Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Kikohozi hadi sauti kukauka mtu anaweza kutumia nini? Achana na dawa za hospital
Katakata limao tano, changanya na vitunguu maji vitatu halafu pondaponda punje sita za vitunguu swaumu. Changanya mchanganyo huo katika lita moja ya maji na uchemshe, chuja upate mchujo safi halafu weka vijiko 15 vya asali koroga tayari kwa matumizi.Tumia vijiko 3×3
 
Katakata limao tano,changanya na vitunguu maji vitatu halafu pondaponda punje sita za vitunguu swaumu.Changanya mchanganyo huo katika lita moja ya maji na uchemshe,chuja upate mchujo safi halafu weka vijiko 15 vya asali koroga tayari kwa matumizi.Tumia vijiko 3×3
Huu mchemsho inabidi kupasha kila unapohitaji kunywa au ukichemsha mara moja inatosha
 
Je, shubiri hurudisha nguvu za kiume?
Kwa kiwango fulani huweza kuleta msisimko, maana ni aina ya lishe ambayo huchochea mzunguko wa damu. Mzunguko wa damu unapokuwa vizuri katika mwili wa binadamu, damu hufika kila mahali. Lakini inategemea na tatizo ila kwa nia ya kuboost ni mojawapo ya kiungo muhimu, vingine ni Karanga mbichi, asali, mbegu za parachichi na maboga, asali na aina yote ya vyakula vyenye madini chuma
 
Kwa kiwango fulani huweza kuleta msisimko,maana ni aina ya lishe ambayo huchochea mzunguko wa damu.Mzunguko wa damu unapokuwa vizuri katika mwili wa binadamu,damu hufika kila mahali.Lakini inategemea na tatizo ila kwa nia ya kuboost ni mojawapo ya kiungo mhimu,vingine ni Karanga mbichi,asali,mbegu za parachichi na maboga,asali,na aina yote ya vyakula vyenye madini chuma
Kuna mtu ana 1Mil akipewa dawa apone tatizo la nguvu za kiume tu! Adindishi tunafanyaje tule hela?
 
Unawezaje kutumia unga wa mjafari ni kweli unatibu nguvu za kiume na je ni sawa na vumbi la kongo (booster)au zinatibu kidogodogo
 
Naomba kujua dawa ya asili ya kutibu kilimi cjui kiswahili kingine naweza kusema vip ,hapa kwenye koromeo kimerefuka kidogo hivyo kinasababisha kukohoa sana ,nini tiba yake tofaut na kukikata
 
Back
Top Bottom