Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Baina ya nyie wawili wewe ni Moto wa nyasi na yeye ni Maji ya kisima kwa maana hii yeye atavutiwa zaidi kwako kulingana na nguvu yako ya utafutaji wa maisha, na vile vile wewe utavutiwa nae zaidi kwa mtizamo wake wa kiimani na mambo ya kiroho.

Ukweli ni kwamba katika mahusiano wewe unahitaji mwenza ambaye ni kama mshkaji na yeye anahitaji mwenza ambaye ni kama mwenye ndoto za mapenzi yaani mapenzi muda wote mfano mwanaume wa ndoto zake nyote wawili hamuendani kwa maana kati yenu hakuna anaeweza kumsaidia mwenzie katika mahitaji yake

Asili yako ya roho ya uthubutu na kujitoa utakuta inakwamishwa sana na yeye ambaye ni tegemezi zaidi kwako na uoga wake pia

Yeye ambaye huwa na hisia kali sana muda wote hata kuona unamapenzi nae zaidi ya kumtaka akutimizie haja zako kingono tu, vile vile atakuona ni mtu ambaye hujatulia mambo mengi na vile ulivyo ni mtu wa kupenda uhuru basi moja kwa moja utajiwekea akilini kuwa huyu ni wa kuwa nae tu kwa muda kisha utatafuta mwingine lakini mahusiano yenu taratibu huanza kuzama mfano umemwaga maji kwenye mchanga kila mtu ataangalia uelekeo wake. ndio ndoa hizi mara nyingi watu wanakuwa pamoja ajili ya kuangalia matumizi na watoto tu lakini ni ndoana.

Rakims
Duh ngachoka kabisaa[emoji24]
 
ME
30/01 Jina K.

KE
17/03 Jina A.

Hasa upande wa fedha na ndoa.
 
Msaada kidogo

ni kwann yanapotokea magomvi hasa ninamkosea mimi mkewang huw nakutan na badluck , Niliwah pat ajar tukiw kwenye ugomv kuibiw pkpk, juz nimebamiz gar nyuma ?
Inategemea na daraja alilonalo mkeo kiroho ama pia inategemea na imani yako ilivyo kwake

Rakims
 
True aisee ila mm sio mchepukaji km yy
Kila mwanadamu ni mwenye kuijua nafsi yake na mwenye kujijua zaidi this is public network naheshimu kinga yako ya kujilinda na heshima yako lakini ukweli utabaki kuwa ukweli mkuu.
 
Me: 7/5 - H
Ke: 31/3- A
Wawili nyingi ni watu ambao hamuendani hata kwa fikra tu kwa maana utawala wa Punda ukiisha ndio unaingia utawala wa Ng'ombe.

Kwanza kabisa wewe sio mtu wa kukurupuka na mshapu kama ilivyo kwa yeye,

Lakini wote wawili mnaonekana kuwa wenye hisia sawa katika kufanya mapenzi.

Yeye ni mwenye mihemko na wewe ni mwenye hisia, nyote wawili ni wenye kufurahia wakati jambo linaendelea.

Tabia yako ya kumtawala mwenza wako moja kwa moja itamfungua kukasirika kwake kwa maana hawa Punda asili yao ni kama ushanga wa dukani ukiugusa tu. Hivyo mtajikuta ni wenye makelele kwenye masuala ya pesa kwa maana wewe una asili ya kuwa na ulinzi wa pesa kitu ambacho yeye kitamuonyesha kuwa una asili ya ubahiri hali ya kuwa yeye ni mwenye ubadhilifu na matumizi ya moto kwenye pesa akipata pesa inayayuka kama moto, na jinsi anavyofanya maamuzi basi moja kwa moja utakuta kwako ni kero.

Ambaye wewe sio mwenye kupenda mambo ya haraka na mabadiriko ya haraka. Mahusiano yenu ya kuvutia mwanzo lakini baadae hugeuka kuwa ndoa Ngumu sana.

kuna siku mtu atakuja kupiga mtu na hadithi itaishia hapo.

Rakims
 
ME:27.12 E
KE: 26.12 J

Hapo mkuu vp...
Asili yako ni watu wenye kukubali watu kama wao, hivyo kwa nyie wawili mnaendana sawa nyota kitu kinachopelekea kuwa ni watu wenye kutokukoseana heshima na kuwakilishana,

Nyote wawili ni wenye tahadhari, wenye kujiheshimu na wenye kufanya kazi kwa bidii na kupenda kutunza akiba. Lakini hata wenye nyota sare mara nyingine wanaweza kuwa na changamoto.

Nyie ni wenye kuendana kingono ama tendo la ndoa inategemea na state ya mahusiano, Lakini katika masuala mengine kila mmoja ni mwenye kusababisha mwenzie kuwa na huzuni na mwenye kukata tamaa,

Kati yenu hakuna anaeweza kumpumzisha mwenzie hata kupumzisha tu nywele yake ukimaliza hili linakuja hili,

Mkiwa ni wa kuhusiana tu yaani mahusiano ya kawaida tu kama mtu na hawara yake kila mtu ana mambo yake mtaona mpo sawa japo sio sawa kabisa kupitiliza. Safari ya mapenzi yenu kadri inavyosogea mbele ndivyo inavyozidi kuwa kwenye mteremko mkali saa yoyote mapenzi yanakufa unabaki ujamaa.

Rakims
 
Habari zenu wana ndoa na wenye ndoto za ndoa,

Yawezekana umewahi kusikia kauli maarufu sana inasema;
"Kosea yote usikosee ndoa"

Katika thread hii nitakupa maana halisi na siri iliyojificha nyuma ya kauli hiyo hivyo ukiweza kunitajia tarehe yako na ya mwenza wako na herufi zenu za mwanzo,mchumba,mpenzi na mwanandoa nitakupa taarifa zako na zake na siri zake kimapenzi hivyo utakachojua hapa ni kitu kitakachokusaidia kuimarisha mahusiano yenu au kuyaharibu kabisa.

View attachment 2185484

Yafuatayo nitakutajia;
  • Tabia zake
  • Sehemu yake ya hisia
  • Jinsi ya kumfanya azidi kuwa karibu na wewe
  • Mtizamo wake kwako
  • Mtizamo wako kwake
  • Unachopenda akufanyie
  • Udhaifu wake
  • Na vingine vya ziada
MATOKEO:
Kwa asilimia 90 nitakayokwambia ni ya kweli kama sivyo basi kuna mmoja kati yenu alidanganya tarehe kwa mwingine,

MFANO WA KUANGALIZIWA
Ili niweze kukuangalizia vizuri andika hivi;

Mimi mwanaume Jina langu (Herufi ya kwanza);
Nimezaliwa tarehe: 14 December mwaka
Mwezi wangu Jina lake (Herufi ya kwanza)
Kazaliwa tarehe: 24 April mwaka

(Kisha unaweza kusema upande gani nikazie zaidi japo sio lazima)

MEMBER WA KWANZA
Ke 24/4 P

Me 14/12 E

Matokeo yake:

MTIZAMO WAKO KWAKE;

Wewe ni mtu mwenye tabia za maji na yeye ni mtu mwenye tabia za udongo kwa mjumuiko huu unaonyesha kabisa nyinyi kuendana ni vigumu na hata kama mnapendana vipi itakuwa dhoruba tu ndani.

Kwa mtizamo anaonekana yeye ni mtu wa kupenda utawala na ukubwa kwa kuongoza mambo/kupelekesha- ambapo wewe unaonekana sio mtu wa kupelekeshwa na hautakubali hilo.

Pia, wewe ni mtu wa kuhitaji mabadiriko,anuwai,matukio ambapo hayo humfanya yeye kujihisi tofauti na wewe kwa kuwa yeye ni mtu wa ambaye hujifanya ni mjuaje na incharge wa mambo yanavyokuwa yanakwenda katika miliki yenu na kujiona ni mtawala mzuri wa tabia za nyumbani na hujiona ni mwenye hekima na heshima na imani zaidi kuliko wewe. Yeye anakuwa ni mtu wa kutaka kufanya mambo ambayo teyari yana uhakika na kutaka kufanya mambo yenye uhakika, wakati wewe unakuwa upo teyari kufanya chochote kinachowezekana.

Na pia wewe ni mtu wa kusema chochote kinachokujia na nimtu wa kumdondoshea maneno tu randomly yanayokujia kichwani kwa fikra yako ambayo humfanya kuanza kujawa na hasira taratibu. Pia kuna tatizo la pesa katika mahusiano yenu, hiyo ni sababu wewe unataka kuzalisha pesa kwa yanayowezekana leo hali ya kuwa yeye anawaza kuhusu mambo ya kesho (ukifa unaniachaje). Mna muda mfupi sana kwenye mahusiano yenu.

MTIZAMO WAKE KWAKO:
Mapenzi yenu yanaweza kwenda kama tu ataweza kujikaza vizuri kuwa na wewe au kukuvumilia kwa maana mtizamo wake kwako wewe ni mtu ambaye huvumiliki. wote mnavutiwa zaidi kwa muonekano wa mwenzi wake, kwa tamaa zake yeye alizonazo katika kufanya tendo anakuwa anavutiwa zaidi na ufanyaji wako.

Lakini ni mtu inamuwia ugumu katika kuvumilia tabia yako ya kupepesa macho na kutizama mambo mapya(wanawake wa nje) wewe ni mtu wa kuchukulia kila jambo poa poa na rahisi rahisi inapokuja katika maswala ya mahusiano na tendo la ndoa wakati yeye ni mtu muda mwingi anataka kuwa serios kwenye mahusiano na kutawala. hali ya kuwa wewe ni mtu ambaye hutaki kutawaliwa kimapenzi na mtu yoyote hakuna baya kwenu lakini ni watu wenye kupishana mara kwa mara uhawara kwenu inakuwa ni starehe kuliko ndoa. maana mnaweza kukaa kwenye uhawara miaka ila mwezi tu ndoa ikawa ndoana.

Mahusiano yenu ya ndoa yatakuwa ni vichekesho tu.

SEHEMU ZAKE ZA HISIA:
Sehemu zake za hisia ni shingo na koo ndio maeneo ambayo kuna hisia zake kubwa za kiwazimu ikiwa;- utagusa eneo hilo,kumbusu na kutomasa eneo hilo hata kama umekaa nae basi utampandisha kwa kasi sana hisia zake na hasa ukiwa umekaa karibu nae ukawa unamgusa hapo chochote unachosema kinaingia kwenye akili yake na roho yake moja kwa moja kuhusu wewe.

Ukimbusu eneo hilo vizuri na kumng'ata kichokozi akiwa kalala chali na kwenye koo lake basi utaona maajabu. Fanya mbinu hii pia itakuongezea umaarufu kwake. Mfanyie massage hii ili kuweza kumfanya siku yake yote ajihisi yupo kwenye raha:

(1)Akiwa kalala kwa mgongo wake muwekee mitetemo kwenye shingo yake karibu na mizunguko ya masikio yake kwa kutumia vidole vyako tumia miondoko ya taratibu sana kwa maana sio punda huyu kama kina fulani huyu anataka vitu sensitive rudia hivyo hadi uone vipele vimesimama kwenye mikono yake. (Be very gentle kuzunguka sehemu ya pipe za hewa kwenye shingo vinginevyo utamniga).

(2) Kumbuka ni mtu mwenye kupenda zaidi kufanyiwa hivyo akiwa kalala kwa tumbo lake hivyo fanya hivyo hadi kukaribia eneo la muunganiko wa uti wa mgongo lakini usitoke nje ya shingo maana umeme utakatika halafu ataona unamtembezea wadudu.
Ukianza kuona vinyweleo vimesimama na vipele basi jua chini hali si shwari wacha niishie hapa na Ramadhan hii nisije nikafanya mambo magumu masaa yamebaki machache.

Ikiwa utamgusa au kumfanyia manjonjo sehemu za shingo yake basi ni mtu mwenye kupata hisia za kiwazimu na wewe ikiwa atajua kucheza na mapaja yako yako basi ataweza kukupeleka mbali sana kihisia hisia zako siwezi kukwambia sana kwa maana wewe unamtizamia yeye.

UTAMVUTIA VIPI:-
Yeye kwanza sio mtu wa papara ni mtu anapenda kama ni utafiki ama mahusiano basi yaanze taratibu kama vile unajenga nyumba mapenzi kwake anataka uanzie msingi kwanza hivyo inakutaka kuwa ni mtu mwenye subira kuweza kummudu kimapenzi na subira wewe muda mwingine ni kitu huwa,

Mbinu;
kwanza kabisa kama ndio unaanza nae basi hakikisha kuwa unakuwa ni mtu wa kwanza kumtafuta na usiende nae kwa pupa kama hujagusa katika kujifanya ni mtu mwenye subira sana basi moja kwa moja hutampata kwa maana kama ni wa dada wazamani huyu atakwambia nisubiri miezi 9 nikufikirie.

Muonyeshe kuwa upo radhi kuwepo muda wote pale anapokuwa anakuhitaji na ujionyeshe kuwa wewe ni mtundu mtundu. Yeye hupenda mtu anaekuwa taratibu taratibu na kama unaweza kumsababisha kucheka cheka basi huna muda mrefu unayoyataka utapata. Pia utaanza kumuona nae ni mtu anautundu utundu na kupenda utani utani na anapenda mtu mwenye kumvutia kwa yale anayoyafikiria akilini kwake yaani unatakiwa kujipendekeza kuuliza unataka niwe vipi?

Tabia zake za kero ndogo ndogo ni mategemeo yake uzifurahie na ujifanye kucheka anapoongea upumbavu au jambo lisilo na maana kwako.

Na kama akisema kwa utani ukajibu kwa utani basi moja kwa moja anakufungulia moyo wake na kuona hakuna mtu kama wewe duniani hapa na anaweza kukuganda kama kupe pia utani wa kimwili kama kumgusa mwili na kumminya minya ni vitu anapenda kama ni mke wako basi jaribu leo hata akinuna ukifanya hivyo anakaa sawa. Ni mtu kama unataka kumtoa basi anapendelea sehemu za hadhi ya juu kidogo na anapenda sehemu anayoenda kuwe kuna watu wanaojua nini wanafanya hasa wapishi. Mnunulie kinyaji kisichokuwa na kilevi ndio mapenzi yake kama sio mlevi lakini kama ni mtumiaji basi utakuta ni mpenzi wa wine.

Mazingira ya nyumbani ukimpikia hata chochote tu hujihisi special sana na hataskia la mtu kuhusu wewe valia mavazi ya kupika unapomuandalia chakula na hakikisha muonekano wako uwe ni safi mfanyie hivyo hata mara moja kwa mwezi utaanza kuona anatoa machozi

Ikiwa mazungumzo yanachelewa basi jitahidi asikushinde kimaongezi na wala usikwame katika kuzungumzia mnayoyapenda hasa akianza kuongelea pesa muhimu tabaka hili ni mwanamke mwenye kupenda pesa na kuigiza hajali pesa.

Pia tengeneza account mbili tatu za bank ili akitizama aone kabisa ni mtu mwenye kushughulika na mambo ya saving hata kama huna pesa atatambua ukipata utatunza.

Usihodhi mazungumzo. anapoanza kuzungumza usimkatishe na usiwe mzembe katika kutoa sifa akifanya kitu hata cha kipuuzi nyumbani,kwenye gari yake,mapambo ni watu wenye kupenda kusifiwa wanapofanya mambo madogo.

Rakims
1/1(A )vs 15/9(B)

Rakims fanya jambo
 
Me 17/10 P
Ke 4/4 A
Wakati nyie ni rahisi kwenu kuvutika kila mmoja kwa mwenzie, ndivyo hivyo hivyo mvutano kutokea haraka na migongano,

Wewe unaonekana ni mwenye kutafuta furaha na amani, wakati yeye asiyependa utulivu na mwenye kupenda fujo anatafuta changamoto na ulimwengu mpya ajili ya yeye kutawala.

Wewe utamuona yeye kama ni mtu asiye na adabu wala busaras;

Yeye anafikiria wewe ni hopelessly na usiyekuwa teyari kupambana na uhalisia.

Yeye anataka anahitaji kujisikia huru lakini anataka uaminifu usio na shaka kutoka kwa mshirika wake,

na hawezi kukusamehe pale unapokuja kushindwa kufanya uamuzi wa kujitolea kwake.

yeye mwenye shauku pia hukasirishwa na hisia zako duni yaani kushindwa kumletea drama.

Kimwili maelewano ni ya ajabu na mazuri kwa muda,

lakini baada ya hapo nini?

Rakims
 
Mimi KE tarehe 17/1

Yeye ME 11/5
Kwa mtizamo hapa unaonekana wewe na yeye mnaendana kwa asilimia 90 kwa maana ni watu wenye kuendana kiasili ya nyota zenu nyote ni udongo ambapo wewe ni udongo wa pwani na yeye ni mchanga wa fungu hivyo ni watu mnaendana vizuri na pia kindoa mnaingia katika mlango wa 12 yaani ni mlango uliojaa fungo na siri kwako utanufaika sana ukiwa nae na ufuatao ni uchambuzi wenu:

Yeye anaonekana kuvutiwa na makusudio yako katika mahusiano yenu na wewe unafurahia zaidi utulivu wake na upendo kwa ujumla anapokuwa na wewe hujihisi yupo juu na kufarijika zaidi na huvutiwa zaidi na mutikio wako wa mambo yake jinsi unavyokuwa unamakinika nae anajihisi kwako wewe kapata na hata kama bado hajaanza kuonyesha hilo.
Nyote mnashauku sawa za kiardhi na asilia kimwili hisia za pamoja mnakuwa mnaenda vema. Yeye kwako anakuwa kakamatika zaidi kihisia na hujihisi muda wote kwenye mapenzi yeye ni mgeni na wewe ni mwenye kumpokea vema. Pia wivu kati yenu sio tatizo sana kuoneana wivu kwa ziada nyote ni wenye kupenda pesa na ulinzi wa mapenzi hasa kupenda kuwa pamoja pamoja ni watu wenye kutizamia kama wamoja wenye nguvu moja na msiogawanyika mna maelewano ya muda mrefu na mmoja wenu akisema kitu kaelewa basi ni jambo hutoka moyoni nyie wawili ni wenye maridhiano makubwa.

SEHEMU YAKE YA HISIA:
Sehemu zake za hisia ni shingo na koo ndio maeneo ambayo kuna hisia zake kubwa za kiwazimu ikiwa;- utagusa eneo hilo,kumbusu na kutomasa eneo hilo hata kama umekaa nae basi utampandisha kwa kasi sana hisia zake na hasa ukiwa umekaa karibu nae ukawa unamgusa hapo chochote unachosema kinaingia kwenye akili yake na roho yake moja kwa moja kuhusu wewe.

Ukimbusu eneo hilo vizuri na kumng'ata kichokozi akiwa kalala chali na kwenye koo lake basi utaona maajabu.

Fanya mbinu hii pia itakuongezea umaarufu kwake
Mfanyie massage hii ili kuweza kumfanya siku yake yote ajihisi yupo kwenye raha:

(1)Akiwa kalala kwa mgongo wake muwekee mitetemo kwenye shingo yake karibu na mizunguko ya masikio yake kwa kutumia vidole vyako tumia miondoko ya taratibu sana kwa maana sio punda huyu kama kina fulani huyu anataka vitu sensitive rudia hivyo hadi uone vipele vimesimama kwenye mikono yake. (Be very
gentle kuzunguka sehemu ya pipe za hewa kwenye shingo vinginevyo utamniga).

(2) Kumbuka ni mtu mwenye kupenda zaidi kufanyiwa hivyo akiwa kalala kwa tumbo lake hivyo fanya hivyo hadi kukaribia eneo la muunganiko wa uti wa mgongo lakini usitoke nje ya shingo maana umeme utakatika halafu ataona unamtembezea wadudu.

Ukianza kuona vinyweleo vimesimama na vipele basi jua chini hali si shwari wacha niishie hapa na Ramadhan hii nisije nikafanya mambo magumu masaa yamebaki machache.

Ikiwa utamgusa au kumfanyia manjonjo sehemu za shingo yake basi ni mtu mwenye kupata hisia za kiwazimu na wewe eneo lako kubwa la hisia ni maungio yote ya mwilini ikiwa atakupatia sehemu hizo vizuri kama hamjafunga ndoa basi utataka itokee kesho.

Rakims
 
Back
Top Bottom