scatter
JF-Expert Member
- Feb 15, 2013
- 1,667
- 926
Wakuu habari zenu,
Kichwa cha habari kinajieleza. Ningependa kufahamishwa kwa nini mtu akitaka kufanya jambo baya utasikia akisema NITAKUFANYIA UMAFIA au utasikia akisema MIMI NI MAFIA NITAKUUA!
Je, kuna uhusiano wowote na kisiwa cha Mafia?
Mwenye kujua kiini cha neno hili ningefurahi kufahamishwa kwani nina trip ya kwenda Mafia so nikikumbuka maneno hayo juu naishiwa hamu kabisa ya safari.
Kama kuna uhusiano na watu wa Mafia chanzo kilikuwa nini?
======
Jumong S says;

Hili ni kundi lililosikika na linalosikika sana duniani na ni maarufu sana nchi za Ulaya hasa Italy, visiwa vya Cicily. Inasemekana jamaa ni wavumbuzi wakubwa wa mbinu za kijasusi, mauaji na ulinzi. Kuna ukweli kuwa wana mbinu nyingi ambazo wakati mwingine hata vyombo vya usalama hawajawahi kuzijua.
Huko kuna kila aina ya practice au mafunzo ya kujifua ikiwa ni pamoja na Martial Art, Karate, Kung Fu, Kick Boxing n.k. Pia hujifunza kwa ustadi mkubwa matumizi ya silaha zote uzijuazo!
Jamaa hubadilika kadri tekinolojia inavyobadilika. Ni vigumu kujua kiongozi wao ni yupi maana mara nyingi hugawanyika ktk vikundi vidogo vidogo ambavyo huwa na uongozi na members huaminishwa kuwa ndo uongozi wa MAFIA japo orders nyingine za kundi hutoka from unknown sources!
Anayewajua zaidi atuelezee maana hivi karibuni serikali ya Italy ilitangaza kuwakamata viongozi wakubwa wa Mafia na kusema kundi linasambaratika!
Je, kuna ukweli kuwa kundi lina association na Kanisa?