Nitatetea tena nafasi yangu ya ubunge jimbo la Nkasi 2025

Status
Not open for further replies.
Haya maneno wanasiasa kote wanaongea hata Madeleka kapost atagombea jimbo la Kivule katweet jana,ulikua pale makao makuu ya CDM na ukasema karibu na kwenu kabla haukuuchangia silu ile kwenye mkutano wa wahariri wa habari ila nasikitika kwamba hata wewe msomi uliokua pale mita hazizidi hamsini haukumwelewa TAL na CDM kwa ujumla na hii ni aibu kwa taaluma yako, subiri nilueleweshe mimi nilieangalia kupitia you tube labda unaweza elewa Bila "mabadiliko hakuna uchaguzi" na "SIO KUSUSIA UCHAGUZI" kwaio CDM wanapush agenda nchi nzima ili mabadiliko yafanyike ili waende kwenye uchaguzi ambao Aida anawaita waje wagombee kwenye sheria za uchaguzi zilizobadilika. Nguvu ya umma kupitia kura ndio waajiri wa madiwani,wabunge na Rais. Hivyo wananchi wakiamua kudai mabadiliko ya Sheria za uchaguzi nchi nzima zitabadilishwa tuu.
 
Utajipigia kura mwenyewe,coz hakuna uchaguzi bila mabadiliko ova.
 
Sijamsikia akisema hayo yaliyoandikwa zaidi ya kusema, "ajaye na aje tutakutana kwenye uchaguzi".
Kauli hii ni sawa na iliyoandikwa!!??
CCM mna propaganda za hovyo kama za enzi zile za kuonyesha video za mauaji ya kimbari ya Rwanda na kuwatisha wananchi kuwa wakichagua upinzani, nchi itakuwa kama Rwanda na Burundi!!

CCM wamekata pumzi.
Mwaka huu lazima kieleweke.
 
Nimependa ujasiri wake anawakilisha kundi la ambao hawataki kuburuzwa na dikteta Lisu na ubabe wake wa No reform no election kisa hana hela za kampeni za uraisi anataka kukomalia ile slogan ya tukose wote sababu yeye hajajipanga
umeona mbali kitu ambacho wadau na wanachadema wengi sio rahisi kukiona na kukigundua 🐒
 
Nimependa ujasiri wake anawakilisha kundi la ambao hawataki kuburuzwa na dikteta Lisu na ubabe wake wa No reform no election kisa hana hela za kampeni za uraisi anataka kukomalia ile slogan ya tukose wote sababu yeye hajajipanga
umeona mbali sana gentleman,

tena umeona kitu ambacho wadau na wanachadema wengi sio rahisi kukiona na kukigundua kutoka kwa huyo jamaa wa no reform no elections 💪👊
 
Nimependa ujasiri wake anawakilisha kundi la ambao hawataki kuburuzwa na dikteta Lisu na ubabe wake wa No reform no election kisa hana hela za kampeni za uraisi anataka kukomalia ile slogan ya tukose wote sababu yeye hajajipanga
Hapa ndio unaona umecheza mind game la hatari😁😁 Ila nyie vilaza bana.
 
Nina mashaka na haya maelezo yote kama kweli kaongea hivi.
 
Typical tabia za Kitanzania za "selfishness" yeye anajijali mwenyewe tu haangalii kwa mtazamo mpana wa Taifa.
 
Kumkomesha Chadema waweke mgombea mwingine tuone ataishia wapi?
 
Hiyo ni moja ya strategy ya CCM, hatuna Sheria ya mgombea binafsi, yeye anagombeaje wakati chama chake hakiko tayari kushiriki uchaguzi?.

Fomu anapewa na kusainiwa na Nani?
Kwani amesema lazima iwe kupitia CDM?
 
Sijamsikia akisema hayo yaliyoandikwa zaidi ya kusema, "ajaye na aje tutakutana kwenye uchaguzi".
Kauli hii ni sawa na iliyoandikwa!!?
Sio kila kitu lazima kisemwe!, 2020, Chadema mlisusa!, huyu hakuukubali ujinga huo!, akagombea, akashinda, mkamsusa!.
Sasa mnarudia tena ujinga ule ule!, wenye akili na wanaojitambua, watagombea!.
Naendelea kuwasisitizia viongozi wenu, hamasisheni watu wakajiandikishe kwenye daftari la kudumu!.
P
 
Hawa ni nyumbu kwerikweri, sasa maana ya 'no election' ni nini. Mara no election mara tutashiriki uchaguzi, the wicked people
 
Aida Joseph Khenani ni mbunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayewakilisha jimbo la Nkasi Kaskazini, Aida ndiye mbunge pekee kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Madai

Kumekuwapo na grafiki inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikionekana kufanana na ya Jambo Tv ikiwa na ujumbe kuwa kuwa alishinda ubunge 2020 licha ya chama kusususia uchaguzi na ameeleza kuwa kaulimbiu ya No reforms No eletion haimuhusu na ataitetea tena nafasi yake mwaka huu. Tazama hapa na hapa

Uhalisia wa madai hayo

Jamiicheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa yanapotosha. JamiiCheck imefuatilia mkutano wa hadhara uliofanywa na CHADEMA mkoani Rukwa katika jimbo la Nkasi Kaskazini ambapo mbunge wa eneo hilo pia Aida Khenani alizungumza. Tazama mkutano huo hapa

Kuhusu uchaguzi wa 2020

Aida Khenani alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo hali ya uchaguzi wa mwaka 2020 akieleza kuwa uchaguzi wa mwaka huo haukuwa wa haki na huru na kama ungekuwa huru wangeshinda kwa shindo.

Kuhusu No reforms No election na uchaguzi mkuu ujao

Katika mazungumzo yake aliyoyafanya katika mkutano huo hakutamka kauli ya No reforms No election na badala yake alieleza kuwa wanamsubiri mwenyekiti atoe tamko kuhusu uchaguzi mkuu ujao. Na amewahakikishia wananchi kuwa uchaguzi ukiwa huru na wa haki lazima watashinda

Aidha tumefuatilia grafiki inayoonekana kufanana na ya Jambo Tv na kubaini kuwa haijachapishwa na Jambo Tv hivyo ni ya kughushi. Grafiki hiyo inaonekana kuwa na msongamano wa maneno mengi, jina la aliyezungumza kukaa chini kabisa ni tofauti na Grafiki halisi za Jambo Tv.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…