Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Hakuna wakati ambapo uchaguzi wa Tanzania ungekuwa mwepesi sana kwa wapinzani kama uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025. Ni wachache mno wanaoridhishwa na serikali hii ya awamu ya sita, kati ya hao ni wateuliwa, baadhi ya wanachama wa CCM wenye maslahi (asilimia kubwa ndani ya chama hawamkubali mwenyekiti wao), chawa na baadhi ya watumishi na wafanyabiashara wenye maslahi yao binafsi ambao wananufaika moja kwa moja na utawala huu.
Tofauti na hapo, hii ingekuwa nafasi kubwa na ya kipekee sana kwa wapinzani kuzichanga karata zao kushinda katika uchaguzi mkuu 2025.
Sishangai purukushani na jitihada kubwa zinazofanywa kuudhoofisha upinzani, hususan siku za hivi karibuni, kwani iko wazi na inajulikana kwamba endapo utawala wa awamu hii utasimama man to man dhidi ya upinzani ulio imara mithili ya ule wa Mrema vs Nyerere au Dr.Slaa vs Kikwete, hakika CCM won't stand a chance.
NB; Ni kweli tume si huru na ya haki, lakini watanzania sasa angalau wanauelewa, endapo upinzani ungeshinda kwa 80% na CCM kwa 20% tume ipi ingekuwa na jeuri ku 'temper' na matokea hayo ambayo yapo 'obvious'?