Nitamtetea na kumsemea Rais Samia na Serikali ya CCM mpaka dakika ya mwisho bila kukatishwi tamaa kwa namna yoyote ile

Kazi kubwa na njema alizozifanya Rais wetu mpendwa ndizo hizo nazozisema na ndio hata kwenye andiko langu nimezitaja japo kwa ufupi.
Sawa Mkuu hata mim namkubali sana ila akikosea ni vyema kumkosoa ili ajue sisi tuliomuajiri akae hapo huu.tupo makini na inch yetu na future ya wajukuu zetu.......
 
Ulipata divisin four , niweke matokeo yako hapa? Dunia îaenda kasi nenda shule uchawa bila elimu ni kituko
 
Naona leo wajumbe wa UWT mmechefukwa baada ya chura kiziwi kuwaamsha!! Ktk hii dunia kuna kitu huitwa fate.... huu upumbavu unaoufanya humu huyo chura kiziwi mwenyewe anakudharau.
 
Tunatamba na Mama Hadi 2030. Mwakani tunatimiza tu wajibu wa uchaguzi. maana mpaka sasa Rais Wetu Mpendwa Mama Samia ni mshindi katika Mioyo ya mamilioni ya watanzania.
UWT ya CCM hamnaga akili!! Magufuli mlimtabiria kutawala milele yuko wapi?
 
Kama unalipwa hamna Shida ila anachofanya huyo mama ako ni kuprove uongozi pekee mwanamke anaopaswa kupewa ni wa kikoba
 
Rais Samia analitetea na kulipigania Taifa letu usiku na mchana.

Lakini CCM kwanza na taifa baadae.

Kama kweli nchi iko mbele ya chama angepigania zaidi katiba ya nchi ambayo kila mtu ana amini ingeleta maendeleo zaidi lakini ubinafsi ndiyo tatizo. Mama alianza vizuri sasa amekuwa yeye kwanza Tanzania baadae kwa mawazo yangu inasikitisha sana
 
Na hapo hakuna wa kusemwa vibaya kwa maana mambo mengi yanakuwa yamenyooka, jamii ndiyo itahukumiwa
 
Hongela
 
Mama anaendelea vizuri sana na ndio maana kila mtu anashuhudia mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya muda mfupi sana wa uongozi wake .hata suala la katiba mpya nalo wala usijali hata kidogo maana mama ana dhamira njema kwa Taifa letu.
 
Unanikumbusha kulala na mafaili, (sleeping next to files)
Moyo wa Mama na mawazo ya Mama ni juu ya ustawi wa Taifa letu na watanzania.ndio maana anafanya kazi muda wote hata kukosa muda wa kutulia na familia yake.kwa sababu ya kutaka kuona watanzania tunapata huduma na maendeleo
 
Hakuna ulazima wa kutuambia yote haya.
 
Kizuri kinajiuza.
Kazi za Rais Samia zinaonekana machoni kwa watanzania wote wasio na upofu wa macho na akili.ndio maana hata mimi nimezitaja kazi hizo bila hofu wala wasiwasi wa aina yoyote ile.
 
Reactions: Tsh
Unaharibu. Kiongozi bora hahitaji kutetewa na mtu au kikundi cha watu kwa maneno mengi yasiyo na mwisho muda wote. Wananchi wenyewe huwa mashahidi wa kazi zake na utendaji wake makini katika kushughulikia matatizo yao. Acha ubora wake wenyewe umshuhudie.

Kiongozi anayehitaji kupiganiwa nyakati zote kwenye media tena na watu wa aina yako (machawa pro-max) huyo ana matatizo makubwa sana. Na kama wanavyosema wadau wengi hapa, siku akiondoka au kuondolewa madarakani, amin nakuambia, wewe utakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kumkana. Tena utamkana mara tatu kwa kuanzia. Naamini hata yeye anakujua vizuri. hivyo, anakaa mkao wa tahadhari pande hiyo.

Muda utasema. Tena ama utabadilisha jina (utambulisho) hapa JF au utakuja na hekaya za kudanganywa. Kwamba ulifichwa ukweli fulani fulani kumhusu huyo kiongozi. Kisha utahamia kwa mpya na mapambio mapya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…