Nitawaambia nini wanachama? Nitajiunga na CCM ya Mzee Wassira endapo kwa namna yoyote Wajumbe wenzangu Watakula rushwa na kumchagua Mbowe

Ondoka, chama cha siasa ni imani,sio mtu.. wewe ni mtu wa maslahi.. kwani lazima Lissu ashinde..
 
Kwani lazima ushabikie siasa ? Mbona kuna mambo tele ya kuyapatia mkazo, uzito na umuhimu kuliko hayo mavyama. Utakufa, utalemaa, au kufilisika bure.
 
kama ulijiunga Chadema kwa sababu ya mtu, uamuzi wako ni sahihi. Lakiji kama kilichokupeleka Chadema ni Itikadi, na falsafa iliyopelekea kuanzoshwa kwa chama hicho,ninyi ndio msiofahamu mnataka nini.
Samahani ikiwa lugha yangu sio sawa.
Sawa lakini sio rushwa
 
Earthmover tunaomba kura kesho kwa TAL na Heche na utusaidie kuomba kura kwa wengine hapo makao makuu,hii itasaidia kuokoa chama mtaani maana wajumbe 1200 hawawezi kushinda uchaguzi bali uchaguzi unashinda ukiwa na wanachama na washabiki.
 
Jiunge tu hakuna namba....
 
WACHA MBOWE ASHINDE TUONE NINI KITATOKEA.....,HAO HAO WASIOMTAKA WATAKIMBILIA CCM AMBAKO WANASEMA MBOWE KAPEWA PESA!!
MSIGWA YUKO WAPI...
 
WACHA MBOWE ASHINDE TUONE NINI KITATOKEA.....,HAO HAO WASIOMTAKA WATAKIMBILIA CCM AMBAKO WANASEMA MBOWE KAPEWA PESA!!
MSIGWA YUKO WAPI...

Ni mpumbavu tu atabaki na Mbowe asiye na teuzi wa benki kuu wala mahakama na polisi na tume ya uchaguzi.

Unabaki CHADEMA kwa wakala wa CCM si bora ukae kiwandani kabisa kuepuka mateso .
Msigwa anaumia sana kwa sababu Iringa kwa Wahehe CHADEMA haikujengwa na Mbowe . Hakuna Mmachame aliyeuawa kwa sababu ya kukijenga CHADEMA Iringa.
Imani ya watu kwa siasa za upinzani haikujengwa kwa rushwa ni imani ya kiroho . Ni watu wanaochukia Ufisadi kutoka rohoni tangu ufisadi wa miaka kabla ya mwaka 1995 watu walipinga rushwa na ugobachori wa wageni kushirikiana na watawala kuibia nchi.

Musimdanganye Mbowe uovu na usaliti kwa binadamu ni Mbaya sana . Hatabaki salama. Karma ya damu za watu kupigania haki itamtafuna. Usione ni kwa nini JPM alidhibiti hivi vyama ikiwemo CCM na CHADEMA na upinzani kwa ujumla damu za watu wengi zimemwagwa kwa sababu ya dili za watu kama Mbowe na Lipumba .Kwa uzee wao wataishia kama Mrema na vyama vyao mfukoni.
Siasa za usanii wa Mbogwe na Lipumba ni Hadaa na miradi ya Watu kujipatia fedha kama halafu eti ni mfanya biashara na anasaidia chama kumbe uongo mtupu. Leo imebainika hata majimboni haziendi fedha . Anathamini pesa kuliko utu. Mapesa anayohonga leo kwa nini hakuwapa fidia familia za wahanga wa kukipigania chama kama Alfonsi Mawazo na Ally Kibao.

Kama CHADEMA ni sawa na CCM kwa ufisadi kuna haja gani ya kubaki CHADEMA kwenye mateso badala ya kwenda kuishi kwa raha CCM.?

Kama mnabisha subirini uchaguzi upite halafu Mbowe apite mikoani ndio mtajua kuwa hamjui . Hakuna mtu wa kuhangaika na siasa za kilaghai . Na pia mwisho wa wauza nchi sio mbali sana . Pesa za rushwa za DP World zimeingia kila mahali mpaka madhebahuni kwenye nyumba za ibada. Hili ni chukizo kubwa sana ,huu ni uovu mkubwa sawa na ushoga zamani za Sodoma na Gomora.Ushoga enzi za Sodoma na hata Leo ukipoonekana ni kitu cha kawaida kwenye jamii ndipo hasira ya Mungu ilipoweka juu ya nchi. Yaani hata leo mfano ubakaji usikemewe na wanaokemea wauawe na kutishwa na kutolewa kwenye uongozi basi kitakachofuata ni jamii kuingia kwenye balaa kubwa. Mfano tu yanayotokea huko USA yananyemelea Tanzania kama mfumo mzima utageuka na kuwa mfumo wa rushwa utekaji na kuwanyamazisha wanaokemea rushwa .

Nawahakikishia wale wote waliomsihi Mbowe ajiengue watajitenga na siasa za Mbowe.Unabalije kwenye siasa za watu wanaoneemeka na rushwa ndani ya Chama kutokana na kuwafurahisha CCM?. Kitakachofuata ni waovu ndani ya Chadema na wenzao ndani ya CCM kugombea madaraka ya kushika dola. Watauana kama kuku maana kwao damu za watu hazina thamani zaidi ya madaraka . Kule ishara imeshajionyesha.

Kama yule mtu mnyenyekevu kule Yule amejiondoa na kupumzika .Huko kwenu watu wema watabaki wakifanya nini ? Au mnafikiri ni lazima kufanya siasa za CCM na Chadema majukwaani ?
Leo Zito hayuko CHADEMA na maisha yanaendelea kwa uzuri kabisa .Na chama chake ndicho chama kikuu cha upinzani maana kimeshika dola kule Zanzibar pamoja na CCM .
 
Pole
 
Pole, yule mwamba , pesa kwake mmmh ? Mate ya fisi
 
🤣 🤣 🤣
 
Wewe mwenyewe unamuogopa Mbowe ndio maana hutumii jina lako halisi, halafu unalaumu wenzio? PUMBAVU!!
 
Umemaliza, Bila D mbili kuelea ngumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…