Nitumie mbinu gani kujifunza kiingereza kwa urahisi

Barikiwa sana Mkuu, Ahsante
 
Dahh πŸ˜…
 
Shukrani sana mkuu, ubarikiwe
 
πŸ‘ŠπŸ‘Š
 
Anza kufanya mazoezi ya kuongea kwa kutufia unachokisikia iwe kwenye movies, music etc fanya shadowing..!

Angalia contents za kingereza kwenye social media, soma comments

Fanya hivi kila siku.. utajikuta ni kama unaishi kwenye jamii ya wanao zungumza kingereza hivyo ita speed up kujifunza kwako

Soma vitabu vya kingereza
Andika kingereza

Pia ingia YouTube usearch courses za kingereza
 
Huyo Kiranga ana balaa na ile line anayopenda kuitumia mara nyingi "non logical sequitur fallacy sijui huwa anamaanisha nini
Mkuu,

Non sequitur ni maneno ya kilatini yenye maana kuwa "Hakuna mfuatano" au "hakuna muunganiko".

Kwenye mantiki, hoja inayochomekwa bila ya kuwa na muunganiko wa kimantiki.

Kwa mfano tazama hoja hii.

1. Mama yangu ni mwanamke anayeitwa Maria.
2. Huyu aliye mbele yangu ni mwanamke anayeitwa Maria.
3. Huyu aliye mbele yangu ni Mama yangu.

Hii hoja hitimisho lake ni "non sequitur logical fallacy".

Kwa sababu hakuna muunganiko wa 2 na 3 hapo juu.

Inawezekana Mama yangu akawa Maria Nyerere, halafu huyu aliye mbele yangu akawa Maria Sarungi, wote ni Maria, lakini huyu Maria aliye mbele yangu, ni Maria Sarungi si Mama yangu Maria Nyerere.

Mfano mwingine.

1. Mimi naishi Tanzania
2. Dodoma ipo Tanzania.
3. Kwa kuwa mimi naishi Tanzania na Dodoma ipo Tanzania, basi mimi naishi Dodoma.

Hata kama 1 na 2 ni sawa, 3 si sawa, kwa sababu naweza kuwa siishi Dodoma lakini naishi Tanzania.

NB: Maria Nyerere si Mama yangu huo ni mfano nimetumia majina maarufu tu.
 
Duh! πŸ€”
 
Ahsante sana Mkuu, nakuappreciate sana endelea kutupa madini
 
Kujua tenses,Grammar na Verbs ni muhimu ili kuweza kuunda sentesi kiurahisi.

Zingatia hilo pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…