Nitamjuza vipi rafiki yangu bila kumkwaza, kwamba akivua viatu chumba kinajaa harufu mbaya?

Nitamjuza vipi rafiki yangu bila kumkwaza, kwamba akivua viatu chumba kinajaa harufu mbaya?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Nina rafiki yangu wa muda mrefu tu na wala hatujawahi kuwa na tatizo, isipokuwa tu akivua viatu yaani chumba huwa kinajaa harufu kali. Ila yeye wala haonagi noma!

Nitawezaje kumjuza bila kumkwaza?
 
Aktaka kuvua mwambie ingia tu mwanangu kimasihara lakn akishaingia navyo ndio unamchana kwamba ungevivua tungehamia nje fanya kuvaa soks au kua unafua viatu kila wkend
 
Inategemea namna mnavyochukuliana, wakati mwingine unaweza kumwambia vizuri tu, ikawa nongwa hadi ukaona Bora ungenyamaza,

Muda mwingine unaweza usimwambie kwa kuepusha shari ukaona labda mbadili tu mazingira ya kukaa, ila akija gundua kuwa huwa unajisikia vibaya na humwambii bado itakuwa kesi
Yaani ni ngumu kujua binadamu tunataka nini.

Ila kama ni deep friendship unamchana kishkaji then maisha yanaendelea
 
Nina rafiki yangu wa muda mrefu tu na wala hatujawahi kuwa na tatizo, isipokuwa tu akivua viatu yaani chumba huwa kinajaa harufu kali. Ila yeye wala haonagi noma!

Nitawezaje kumjuza bila kumkwaza?
Akitaka kuvua mwambie
Nina rafiki yangu wa muda mrefu tu na wala hatujawahi kuwa na tatizo, isipokuwa tu akivua viatu yaani chumba huwa kinajaa harufu kali. Ila yeye wala haonagi noma!

Nitawezaje kumjuza bila kumkwaza?
Akitaka kuvua mwambie ingia navyo tu mshikaji wangu wala usiwaze, usiongee neno lingine, mkaribishe muendelee na stori nyingine hicho kitendo tu lazima ajishtukie kama ni mwelewa atajirekebisha au akijua anakuja kwako atavaa sandozi, sema huyo rafiki yako unamuogopa sana utadhani ni baba yako.
 
[emoji28][emoji28]believe me huyo siyo rafiki yako.

rafiki yako anuke mdomo,soksi,kikwapa,huwezi sita sita kumwambia.

hivi unajua kwann marafiki wanapewa vipaumbele hata kwenye familia siku hizi kuliko ndugu??sababu ni watu ambao hawakubali uharibikiwe.
 
Kama umeshindwa kumchana basi huyo sio rafiki yako, marafiki huyu tunaambiana ukweli pale tunapozingua
 
Unavumilia harufu kisa urafiki!!! Mwambie ajue shida ni nini.. aweke viatu nje.. kuna majamboz hayavumiliki hata iweje.. hilo mojawapo.. Mie mwili tu wa mtu hata nje nitamupeleka akakae na sio ndani kwangu nikalie harufu ya muntu.
 
Mweleze kwa ukarimu tu atakuelewa!
Huenda ana tatizo la pua kushindwa kunusa harufu mbaya.
 
mkishapika ugali wenu hakikisha ugali unaiva na kuweka ule ukoko chini ,mkiloweka sufuria basi Yale maji na ukoko ule atumie kuoshea miguu ,haitanuka kamwe

Wacha mambo ya ajabu mzee,..Imani za hovyo mno hapo mtu Avae kiatu original tu kesi imeisha
 
mkishapika ugali wenu hakikisha ugali unaiva na kuweka ule ukoko chini ,mkiloweka sufuria basi Yale maji na ukoko ule atumie kuoshea miguu ,haitanuka kamwe
Hata watoto wakianza puberty, haya maji wapitishe makwapani na miguuni for boys, hawawezi kunuka hadi kufa..
 
Mwanangu huwa unaoga na viatu huwa hujawahi kuvivua kabisa maishani au?

Siku nyengine ukiingia humu ndani miguu iache nje!
 
Rafiki Tu unatusumbua na thread
Angekuwa mama mkwe je?
 
Nina rafiki yangu wa muda mrefu tu na wala hatujawahi kuwa na tatizo, isipokuwa tu akivua viatu yaani chumba huwa kinajaa harufu kali. Ila yeye wala haonagi noma!

Nitawezaje kumjuza bila kumkwaza?
Mwambie kwamba hivi "Naona ndugu yangu una tatizo kama langu la zamani,yaani lilinisumbua sana,ila sema nikafanikiwa kulimaliza ijapo kwa shida kidogo...... atakuuliza tatizo gani hilo? utajibu hili la fangasi za miguuni. haalafu baada ya hapo utakuwa umeshafungua mjadala rafiki.utaendelea kwa pamoja kujadili kwa nianjema ya kusolve tatizo..Ila Hakikisha unazo abc za jinsi ya kudhibiti tatizo la harufu miguuni ili usaidie kutoa ushauri utakao msaidia ndugu yako(maana huyo ni ndugu yako si rafiki tena)
 
Back
Top Bottom