PreGE2025 Nitashangaa ikiwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vitaliacha hili jambo lipite bila kuchukua hatua. Tunakoelekea sio kuzuri

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Habari zinazosambaa mitandaoni zinatisha. Kama ni za kweli au la hilo tuliache kwa vyombo vyenye mamlaka.

Imefika mahali Watu wanashirikiana na watu wasiolitakia mema Tanzania kutia hofu, kuleta taharuki na vurugu. Hii yoote ni kwa sababu gani?

Kwanini chama cha siasa kisitumie mbinu zake za kisiasa kushawishi watu badala ya kutisha na kuleta uchochezi? Huu Uchochezi ni wakawaida? Je kuna kitu kinaandaliwa ili baadae waje waseme, Tulisema hayo sasa yametokea!

Watu wanatunga uongo, wanatisha Wananchi, wanachochea vurugu na uhasama. Tatizo ni nini lakini?

Kuna mahali nimeona Mheshimiwa mmoja wa chama fulani anahutubia kwamba Chadema wana mpango wa kuingiza Bio Weapons kama Ebola na Mpox. Hehehe😅😅😅

Hivi Mheshimiwa anajua athari zinazoweza kutokana na Kauli zake? Kama sio yeye aka ametengenezewa clip na postures za uongo basi ni vema ajitokeze kukanusha na kujisafisha. Mimi bado si amini kama ni yeye anaweza kufanya jambo hili. Naamini anajua madhara ya kauli zake kiuchumi na kiusalama pia.

Juzi tu tumearifiwa na Ubalozi wa Marekani kuwa na tishio la shambulio la kigaidi linaweza kutokea Mkoa wa Pwani, japo vyombo vyetu viko bize kuhakikisha Jambo hilo linadhibitiwa naona kauli kama hizi kuanza kujitokeza kipindi hiki kama kudivert attention ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Ni bora vikamuita na kumhoji na kumchukulia hatua za kisheria.

Kundi hilo hilo la kina Fidodido limekuja na Audio Clip na kuisambaza mitandaoni wakidai ni Mh Sugu anatafuta vijana 200- 300 wa kufanya vurugu Mkoani Mbeya. Ni hatari sana.

Jambo Moja la kuwakumbusha ni kuwa Unabii Umeshasema kila watakapo jaribu Kuzuia basi watakikuta wanaharibu zaidi.

Inawezekana ndio yanatimia?? Hii panic inatokana na nini? I don't see the need to jeorpadize our harmony for sake of their interest.

Vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama vimehakikisha amani inadumu Tanzania wakati wote. Tuna imani na nyie wazee.
Vyombo vyote vya dola vinalamba nyayo za ccm, hakuna yeyote wa kuiletea fyokofyoko ccm
 
Hawa CCM wanahangaika kujinasua ila ndio wanazidi kunasa,kwanini wasisubiri kuona uchaguzi utakavyozuiliwa?si walisema hakuna wa kuzuia uchaguzi?
Kama ni kweli Chadema wanapanga kuleta Ebola kwanini hawakamatwi badala yake anaongea mtu jukwaani?

Wasitufanye sisi wajinga.
Hajuna jipya ni issu ya ngungurì na ngangari umesahau makoentena ya mapanga bandarini
 
So
Kabla ya kuanza kumlaumu makala jiulize Kwanza kwani chadema hawawezi kuyafanya hayo?kwangu Mimi chama hiki nakijua kama chama hatari Kwa usalama wa nchi hii kwani wamewahi kufanya matukio mengi na ya hatari tukio la Kwanza bomu la Arusha hili ni tukio limejulikana lilikua tukio la kupangwa na chadema wenyewe Kwa malengo yao ya kupata political tension tukio la pili kutekekwa na kupigwa Kwa Joseph Yona tukio la tatu kulishwa sumu zitto na kuuwawa Kwa chacha wangwe haya ni baadhi tu ya matukio kati ya mengi yanayoonyesha uhatari wa chama hiki
Akina soka,ben saanane,,Ali kibao hujawataja apo! au hao mlihusika nao nyie
 
Hii inanikumbusha kuna jamaa mmoja kipindi hicho, alikuwa anamtaka dem ambaye na mimi nilikuwa nataka nimle, sasa yeye alikuwa kwenye friend zone na huyo manzi. Njia pekee aliyofanya kuharibu alimwambia mimi ninangoma, na huwa naenda kuchukua ARV hospital ya mbali, daaah mbaya sana hii
Mm mmoja alinipiga hiyo tena kwa crush wangu wa chuo ,badae akaja muoa ,jamaa wana watoto wanne ila ukwel watatu maana huyu wa nne nilipambana ni mm,na nitapigia miti mpaka anaingia kaburini ikiwemo kunisomeshea mainternational kijana wangu
 
Hivi mtu akikupa taarifa kuwa kuna watu wanataka kuja kukushambulia , njia bora ni wewe kupokea taarifa na kuchukua tahadhari au wewe kumdhuru aliyekuletea taarifa?

Tafakari.

Makala ni mpumbavu kutokana na aina ya Katiba na tume tuliyo nayo inayosababisha watu kushinda bila kuchaguliwa .

Nchi inaongozwa na wapumbavu wengi.

Hiyo clip itatafsiriwa kwa lugha zote za kimataifa hallafu ipelekwe WHO ili Amos makala asaidie kujua hao wanaouza hivyo virusi.

Yaani kumbe ugonjwa huo unaingia Tanzania kwa kununuliwa halafu WHO wapo kimya.

Na Makala asaidie pia UN kutoa tamko dhidi ya wauzaji wa Virusi kiholela .
Mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu yatoe tamko la kwa nini wapo kimya wakati kuna watu wana uza na kununua virusi hatari vya ebola ili kuangamiza wenzao tena ndani ya nchi moja ambayo kwa miaka mingi watu wameishi kwa umoja mpaka awamu ya sita ilipoanza kutumia Machawa na mafunza kufanya siasa .

Hapa ndipo pazuri pa Makala kutoa ushahidi na vielelezo vyake maana tamko la CCM ni tamko la serikali .

Samia mwenyekiti wa CCM tunaamini amepata taarifa za kutosha juu ya hizo nchi wanazouza virusi .

CCM linapokuja suala la uchaguzi wanageuka wanakua mashetani na hawajali tena diplomasia za kimata mpaka uchaguzi uishe wanarudisha diplomasia kwa gharama za kuuza rasilimali zetu kama njia ya kuwavutia wageni . Huu ni upumbavu mkubwa sana na hasara kubwa kwa taifa.
Makala hana hoja tena wala sera.

Kwa nini asijifunze jinsi Kinana na Nape walivyopambana kuijenga CCM iliyokua imekufa mwishoni mwa utawala wa JK mpaka wakashinda tena.
Hizi siasa za kuleta taharuki zina faida gani?

Watanzania wenye akili wameshauri kuwa tume ya uchaguzi ifanyiwe marekebisho kabla ya uchaguzi.

Uchaguzi ukifanywa kwa tume hii na utaratibu huu wa kuwatumbia macho wahuni kama makala ni hatari sana . Hawa CCM ya wafa maji inafanya lolote sasa ili irudi madarakani.

Ila Makala akiwa na uzima ataiona CCM ikipotea kabisa katika ulimwengu wa siasa .Bora wangeweka ushindani mzuri wa kisiasa ili wenye akili ndani ya CCM wajulikane.
 
Kabla ya kuanza kumlaumu makala jiulize Kwanza kwani chadema hawawezi kuyafanya hayo?kwangu Mimi chama hiki nakijua kama chama hatari Kwa usalama wa nchi hii kwani wamewahi kufanya matukio mengi na ya hatari tukio la Kwanza bomu la Arusha hili ni tukio limejulikana lilikua tukio la kupangwa na chadema wenyewe Kwa malengo yao ya kupata political tension tukio la pili kutekekwa na kupigwa Kwa Joseph Yona tukio la tatu kulishwa sumu zitto na kuuwawa Kwa chacha wangwe haya ni baadhi tu ya matukio kati ya mengi yanayoonyesha uhatari wa chama hiki

Sio kweli .
Fanya uchunguzi wa kutosha.

Hivi vyama vina mamluki wa usalama wa taifa wanaolipwa na serikali .
Hawa wanafanya mpaka vurugu huku wakiwa na mavazi na kadi za vyama vya upinzani .

Ndio maana hakuna anayekamatwa wala kufungwa. Polisi wanapata shida zana kwa sababu ya matukio yanyoratibiwa na watu wa usalama kwani wakiwakamata wanakuta ni watu wa mfumo .

Hakuna mpinzani anayeweza kufanya tukio hata la kuchoma picha ya Samia akabaki salama sembuse kupata bomu na kulilipua na kuua watu hadharani tena kwenye mkutano wa halaiki ya watu !!
Mtoto mdogo alichora picha ya mungu Samia akapotezwa kama takataka sembuse hama cha siasa kiinguze silaha hatari kama mabomu.

Ikifikia mahali vyama vya siasa vikaweza kuingiza mabomu makubwa kuliko ya machozi ya polisi basi Jeshi linapaswa kuchukua nchi haraka sana .

Vijana wakiwa wapumbavu nchi itaongozwa kipumbavu kwa sababu hawana uelewa wa mambo makubwa kama utumiaji wa mabomu hatari ya milipuko na jinsi Jeshi linavyokua imara kufuatilia yanapotoka na nani anayeyatumia . Tanzania ina Jeshi imara sana ambalo haliwezi kuangalia wapinzani kuanza kumiliki mabomu . Kama ni kweli wa nini wasilipue majengo na ofisi za CCM kama kule mkuranga ambapo watu wote ni CCM na hakuna Chadema kabisa lakini uhalifu na ugaidi wa kutumia silaha za kivita haukomi?
CCM nchi imewashinda kwa sababu mnawaza maslahi yenu na madaraka sasa kila mtu anakua adui wa maslahi yenu.

Maslahi ya nchi yanalindwa na viongozi bora wanaopatikana kwa hoja sio nguvu na wizi wa kura .
 
Hata kama ni propaganda, hii ya kwao ni ya kipumbavu na kijuha kabisa. Unaleta propaganda ya magonjwa yasio na tiba kuleta taharuki kwa wananchi kwa sababu tu ya uroho wa kutaka kuendelea kutawala? Huu ni ujuha wa namna gani huu?
 
Sio kweli .
Fanya uchunguzi wa kutosha.

Hivi vyama vina mamluki wa usalama wa taifa wanaolipwa na serikali .
Hawa wanafanya mpaka vurugu huku wakiwa na mavazi na kadi za vyama vya upinzani .

Ndio maana hakuna anayekamatwa wala kufungwa. Polisi wanapata shida zana kwa sababu ya matukio yanyoratibiwa na watu wa usalama kwani wakiwakamata wanakuta ni watu wa mfumo .

Hakuna mpinzani anayeweza kufanya tukio hata la kuchoma picha ya Samia akabaki salama sembuse kupata bomu na kulilipua na kuua watu hadharani tena kwenye mkutano wa halaiki ya watu !!
Mtoto mdogo alichora picha ya mungu Samia akapotezwa kama takataka sembuse hama cha siasa kiinguze silaha hatari kama mabomu.

Ikifikia mahali vyama vya siasa vikaweza kuingiza mabomu makubwa kuliko ya machozi ya polisi basi Jeshi linapaswa kuchukua nchi haraka sana .

Vijana wakiwa wapumbavu nchi itaongozwa kipumbavu kwa sababu hawana uelewa wa mambo makubwa kama utumiaji wa mabomu hatari ya milipuko na jinsi Jeshi linavyokua imara kufuatilia yanapotoka na nani anayeyatumia . Tanzania ina Jeshi imara sana ambalo haliwezi kuangalia wapinzani kuanza kumiliki mabomu . Kama ni kweli wa nini wasilipue majengo na ofisi za CCM kama kule mkuranga ambapo watu wote ni CCM na hakuna Chadema kabisa lakini uhalifu na ugaidi wa kutumia silaha za kivita haukomi?
CCM nchi imewashinda kwa sababu mnawaza maslahi yenu na madaraka sasa kila mtu anakua adui wa maslahi yenu.

Maslahi ya nchi yanalindwa na viongozi bora wanaopatikana kwa hoja sio nguvu na wizi wa kura .
A word
 
Habari zinazosambaa mitandaoni zinatisha. Kama ni za kweli au la hilo tuliache kwa vyombo vyenye mamlaka.

Imefika mahali Watu wanashirikiana na watu wasiolitakia mema Tanzania kutia hofu, kuleta taharuki na vurugu. Hii yoote ni kwa sababu gani?

Kwanini chama cha siasa kisitumie mbinu zake za kisiasa kushawishi watu badala ya kutisha na kuleta uchochezi? Huu Uchochezi ni wakawaida? Je kuna kitu kinaandaliwa ili baadae waje waseme, Tulisema hayo sasa yametokea!

Watu wanatunga uongo, wanatisha Wananchi, wanachochea vurugu na uhasama. Tatizo ni nini lakini?

Kuna mahali nimeona Mheshimiwa mmoja wa chama fulani anahutubia kwamba Chadema wana mpango wa kuingiza Bio Weapons kama Ebola na Mpox. Hehehe😅😅😅

Hivi Mheshimiwa anajua athari zinazoweza kutokana na Kauli zake? Kama sio yeye aka ametengenezewa clip na postures za uongo basi ni vema ajitokeze kukanusha na kujisafisha. Mimi bado si amini kama ni yeye anaweza kufanya jambo hili. Naamini anajua madhara ya kauli zake kiuchumi na kiusalama pia.

Juzi tu tumearifiwa na Ubalozi wa Marekani kuwa na tishio la shambulio la kigaidi linaweza kutokea Mkoa wa Pwani, japo vyombo vyetu viko bize kuhakikisha Jambo hilo linadhibitiwa naona kauli kama hizi kuanza kujitokeza kipindi hiki kama kudivert attention ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Ni bora vikamuita na kumhoji na kumchukulia hatua za kisheria.

Kundi hilo hilo la kina Fidodido limekuja na Audio Clip na kuisambaza mitandaoni wakidai ni Mh Sugu anatafuta vijana 200- 300 wa kufanya vurugu Mkoani Mbeya. Ni hatari sana.

Jambo Moja la kuwakumbusha ni kuwa Unabii Umeshasema kila watakapo jaribu Kuzuia basi watakikuta wanaharibu zaidi.

Inawezekana ndio yanatimia?? Hii panic inatokana na nini? I don't see the need to jeorpadize our harmony for sake of their interest.

Vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama vimehakikisha amani inadumu Tanzania wakati wote. Tuna imani na nyie wazee.
Hawana peace of mind Chamani kutokana na kuwadhalilisha wazee waliokuwa na uwezo wa kutoa majibu kwenye Maswali magumu yaliyokuwa yakielekezwa kwa Chama !

Sasa wamebaki na watu ambao uwezo wao ni huo wa kuzua taharuki na kutumia mabavu ! Sio hoja kujibiwa kwa hoja !

Wenye Akili wamekaa pembeni wanawaZoom tu na kuwacheka 🤣🤣 !
 
Back
Top Bottom