Nitumie mbinu gani kujifunza kiingereza kwa urahisi

Namna nzuri ya kujifunza ni kwanza kuwa na bidii (tena sana) Kiingereza ni kigumu na kinataka ukifanyie mazoezi hivyo anza na hiki

Kuna App ambayo unaweza kuinstall kwenye simu nyingi ni free ambazo utajifunza taratibu nashauri English Grammar Test ( Nithra) ipo Playstore

Yenyewe inakufundisha kila kipengele halafu kuna quiz baada ya hiko kipengele

Mfano ; Parts of Speech: inafafanua adjectives ni nini inatumikaje na kanuni zake kisha kuna maswali ambayo unajibu mwisho inasahihisha na kuendelea na vipengele ni vingi kuanzia Question Tags, Phrases, Prepositions etc. Zaidi ya 30 hivi vyote ukivipitia utapata kitu

2. Kusoma Vitabu ( hii ni ngumu sana kama unajifunza ila inasaidia sana kama ni Begginer lakini una uelewa mdogo wa kuanzia) kama bado kabisa iweke mwisho ila husaidia kujua namna sentesi zinavyopangwa na nyakati mbalimbali

Muhimu kuanza na vitabu rahisi (Comics, Story fupi kadri muda unavyoenda utaelekea kwenye advanced kama Novels na fiction nyingine)

3. Movies , Interviews na Media kwa ujumla
Hii ndio njia rahisi zaidi kujifunza na inakusaidia kujua matamshi

Ukiangalia movie hakikisha unaweka Subtitle na unakuu kila neno gumu ambalo wametamka na hakikisha unafuatilia kupata picha ya kinachozungumzwa (kuna muda mwengine inaweza kukupita ila ukiunganisha matukio ya kile kinachoonekana taratibu unajijenga) Tazama Interview mbalimbali za Kiingereza iwe ya wasanii, watu maarufu n.k kwenye sehemu kama youtube kuna option ya Subtitles kukusaidia kuelewa kinachozunguzwa huku unajifunza

Mwisho Tazama Chanel za Kiingereza mfano BBC na hata sikiliza redio zinazozungumza kiiingereza hii itasaidia kukupa uelewa wa masuala mtambuka na matumizi sahihi ya lugha; mfano wakati wa uchaguzi watazungumzia misamiati ya kiuchaguzi hivyo itakujenga na kukuelewesha namna sahihi ya kutumia lugha hiyo

4. Na mwisho Tafuta Rafiki wa kuzungumza nae au kuchat nae hii itakusaidia kuunda sentensi na ni muhimu kumjuza kuwa unajifunza ili akusaidie unapokosea, ukikosa tumia AI kama Chat GPT kwa kumuuliza maswali bae atakujibu hivyo unajifunza taratibu

Hiyo ni kama kujifunza, ila kama kufundishwa kuna vituo mbalimbali ambavyo vinafundisha lugha ya kiingereza na vitakusaidia kujijenga wakati unachanganya na hivyo vya juu
 
Ila wee mzee muongo
 
Tumia app inaitwa Cambly mule kuna walimu kabisa unakuwa unaongea nao kila siku kwa nusu saa au lisaa inategemeana na wewe na mudawako but ni ya kulipia
ila utakutana na walimu best sana
 

View: https://www.instagram.com/p/DQQgWAUE4HW/?igsh=YzljYTk1ODg3Zg==
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…