Uchaguzi 2020 Nitawashangaa CHADEMA kama watampitisha Tundu Lissu kuwa mgombea

Uchaguzi 2020 Nitawashangaa CHADEMA kama watampitisha Tundu Lissu kuwa mgombea

Hilo la udikteta, mjivuni na dharau kwa wenzake ni kweli. Lissu ana haya matatizo sasa njemba yenye madhaifu ya hivi ikiwa amiri jeshi mkuu itaturudisha utumwani..
Lissu endelea kuwa mwanaharakati wa haki za kijinsia urais wa nchi haukufai
 
Umekumbuka jana nilikuambia ccm hawako tayari Magufuli aingie kwenye ushindani na hasa Tundu Lisu? Huo ndio mrejesho. Inafahamika kuwa iwapo Lisu atagombea, atamuweka Magufuli kwenye wakati mgumu sana.

Kuna mgombea urais aliwahi kuwaambia wapiga kura kwenye mkutano wa kampeni kuwa afadhali yeye kukosa kura za urais kuliko Lissu kuchaguliwa kuwa mbunge! Hii inaonyesha jinsi asivyokubalika miongoni mwa baadhi ya wanasiasa wa nchi hii. Kama kuna jambo ambalo baadhi ya wanasiasa wa nchi hii watapigana kufa na kupona, na ikibidi kuvunja sheria zote za nchi hii ili kuhakikisha halitokei ni kuzuia Lissu kupanda jukwaani kufanya kampeni kwenye uchaguzi ujao.
 
Tundu kweli simpendagi anashusha heshima zenu.
😂🤣🤣🤣 kabla ya kupigwa risasi alikuwa anavuruga sana watu.
 
Umekumbuka jana nilikuambia ccm hawako tayari Magufuli aingie kwenye ushindani na hasa Tundu Lisu? Huo ndio mrejesho. Inafahamika kuwa iwapo Lisu atagombea, atamuweka Magufuli kwenye wakati mgumu sana.
na Lissu ndiye mgombea wa Chadema na Dunia , nisome vizuri , Magufuli ni rais wa miaka mitano 5 tu , kwa kujiamini naandika haya , hongera wastaafu wa ccm kwa kurahisisha mchakato
 
Samahan kidogo naona Kuna watu wengi Wana Sema CCM Wana mgwaya lisu

Je? Lisu ame kuwa hatari kuliko alivyo kuwa Edward lowasa??

Nguvu ya lowasa +muungano wa vyama vyote vya upinzan mkashindwa kuindoa CCM...

binafs naona kabisa guvu ya wa pinzan bado haitoshi kwaiyo waweke yoyote Ata wakuweza waweke wote
 
Yule Jamaa mropkaji wa matusi akiputishwa dunia itatucheka
'' na wewe tunakuweka hapo ili mkagombanie wanaume''. Hii kauli ni kuropoka? Kukosa staha? Jazba? Kukosa busara? Kuona wengine si chochote zaidi ya kugombania vitu vidogovidogo? Au? Hebu nipe jibu comrade.
 
Hapo alikuwa akiwatania watani zake wazaramo
 
Yanga; Hii timu ya Simba kama inataka ushindi dhidi yetu sidhani kama inastahili kumpanga Meddie Kagere pale mbele. Kwanza huwa hajui kufunga, na uwezo wa kupiga Mpira vichwa hana kabisa. Yaani itakuwa hasara kubwa kumuweka hata benchi la akiba.

Simba; Pelekeni ujinga wenu huko, ebo!
Nimelipenda sana hili jibu kwa wana-Lumumba. Wape salam. Simba na Yanga kweli watakutana fainali ya FA?
 
Tundu lissu ni mwenyekiti wa CCM?
Usipotoshe lengo bwana sheikh kama nyie wenyewe mmeshindwa kumtetea basi hafai
Wote wawili magu na Tundu lisu walishajidhihirisha mbele ya jamii...kwa misingi kwamba jamii inawajua hulka na Tabia zao mzee, Sasa hizo sifa ulizoainisha kwenye bandiko lako Ni sifa ama hulka za mwenyekiti wenu magu hakuna ubishi juu ya Hilo. Vinginevyo uendeleze propaganda tu hapa nitakuelewa.
 
Back
Top Bottom