Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Na haitaondoa ukweli kuwa wewe ni Mpumbavu kunilingania mimi hali ya kuwa wewe ni kafiri jilinganie wewe kwanza.
Ukishatakata ndio ulinganie ukoo wenu, ukisha takata ndio ulinganie, mkeo,na ndugu zako wote kisha wananchi wenzio. Kisha watu wasiojulikana kisha Member wa jamii forums kisha duniani na kwingine kote ila mimi niache na upotovu wangu... Maana ni bora kuwa mpotovu kuliko kusikiliza mjinga..

Imagine umekaa na kichaa unamsikiliza. ndio mimi nikae nakusikiliza wewe eti unaharamisha nyota unahalalisha zinaa halafu kwa upumbavu wako umeziba profile ili akili yako ilivyofinyu sasa hivi unaanza kukataa ili kutoa ushahidi wewe ni mdogo sana kimaarifa mdogo wangu Mpumbavu. Badirika You playing yourself like solitaire

Yani unataka kuwaaminisha watu wewe mtakatifu wakati ni kafiri kufurah Neemah

Rakims
Ninachokiona ni ww kutumia ad-hominems tu badala ya kuona nimeuweka wazi ushirikina unaoufanya.

Hakuna sehemu nimehalalisha zinaa, kufanya zinaa no tofauti na kuhalalisha zinaa...ukifanya zinaa unakuwa umefanya miongoni mwa madhambi makubwa ambayo hayamtoi mja katika uislam..ila ukihalalisha zinaa unakuwa umetenda Kufr inayokutoa katika uislam. Kaa chini usome misingi ya aqeedah sahihi ya uislam.

Allah amesema kuwa hasamehi dhambi ya kushirikishwa ila anasamehe mengine yasiyokuwa hayo madhali mja ametubia . Ukifa na itikadi yako hiyo ya uchawi na ushirikina (horoscope) unakufa hali ya kuwa upo nje ya uislam.

Btw, hakuna sehemu niliyosema au kujifanya mimi ni mtakatifu,am just a sinner like everybody else but i am not mushrik like you .

Tubia kwa ALLAH na uache ushirikina wako.
 
Katika mahusiano haya mnaonekana ni wawili msioendana hasa ukizingatia kwamba yeye ni mchanga wa bahari na wewe ni Upepo wa kimbunga;

Unaonaje dhoruba ikitokea kando ya bahari?

Hayo ndio mahusiano yenu yalivyo mkiunganisha roho,

yeye atajikuta anakuona wewe ni mtu usiyeweza kumtabiri, na wewe utajikuta ni mtu ambaye unashindwa kwenda na yeye kirahisi hadi utumie nguvu nyingi,

Mbinu zake za kawaida tu za kukuendea hata katika kuomba mchezo utakuta kwake ni kero kubwa sana na atakuona kama vile muda wote wewe ni mwenye kumtibua tu mwanzoni utaona kama anakuvumilia lakini baadae sura kamili ya dhoruba itaonekana.

wewe hujiamini katika kujieleza kimtizamo wako bila maneno.

Na yeye hujiamini katika kujiheshimu bila mipaka, mawasiliano yenu kila mmoja atajikuta haeleweki kwa mwenzie na pia ataona kama anaaibika na kudhalilika kwa mwenzie.

wewe utakuta ni mtu wa kupenda mitoko na yeye utakuta ni mtu wa kupenda mtu mwenye kumaintain maisha ya nyumbani wewe ni mtu mtafutaji yeye atafurahishwa kwa utafutaji wako mwanzo kwa kufuata mkumbo lakini baadae itakuwa too much hata kama utamletea maigizo sasa hivi lakini baadae visafari vya kwa ndugu jamaa na marafiki huwa havikatiki.

wewe vile ni mpenda uhuru, safari ya mapenzi yenu itakuwa ngumu sana na uvumilivu wako kwake ni mdogo wewe unataka mtu mwenye nyota ya moto wa mkaa ambaye wewe ukimletea habari za kutoka unakuwa kama umemtia hamasa.
Hakika wewe ni mwenye kupenda kutoka sasa akitaka kukufunga funga kwa maisha yake ya siasa kimbunga kitazunguka kisha vumbi lako litapeperuka na kubaki umemvuruga.

Nyie mnapendeza zaidi kuwa ni wenye urafiki tu na hata mapenzi yenu mara nyingi huishia kirafiki tu.

Rakims
Yaani haya masuala yako ya horoscope unapelekea watu wavunje ndoa zao wakiamini kuwa nyota zao haziendani....ama kweli Quran imesema kweli kuwa nyinyi wachawi mmejofunza uchawi kwa ajili ya kufarakanisha mke na mume (Ndoa) ili waachane wakiamini kuwa hawaendani ili mumrahisishie kazi baba yenu iblis

Al-Baqarah 2:102

وَٱتَّبَعُوا۟ مَا تَتْلُوا۟ ٱلشَّيَٰطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَٰنَۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَٰنُ وَلَٰكِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ كَفَرُوا۟ يُعَلِّمُونَ ٱلنَّاسَ ٱلسِّحْرَ وَمَآ أُنزِلَ عَلَى ٱلْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَٰرُوتَ وَمَٰرُوتَۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَآ إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِۦ بَيْنَ ٱلْمَرْءِ وَزَوْجِهِۦۚ وَمَا هُم بِضَآرِّينَ بِهِۦ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا۟ لَمَنِ ٱشْتَرَىٰهُ مَا لَهُۥ فِى ٱلْءَاخِرَةِ مِنْ خَلَٰقٍۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا۟ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمْۚ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ

Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani

Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.
 
Utangamano

Wawili nyie ni wenye kuvutiana zaidi kwenye tendo la ndoa, hata tamaa zenu za mapenzi zaidi zimelalia huko kwenye mchezo huo,
Lakini ni wenye kuhitaji furaha zaidi kwanza hadi kufikia kwenye hatua hiyo ya kuingia chumbani baada ya kuelewana kwa tofauti zenu wote nje ya chumba.

Kwa maana yeye mwenye hisia zaidi utaona ni mwenye kuchukizwa zaidi na tabia zako za kutaka kutawala mapenzi.
Na wewe utajikuta ni mwenye kushindwa kuendelea kukubaliana na matakwa yake yaliojaa ung'ang'anizi na hisia ndani yake mithili ya mtu anaetaka kulia na ukizidisha tu ukali utaona machozi teyari, Yeye anataka zaidi mtu mwenye uchangamfu wa kihisia ili kumchangamsha yaani mwenye upendo unaotoka moyoni na atachanganywa na asili yako ya mgomo baridi.

Wawili nyie wote ni wenye kuhofia kukataliwa pale anapotaka lake, Lakini yeye ni mwepesi kutoa na wewe ni mchoyo ama kwa maneno mengine yeye ni mwenye kupenda kutoa na wewe ni mwenye asili ya uchoyo.

Pia yeye ni mwenye kukupa mapenzi unayoyataka lakini wewe ni mwenye uchoyo wa mapenzi na hata ukiambiwa hukubali.
wawili nyie kwa mtizamo hapa ni nyota mbili tofauti na zinapinga mtizamo mzima wa unajimu.

Rakims
Tena hapa unasababisha faraqa baina ya mke na Mume kwa kuwadanganya kuwa hawaendani ki nyota ama kweli QURAN imewabainisha vilivyo enyi wachawi na uchawi wenu wa unajimu.

Al-Baqarah 2:102

وَٱتَّبَعُوا۟ مَا تَتْلُوا۟ ٱلشَّيَٰطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَٰنَۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَٰنُ وَلَٰكِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ كَفَرُوا۟ يُعَلِّمُونَ ٱلنَّاسَ ٱلسِّحْرَ وَمَآ أُنزِلَ عَلَى ٱلْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَٰرُوتَ وَمَٰرُوتَۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَآ إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِۦ بَيْنَ ٱلْمَرْءِ وَزَوْجِهِۦۚ وَمَا هُم بِضَآرِّينَ بِهِۦ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا۟ لَمَنِ ٱشْتَرَىٰهُ مَا لَهُۥ فِى ٱلْءَاخِرَةِ مِنْ خَلَٰقٍۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا۟ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمْۚ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ

Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani

Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.
 
Ngoja nikutabirie kwanza wewe
Hamuachani mpaka mbingu iseme pooh
Tulia tu na mama chanja
Hahahahahhaha!.

Endapo mtoa Mada atatoa majibu mengine tofauti na yako nitamtimua. Haya ndiyo majibu sahihi mno.

Twende kwako sasa..
 
Hahahahahhaha!.

Endapo mtoa Mada atatoa majibu mengine tofauti na yako nitamtimua. Haya ndiyo majibu sahihi mno.

Twende kwako sasa..

Umtimue aende wapi sasa ubavu wako wa pili

Ke 15/02
Me 22/01 [emoji23][emoji23]
Uchawi huu ndugu yangu
 
Mkuu ukipata muda niangalizie hapa kabla sijamuweka ndani huyu mwali

Mimi ni mwanaume

Jina: J
Kuzaliwa: 20 mwezi 08

Yeye

Jina: E

Kuzaliwa: 02 mwezi 04
 
Haya [mention]Rakims [/mention] Sijawahi kuamini kwenye mambo ya nyota ila kama ukipatia hapa lazima niamini na ntakutafuta

Mimi Me : 03/01 (Herufi ya kwanza D)

yeye ke : 25/09 (Herufi ya kwanza H)
 
Back
Top Bottom