Nitapenda kupokea ushauri kuhusu chapa ya DOVE

Nitapenda kupokea ushauri kuhusu chapa ya DOVE

Kilangi masanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
4,495
Reaction score
5,025
Wadau wa Jamii Forums habari zenu, nimekuja kwenu nikiwa na maswali ila pia nitapenda kupokea ushauri kuhusu chapa tajwa hapo juu.

Nimekua nikiona tu hizi bidhaa za hii kampuni ya njiwa (Dove) mitandaon na sehemu mbalimbali. Nataka kujua je, hii chapa ni ya nchi gani kwa asili? Je bidhaa zao zimejumuisha bidhaa zote muhimu kama sabuni, dawa za meno, deodorant, mafuta ya nywele, body spray na vingine?

Ufanisi wake (matokeo yake) kwa mtumiaji ni mazuri? Ni wapi kwa mikoa yetu mikubwa hasa Dar naweza pata kifurushi kamili cha bidhaa hizi, bei zake zipoje?
 
Wadau wa jamiiforum habari zenu, nimekuja kwenu nikiwa na maswali ila pia nitapenda kupokea ushauri kuhusu brand tajwa hapo juu.
Nimekua nikiona tu hizi bidhaa za hii kampuni ya njiwa ( dove) mitandaon na sehemu mbalimbali .
Nataka kujua je hii brand ni ya nchi gani by origin.
Je bidhaa zao zimejumuisha bidhaa zote muhimu kama sabuni, dawa za meno ,deodorant, mafuta ya nywele,body spray na vingine?
Ufanisi wake ( matokeo yake) kwa kwa mtumiaji ni mazuri?
Ni wapi kwa mikoa yetu mikubwa hasa dar naweza pata full package ya bidhaa hizi ,bei zake zipoje?

Ndio wana product zote ni nzuri sana, kama upo dar nenda S.H amon huwezi kosa au maduka ya cosmetics kariakoo kule mtaa wa msimbazi au cosmetics shops za mlimani city na city mall
 
Ndio wana product zote ni nzuri sana, kama upo dar nenda S.H amon huwezi kosa au maduka ya cosmetics kariakoo kule mtaa wa msimbazi au cosmetics shops za mlimani city na city mall
Siko Dar kwa sasa ila nimeamua kutaja apo nikiwa naiman nitazipat je unaweza nipa mfano wa bei za bidhaa ulizowah nunua nijue pa kuanzia
 
Siko dar kwa sasa ila nimeamua kutaja apo nikiwa naiman nitazipat je unaweza nipa mfano wa bei za bidhaa ulizowah nunua nijue pa kuanzia

Sabuni inarange 5000-7000
Shower gel inaanzia 12,000 na kuendelea depending on eneo unalonunua
Body lotion 25,000 inaweza kupungua au kuongezeka depending na aina, ujazo na location
 
Back
Top Bottom