivu kwa ziada nyote ni wenye kupenda pesa na ulinzi wa mapenzi hasa kupenda kuwa pamoja pamoja ni watu wenye kutizamia kama wamoja wenye nguvu moja na msiogawanyika mna maelewano ya muda mrefu na mmoja wenu akisema kitu kaelewa basi ni jambo hutoka moyoni nyie wawili ni wenye maridhiano makubwa.

SEHEMU YAKE YA HISIA:
Sehemu zake za hisia ni shingo na koo ndio maeneo ambayo kuna hisia zake kubwa za kiwazimu ikiwa;- utagusa eneo hilo,kumbusu na kutomasa eneo hilo hata kama umekaa nae basi utampandisha kwa kasi sana hisia zake na hasa ukiwa umekaa karibu nae ukawa unamgusa hapo chochote unachosema kinaingia kwenye akili yake na roho yake moja kwa moja kuhusu wewe.

Ukimbusu eneo hilo vizuri na kumng'ata kichokozi akiwa kalala chali na kwenye koo lake basi utaona maajabu.
Fanya mbinu hii pia itakuongezea umaarufu kwake

Mfanyie massage hii ili kuweza kumfanya siku yake yote ajihisi yupo kwenye raha:

(1)Akiwa kalala kwa mgongo wake muwekee mitetemo kwenye shingo yake karibu na mizunguko ya masikio yake kwa kutumia vidole vyako tumia miondoko ya taratibu sana kwa maana sio punda huyu kama kina fulani huyu anataka vitu sensitive rudia hivyo hadi uone vipele vimesimama kwenye mikono yake. (Be very
gentle kuzunguka sehemu ya pipe za hewa kwenye shingo vinginevyo utamniga).

(2) Kumbuka ni mtu mwenye kupenda zaidi kufanyiwa hivyo akiwa kalala kwa tumbo lake hivyo fanya hivyo hadi kukaribia eneo la muunganiko wa uti wa mgongo lakini usitoke nje ya shingo maana umeme utakatika halafu ataona unamtembezea wadudu.
Ukianza kuona vinyweleo vimesimama na vipele basi jua chini hali si shwari wacha niishie hapa na Ramadhan hii nisije nikafanya mambo magumu masaa yamebaki machache.

Ikiwa utamgusa au kumfanyia manjonjo sehemu za shingo yake basi ni mtu mwenye kupata hisia za kiwazimu na wewe eneo lako kubwa la hisia ni maungio yote ya mwilini ikiwa atakupatia sehemu hizo vizuri kama hamjafunga ndoa basi utataka itokee kesho.

Rakims
 
Mpuuzi wewe
Yani Astrology ni wasanii? huna ulijuwalo hapa duniani.

Hivi kila kitu mpaka uambiwe na paroko wako aliyekushika akili?

Unaelewa wale mamajusi walikuwa ni watu gani? Waliiona nyota ya mashariki masiha amezaliwa wakaenda kumsujudia na kumpa zawadi ya mavumba, dhahabu ubani na manemane.

Swali unawajuwa mamajusi ni watu gani? Kwa kukusaidia anzia Google kabisa halafu ndio urudi hapa.
Asante mkuu kwa kunisaidia kujibu hawa watoto waliogeuza bange chakula badala ya starehe.
 
Mimi wakiume 30/08 jina linaanza na H na ke ni 26/01jina linaanza na i

Sent from my Infinix X606C using JamiiForums mobile app
Sawa mkuu kwa mtizamo unaonekana ni mtu mwenye mwenendo wa mchanga mwekundu na yeye ni upepo wa kimbunga kwa mtizamo huu tu ni watu ambao hamuendani lakini nitakufafanulia hapa kwa ziada maana mnaendana kwa asilimia 28 tu.

Nyote mnaonekana ni wenye busara na mko vema kiakili na ni wenye mtazamo wa upendo katika mwanzo mwanzo. Wito wake na mawazo pamoja na mitazamo yake hukuona huwa unachukulia poa na rahisi rahisi tu. Pia nyote kila mtu ana mitizamo yake tofauti na mwenzie na pia wewe ni mtu mwenye tahadhari sana kwake linapokuja swala la kuonyesha hisia zako nae fikra zake huwa mbali sana na mawazo yake pia ni mtu akiwa na wewe hata ukiongea anakuwa anawaza vitu vingine yeye anakuwa ni mwenye kuvutika na watu tofauti na wewe na hata ukimuuliza interest zake zinakuwa ni tofauti zaidi kutoka kwako yaani vigezo vyake unakuwa hukidhi. Wewe ni mtu unaonekana mwenye kujitafutia mambo yako na mwenye kutaka kufanikisha yako unayo yataka wewe na kujihifadhia pesa.
Lakini yeye anakuwa ni mtu wa kuwaza na kumaliza muda wake katika ubunifu,maono, na hujiona kama Bikira amehifadhiwa, mwenye busara,
na kuonyesha vitendo sana kuhusu matamanio yake.
Kama unawaza kuwa nae kindoa acha mawazo hayo unapotea na vile vile hata urafiki tu kwenu kuendana hakuna.

SEHEMU YAKE YA HISIA;
Sehemu yake ya hisia zaidi ni supu za miguu na ankles. Gusa,papasa,tomasa au mbusu sehemu hizo basi ukifanya hivyo utaona hisia zake zinapanda kwa kasi na anakuwa radhi hilo ni eneo nyeti sana kwake na wengine wao hupenda kusafishwa miguu saloon hivyo Kugusa,
kusugua, kupapasa, au kumbusu sehemu hii ya mapenzi ya anatomia kwa kiasi kikubwa humuamsha hamu ya tendo.
mfanyie kumbembeleza kifundo cha mguu, kusonga hadi supu kama massage laini, na uone jinsi anajibu haraka.
Wanamaji hupenda kuwa na miguu ya chini na vifundo vyao vya miguu vilivyotiwa ujazo mfano mguu wa bia hupenda pia mchezo wa kumwagiwa maji miguuni.

Kama hatua ya awali ya kufanya mapenzi, mpe massage nzuri ya miguu. Tumia vidole vyako au kucha, na na uwe kama unampatia ganzi kiasi
utaona analalama kwa upole. Anza kwenye vifundo vya miguu, na ueleze polepole duru kuzunguka mfupa wa kifundo cha mguu.
Mpake mafuta kwenda juu kwa taratiibu hadi eneo lote la nyuma uone mguu umelegea Wakati wa kufanya mapenzi, jitahidi kushika miguu yake na kuifanyia mitelezo utaona anazidi kutoa sauti za mahaba na mawadah.
japo kuwa hamuendani hii inaweza kukusaidia kwa nafasi kubwa kuweza kumkamata.

Rakims
 
Mkuu nini maana ya hio milango
Unaweza kuisoma kwenye thread yangu hii
 
Karibu mkuu kwa mtizamo wake mume:

Mume 7 June
Mke 26 November

Kwa mtizamo huu huyu bwana mdogo anaonekana kuwa na huyu binti wanaendana kwa asilimia 95 yaani pea yao imekaa vizuri sana na kuna maisha ya mapenzi na ndoa hapo yenye heshima,amani na upendo kwa maana huyu bwana ni Upepo wa juu na huyu binti ni upepo wa nyasi hivyo wanaendana vizuri hawa mkuu. nao watafunga ndoa ya amani na yeye kukubarika mtizamo wao upo hivi;
Hawa wawili ni kama hasi na chanya na kulia na kushoto au ni kama jengo lenye nguzo mbili wanaendana na wanamvuto kwa kila mmoja wenye kani ya sumaku na ni wenye fikra na akili moja na mawazo ya pamoja kwa pamoja wanaonekana ni watu wenye kukubaliana kwa mitizamo ya kila mmoja kwa mwenzie na wote huchangia pamoja maelewano yao na ni wenye utulivu katika upendo wao.
Binti huelekea kuwa ni mwenye akili zaidi na bwana ni mtu wa watu pia wote hawana utulivu wakikutana na hupenda kubishana bishana kwa upendo na wote ni wenye kupenda uhuru na kupeana uhuru. ijapokuwa wanaweza kutokuridhishana kwenye tendo lakini ni wenye kupenda kufundishana na kuambiana kila mmoja vile anavyotaka kwa kuwa ni wenye maelewano hufikia kuiokoa ndoa yao kwa kila tatizo linapowaijia hawa ni wenye kukutana kwa usalama na hata ikitokea wameachana basi huachana kwa usalama.

Kwa kuwa ni wanao haina umuhimu wa kukutajia sehemu zao za hisia.

Ke ni 7/3 herufi H..Me ni 8/6 herufi R
 
Mimi ni mwanamke ninayeuliza
Nimezaliwa 17/6 jina langu linaanzia na M
Yeye 27/4 jina linaanzia na J
Mahusiano, wanandoa.
 
Back
Top Bottom