Mungu ni mwema Watanzania wenzangu maana ishara ya baraka kutoka kwake (Mvua) tunaendelea kuishuhudia, mfano hapa nilipo mimi ni tangu asubuhi mpaka sasa inaendelea kunyesha!
Watu wengi sana wanasumbuliwa na magonjwa ya uvimbe katika sehemu mbalimbali za miili yao, inaweza kuwa tumboni, kwenye utumbo, figo, mirija ya uzazi na sehemu nyingine za mwili. Asilimia kubwa hufanyiwa upasuaji ili kuondoa vimbe hizo na wengine kulingana na unyeti wa sehemu zilipo wanaendelea kuishi kwa matumaini ya kutumia vidonge vya kutuliza maumivu huku siku zikisogea,na asilimia ndogo hupata suluhisho kupitia tiba mbadala na kupona kabisa bila kufanyiwa upasuaji wowote.
Mti huu wa Nsuha (rejea katika picha) unafanya kazi hii ya kuondoa uvimbe mwilini kwa ufanisi mkubwa sana kama utazingatia uandaaji na matumizi yake, kila sehemu yake ni dawa lakini kwa mimi hapa nazungumzia mizizi yake. Mizizi yake huvunwa na kukaushwa (siyo juani) vyema ili isipoteze ubora na baadaye husagwa vizuri kwa ajili ya matumizi.
Mtu mwenye uvimbe wa aina yoyote anaweza kuitumia kwa muda wa mwezi mmoja tu akapata nafuu na kupona kabisa tatizo. Asubuhi na jioni kijiko kimoja cha chai katika maji moto ama uji. ACHA KUPUUZA NA KUDHARAU VITU.
Kuna miti mingi sana yenye uwezo wa kuondoa kabisa vimbe sugu katika mwili wa binadamu, na inaweza hata kuchanganywa miwili ama mitatu kwa ufanisi na ikatoa matokea makuu sana kwa ajili ya kujifunza tutajifunza mmoja baada ya mwingine. Usiogope kujaribu mitishamba ni hazina kubwa sana.
Mungu akubariki!
Ezekiel 47:12.
View attachment 2086499