🛑 NITATETEA TENA NAFASI YANGU YA UBUNGE JIMBO LA NKASI 2025
NILISHINDA UBUNGE 2020 LICHA YA CHAMA KUSUSIA UCHAGUZI, KAULIMBIU YA 'NO REFORMS, NO ELECTION' HAINIHUSU - NITATETEA TENA NAFASI YANGU MWAKA (2025) HUU - AIDA KHENAN, MBUNGE WA CHADEMA NKASI KASKAZINI
====
JamiiCheck imefuatilia madai haya na kubaini kuwa yanapotosha
NILISHINDA UBUNGE 2020 LICHA YA CHAMA KUSUSIA UCHAGUZI, KAULIMBIU YA 'NO REFORMS, NO ELECTION' HAINIHUSU - NITATETEA TENA NAFASI YANGU MWAKA (2025) HUU - AIDA KHENAN, MBUNGE WA CHADEMA NKASI KASKAZINI
====
JamiiCheck imefuatilia madai haya na kubaini kuwa yanapotosha
Aida Joseph Khenani ni mbunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayewakilisha jimbo la Nkasi Kaskazini, Aida ndiye mbunge pekee kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
Madai
Kumekuwapo na grafiki inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikionekana kufanana na ya Jambo Tv ikiwa na ujumbe kuwa kuwa alishinda ubunge 2020 licha ya chama kusususia uchaguzi na ameeleza kuwa kaulimbiu ya No reforms No eletion haimuhusu na ataitetea tena nafasi yake mwaka huu. Tazama hapa na hapa
Uhalisia wa madai hayo
Jamiicheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa yanapotosha. JamiiCheck imefuatilia mkutano wa hadhara uliofanywa na CHADEMA mkoani Rukwa katika jimbo la Nkasi Kaskazini ambapo mbunge wa eneo hilo pia Aida Khenani alizungumza. Tazama mkutano huo hapa
Kuhusu uchaguzi wa 2020
Aida Khenani alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo hali ya uchaguzi wa mwaka 2020 akieleza kuwa uchaguzi wa mwaka huo haukuwa wa haki na huru na kama ungekuwa huru wangeshinda kwa shindo.
Kuhusu No reforms No election na uchaguzi mkuu ujao
Katika mazungumzo yake aliyoyafanya katika mkutano huo hakutamka kauli ya No reforms No election na badala yake alieleza kuwa wanamsubiri mwenyekiti atoe tamko kuhusu uchaguzi mkuu ujao. Na amewahakikishia wananchi kuwa uchaguzi ukiwa huru na wa haki lazima watashinda
Aidha tumefuatilia grafiki inayoonekana kufanana na ya Jambo Tv na kubaini kuwa haijachapishwa na Jambo Tv hivyo ni ya kughushi. Grafiki hiyo inaonekana kuwa na msongamano wa maneno mengi, jina la aliyezungumza kukaa chini kabisa ni tofauti na Grafiki halisi za Jambo Tv.