Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Yes!
Tiba haikuwa sahihi!


Sent using Jamii Forums mobile app
Hili si tatizo dogo kama ambavyo baadhi hufikiria! Na ndio maana linaendelea kuwatesa huku wakiendelea na tiba bila mafanikio.

Hata katika mitishamba,lazima upate mchanganyo sahihi sana na utumie kwa juhudi kubwa na kwa muda unaotakiwa.Tatizo hili hupona kabisa na kutojirudia tena.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Tiba ya uhakika hii hapa, mpigie huyo utaipata atakuelekeza pa kuipata

322DC74E-1343-424E-94B8-CB602641699E.jpeg
 
Nawa tu ivi usiku ntalala kweli au ntakuwa nageuka geuka kitandan
 
Mimi nasumbuliwa na misuri kwenye nyonga na cha ajabu maumivu yanaama ama mara mguu wa kulia ukiacha unakuja mguu wa kushoto. Na wakati mwingine kinakuja kama kichomi kinabana kwenye paja. Nikinywa kitu cha moto sana maumivu yanapungua. Nahitaji msaada mwenye utaalamu
 
Hapa kwenye UTI ni suala la uelewa pia.Unaweza kufikiri ni muathiriko kwenye njia ya mkojo tu,kumbe ugonjwa umeshapiga hatua mbele.Mfano wanawake wengi hupata maambukizi katika njia zao za mkojo,lakini maambukizi hayo hupelekea kupata fangasi sugu inayoweza kusababisha hata maambukizi katika mji wa mimba (PID),sasa mara nyingi wanapopima katika maabara hizi za kawaida huonwa na bakteria katika mkojo lakini secondary problem iliyoletelezwa na hao bakteria huwa haionekani kirahisi.Wanaume hubeba bakteria hao kwa njia ya kujamiana na inakuwa kama magonjwa ya zinaa na dalili ni zilezile endapo ugonjwa utakomaa,utawashwa kwenye mshipa wa uume,utatokwa uchafu mweupe na wakati mwingine utapata shida ya kukojoa huku homa kali na unyonge vikikuandama.Kwa wanawake suala linapofika hatua kubwa uchafu utaanza kutoka sehemu za siri na utaambatana na harufu mbaya,na inaweza kupelekea uchafu kuwa wa kijani alert ambayo ni mbaya zaidi kuna uwezekano wa kansa.

Kama mtu yuko kwenye ndoa na ana tatizo hili ambalo sasa imezoeleka ni UTI lazima mme na mke watumie dozi wote vinginevyo ni kujitapelivmwenyewe. Zipo dawa za mitishamba ambazo husafisha kabisa matatizo haya.
Zitaje hizo dawa za mitishamba
 
Dawa za asili kibao hatujazifanyia utafiti.

Mimea na matunda kibao hatujui kwzi yake lakini tunakimbilia antibiotics ambazo sife effects zake ni kiboko kuliko faida zake
 
Mkuu Mshana Jr. Bado Tuko kwenye Oktava ya Mwaka mpya 2022. Happy New yr.[emoji1787] aithee.
Huo mti uliooneshwa hapo kwenye picha wenye maua makubwa mekundu SIO Mjafari.
Mjafari huku Umasaini ni mingi sana na Unaitwa Oloisuki. Baadhi ya makabila wanauita Mlungulunguani, Wahehe wanauita Mkhunungu. Unamatumizi-dawa mengi sana. Majani yake machanga huweza kutumika kama mboga(Mlenda). Matunda yake yaliyokomaa yanafanana sana na pilipili manga. Hukaushwa na kusagwa na hutumika kama Tangawizi kwenye chai- hutibu matatizo ya kifua kinachobana. Mizizi yake iliyokaushwa na kusagwa hutumika kutibu maumivu ya viungo/mifupa ikiwepo arthritis, mgongo, kiuno n.k. n.k.
Mti huo picha yake ni hii hapa:
Angalia maua yake yalivyo ni tofauti na yale mekundu katika picha iliyooneshwa. Picha (Mti) uliyooneshwa wenye maua makubwa mekundu huku Umasaini tunauita mti huo Olng'aroji.

View attachment 2071796

View attachment 2071800

View attachment 2071807
Huu ndiyo wenye harufu kama machungwa ?
 
Dawa gani asili ya bawasiri
Tafuta dawa inyaitwa mbegu za habati sauda.. ni nyeusi hivi tii
chukua mkaa uweke kwenye tezo kama tunavyofanyaga kwenye kusoma dua..
weka hizo mbegu kwenye mkaa wa moto uliopo kwenye tezo...
jifukize kwenye sehemu yenye bawasiri probably ni sehemu ya haja kubwa so utafanya kama unakalia ili moshi upige hiyo sehemu yenye bawasiri..
fanya hivo kwa siku saba... halafu uje ulete mrejesho ili nawenye tatizo wengine waweze kupona....

kama hujaelewa matumizi pia uliza ntakujibu
 
Jambo watanzania wenzangu!!

Katika kubadilishana maarifa ninaomba kuulizwa chochote juu ya dawa asili za mimea na mitishamba katika kutibu magonjwa mbalimbali.

NB:Maswali hayo yasihusishe ramli na mambo ya kishirikina,ama mambo dhahania,maswali yajielekeze katika magonjwa ya kila siku ambayo tunaishi nayo na yanatusumbua.
Ili Kuitengeneza Dawa kutoka Kuwa ya Unga na kwenda Kuwa Ya Maji unatakiwa uwe na Vitu gani na gani Vya kuchanganya ????
 
Dawa ya kusafisha mishipa ya damu unayo?? Yani mishipa huenda imeziba inahitaji kuzibuka.
 
Dawa ya kusafisha mishipa ya damu unayo?? Yani mishipa huenda imeziba inahitaji kuzibuka.
Mishipa ya damu huziba kwa sababu ya lehemu inayotokana na matumizi ya vyakula vya mafuta kupita kiasi,hivyo kusababisha madhara makubwa katika mzunguko wa damu.Dawa ipo na inaweza kusafisha kabisa na kuondoa lehemu yote ama mafutamafuta katika mishipa ya dama na kuifanya damu kuwa nyepesi kufikia kila sehemu ya mwili kwa wakati.
 
Mishipa ya damu huziba kwa sababu ya lehemu inayotokana na matumizi ya vyakula vya mafuta kupita kiasi,hivyo kusababisha madhara makubwa katika mzunguko wa damu.Dawa ipo na inaweza kusafisha kabisa na kuondoa lehemu yote ama mafutamafuta katika mishipa ya dama na kuifanya damu kuwa nyepesi kufikia kila sehemu ya mwili kwa wakati.

Inapatika wapi iyo dawa mkuu?
 
Back
Top Bottom