Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Sijakuelewa una maana gani??
Wewe si unaitwa Baba Vladimir. Raisi wa Urusi si ni Vladimir Putin. Sasa kama wewe ni baba Vladimir it means mwanao ni Vladimir Putin raisi wa urusi.

Jamaa hapo anakuomba umwambie mwanao aache kugombana na Ukrane ili waafrika wakiwemo watanzania waliopo kule Ukraine waweze rejea makwao.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahaa! Najitahidi kusihi....lakini anaelekea kunielewa,maana pia ni kwa maslahi ya usalama wetu kama familia!! Kwa hiyo tumetoa masharti kama yataridhiwa bila shaka mambo yatakwenda vizuri.
 
Chimba Mizizi ya tulatula kiasi, ongeza na mizizi ya papai la kiume na uichemshe vizuri, Ongeza kidogo unga wa mizizi ya mti wa nsuha baadaye chuja maji yake. Tumia glass moja ×3.
Kwa wengine hatujui mimea kwa majina, kwa kutusaidia hebu weka picha.
 
PID (Pelvic Inflammatory Desease) Yaani maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke/ mji wa mimba.

PID huhusisha maambukizi katika mji wa mimba. Bacteria aina ya Candida hushambulia via vya uzazi vya mwanamke na kusababisha Fangasi ambayo hupelekea maambukizi zaidi katika mji wa mimba yaani PID. Hata kabla haujafika kwa daktari unaweza kujitambua mwenyewe kama umeathirika na ugonjwa huu wa PID.

1. Kama uliambiwa kuwa una UTI na umeitibu kwa dozi sahihi, mara kadhaa na kwa muda mrefu bila mafanikio, ujue kuwa umeathirika na ugonjwa huu wa PID.

2. Kama umetumia dawa za kupachika ukeni kwa lengo la kutibu Fangasi au UTI kwa muda mrefu na unapona, lakini tatizo linarudia tena kila mara, ujue kuwa umeathirika na ugonjwa huu wa PID.

3. Kama huna matatizo ya magonjwa ya zinaa, lakini unatokwa uchafu mweupe, njano, kijani ama majimaji yanayotoa harufu kali sehemu za siri, ujue kuwa una shida ya PID.

PID haiponi kwa urahisi kama wengi wanavyodhani, ni ugonjwa unaoweza kusababisha saratani ya mlango wa kizazi hasa inapofikia hatua ya kutokwa na uchafu wa kijani, maana maambukizi yanakuwa yamefikia kiwango cha juu zaidi(Severely abnormal).

PID inaweza kusababisha kutoshika ujauzito, kuziba kwa mirija ya uzazi, maumivu makali wakati wa tendo yanayoambatana na kutokwa damu na miwasho sehemu za ukeni.

Bakteria wanaosababisha PID huweza kumwingia pia mwanaume kupitia njia ya kujamiana na kumsababishia dhahama kubwa. Mwanaume anaweza kutokwa na uchafu kwenye mrija wa uume na wakati mwingine maumivu makali ndani ya mrija.Mara nyingi unapokwenda kuchukua vipimo majibu huwa ni UTI, lakini kila unapotumia dozi unaweza kuhisi nafuu na baadaye tatizo huendelea.

Ili kujitibu tatizo hili kwa urahisi na kuweza kupona kabisa, unashauriwa kujitibu wewe na mwenza wako kwa pamoja ili kuepusha maambukizi mapya ya Bakteria, wengi wanahangaika na shida hii kwa muda mrefu sana bila kugundua na wanazidi kumeza antibiotics kila mara bila mafanikio.

Unaweza pia kutumia mitishamba inayoweza kuua kabisa bakteria hawa na ukapona kabisa tatizo hili.

Chimba Mizizi ya tulatula kiasi, ongeza na mizizi ya papai la kiume na uichemshe vizuri, Ongeza kidogo unga wa mizizi ya mti wa nsuha baadaye chuja maji yake. Tumia glass moja ×3.

Unaweza kuhisi nafuu ndani ya masaa 24, lakini unakiwa kufanya hivi kwa wiki 2 au 4 mfululizo kutegemeana na ukomavu wa ugonjwa.

Mungu akubariki sana!
Duh,kwenye tiba ss ndo najanga,mpapai dume? Ndo ukoje huo jmn?
 
Watu wa tiba mbadala mna tatizo moja, utaelezea ugonjwa vizuri sana, utatoa ushauli vizuri tu na utataja dawa kwa umakini ikifuatiqa na kutaja mmoja ya mmea utakaokuwa unaufaham wewe mwenyewe, nini maana yake?.

Hutaki kuondoka patupu, yaani unataka lazima utafutwe ili upige mapato.
Yaani shida sn
 
Si hivyo ndugu yangu,mimea hiyo inafahamika popote unaweza kujitengenezea,ula kama huwezi ndipo unaweza kupata msaada wa kuandaliwa ambao lazima utahusisha gharama.
Kwa mfano mi hapo hakuna hata mmea mmoja naufahamu hapo!
Na sijawahi kusikia papai dume[emoji848]
Au ndo ile mipapai isiyozaa?
 
Watu wa tiba mbadala mna tatizo moja, utaelezea ugonjwa vizuri sana, utatoa ushauli vizuri tu na utataja dawa kwa umakini ikifuatiqa na kutaja mmoja ya mmea utakaokuwa unaufaham wewe mwenyewe, nini maana yake?.

Hutaki kuondoka patupu, yaani unataka lazima utafutwe ili upige mapato.
Ungekuwa wew ungetaja chimbo la almasi au lawama kama kawaida yetu wabonho tukiongozwa na bashite
 
Back
Top Bottom