Nitumie mbinu gani kujifunza kiingereza kwa urahisi

Vitabu
Na movies zenye subtitle
Hapa utakuwa mzuri kwenye eneo la kusoma na kusikia ila siyo kuongea.

Ili ujue kuongea lugha yoyote ile lazima uipractice. Nje ya hapo utaishia kusikia maneno ila likoja swala la wewe kuongea inakuwa kamzozo.

Kuna Binti beki tatu hakuna na shule kabisa ila nyumba aliyokuwa anaishi muda mwingi wanaongea kiingereza,with time nae alijua kuongea fluent English kama amesoma-How? Alikuwa anaongea.

Mwanzo errors zinakuwa nyingi sana ila usizingatie makosa we endelea kuongea, eventually utakuwa vizuri.
 
1. Jitutumekwenye kuwaza kwa kingereza
2. Ukiwa mwenyewe, jaribu kusimulia jambo lolote kwa kingereza kisha jirekebishe rekebishe
3. Tazama movies zenye sub titles
4. Ingia kwenye forums za watu wanaozungumza kingereza, kama vile Quora, jitutume kulumbana nao kwenye hoja tofauti
5. Pia tafuta forums zetu sisi Wakenya, maana sisi huchanganya lugha zote mbili, hivyo utapiga hatua
6. Tafuta dem Mkenya kwenye Whatsapp muwe mnaongea kwa kingereza, usijali hata kama kinakupa tabu, utakua sawa tu
7. Soma majarida na vitabu vya kingereza
8. Mwisho, jiboreshe kwenye kufahamu kingereza kwa usanifu, jielimishe zaidi
 
Nilifanya utafiti mdogo kwa nini wabongo wengi hawajui kuongea kiingereza hata baada ya kwenda kozi za English kama Ras Simba na kwingineko.

Nilichokuja kugundua ni kuwa;

1.Wabongo kabla ya kujifunza kingereza wanakuwa na high expectations kuwa nikienda kozi miezi mitatu tu nakuwa naongea kama mzungu(ndiyo wanavyombiwa huko wanakojifunza ila hawaambiwi Kila kitu kina level huwezi kuwa beginer unajua kuongea kama mzungu miezi 3).
katika lugha yoyote hakuna kitu kama iko kuongea kama native speakers kwa muda mfupi. Wakitoka short course wanajiona mbona hakuna mabadiliko? Wanakata tamaa.

2. kuogopa kukosea wakati wa
kujifunza.

Wazungu wakija kujifunza kiswahili wanachapia sana mwanzoni ila hawaogopi kukosea maana wanajua hii siyo mother language nipo hapa kujifunza,ila kwa mbongo iko tofauti.

3. Kuongea kiingereza kichwani kabla ya kuongea mdomoni.

Kuna muda mtu anafikiria aongeeje ili aweze kusound kama Msomi au amebobea kwenye lugha,matokeo yake anajikuta akiongea ni tofauti na vile alivyokuwa anawaza kabla hajaongea. Anajikuta anakwama wakati anaongea.

4. Kukatishwa tamaa na waswahili mtaani.

Wabongo hawapendi mtu anayeongea kingereza kabisa Huku mtaani. Ukileta mambo ya kuchanganya lugha unaonekana wa ajabu. Hii inapelekea wanaojifunza kukata tamaa maana hakuna wa kuongea nao street.

5. Kupungukiwa misamiati ya kingereza.

Lugha yoyote ile ili kuimaster vizuri lazima uwe na vocabularies za kutosha. Vinginevyo hautoboi. Hapa ndiyo linakuja swala la kusoma vitabu na kufollow acc ya wanaoongea kingereza huko mitandaoni.

Mfano Mimi mwenyewe nilikuwa sijui sherehe za uapisho zinaitwaje kwa kiingereza ila nilivyokuwa napitia zile accounts za watu wa nje wanaliokuwa wakosoaji wa Samia nikaona neno "inauguration" linajirudia sana. Kuanzia hapo nikaongeza msamiati mpya.

Kujifunza hakuna mwisho kwenye jambo lolote.

Ushauri wangu kwa mleta mada na wengine

Tafuta watu wanaoongea kingereza alafu jitahidi Kila siku uwe unaongea nao hasa usiku ukiwa umetulia,angalau nusu saa Kila siku. Utakuwa vizuri.

Kuna mdada slay queen mmoja alinitafutaga akaniomba hiki kitu niwe naongea nae kingereza ili aweze kubust confidence na kuwa vizuri kwa ujumla wakati wa kuongea na alifanikiwa. Nami nilifanikiwa pia kwenye jambo Fulani. Ikawa win win situation.
 
Hiyo post yako,andika tena chini ukini quote andika kwa kingereza hili tujue uwezo wako wa kuongea kikristo,.

A1 (Basic)
A2 (Elementary)
B1 (Intermediate)
B2 (Upper-Intermediate)
C1 (Advanced)
C2 (Proficient)

Kaka yako nimekwama kwenye C1,kila nikifanya mtihani kusogea kwenye C2 naambiwa sina vocabulary kama za Kiranga..
 
Lugha yoyote bila mazoezi ya kuiongea kila mara, lazima ita evaporate...😂
 
Hahaha, kuana huyu kijana anaitwa mtumba English, ambaye anasema watu wengi hawaongei kiingereza bali kitu kinachofana na kiingereza kwa mbali.
Mkuu, ukitaka kujua kwamba hakuna bingwa wa English nenda Scotland, Northern Ireland na Wales.

Mzee hiyo English inayozunguzwa na Native speakers wa Scotland hata akija mmarekani watashindwa kuelewana.

Ni sawa na mtu wa simiyu vijijini aje akutane na kiswahili cha wadudu wa Arusha. Kile cha oraa jomba ni gani!
 
Mkuu Mimi Bado ninajifunza kiingereza ili at least niweze kuelewana na watu wa maeneo mbalimbali jopo na kupata huduma niitakayo.
 
Mkuu Mimi Bado ninajifunza kiingereza ili at least niweze kuelewana na watu wa maeneo mbalimbali jopo na kupata huduma niitakayo.
Jambo la muhimu sana hilo mkuu.

Lugha ni kitu muhimu sana katika kuwasiliana.

Hasa English ndio lugha kuu ya Dunia.

Taarifa nyingi zipo kwa lugha ya kiingereza, na tatizo kubwa la watanzania hawataki kujifunza lugha hii na maarifa mengi yanawapita.
 
Hakika mkuu.
Ngoja niipambanie sana
 
Jifunze huu wimbo wa "Bwana Shamba had a farm, iai iai ooh" and on his farm he keeps some cows, iai iai ooh! With momoo here, and momoo there! here, moo; there moo, everywhere momoo! Bwana Shamba had a farm, iai iai ooh"

Huu wimbo ukiuimba kila siku asubuhi na jioni, ndani ya wiki mbili tu unaongea Kiingereza.
 
"Hatakama bado hujui hiyo lugha Kwa usahihi, jitahidi kusoma maneno yake na kusikiliza hata videos ili uizoee akilini mwako hatakama huelewi kinacho zungumzwa"

Ahsante sana Mkuu
 
Ningesema uje inbox ili tuwe marafiki niwe napiga ngeli tu na wewe ila Mimi mpaka nilewe ndiyo utajua kuwa Mimi ni msomi na kingereza nakijua nje ndani ila Kama sijalewa nachapia Sana Tena Sana kiasi kuwa huwa naogopa hata kumuongelesha hata mtoto wa darasa la tatu wa shule za njano

Ila nikilewa hakika utashangaa na utanitangaza mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…