Mkuu Mshana Jr. Bado Tuko kwenye Oktava ya Mwaka mpya 2022. Happy New yr.[emoji1787] aithee.
Huo mti uliooneshwa hapo kwenye picha wenye maua makubwa mekundu SIO Mjafari.
Mjafari huku Umasaini ni mingi sana na Unaitwa Oloisuki. Baadhi ya makabila wanauita Mlungulunguani, Wahehe wanauita Mkhunungu. Unamatumizi-dawa mengi sana. Majani yake machanga huweza kutumika kama mboga(Mlenda). Matunda yake yaliyokomaa yanafanana sana na pilipili manga. Hukaushwa na kusagwa na hutumika kama
Tangawizi kwenye chai- hutibu matatizo ya kifua kinachobana. Mizizi yake iliyokaushwa na kusagwa hutumika kutibu maumivu ya viungo/mifupa ikiwepo arthritis, mgongo, kiuno n.k. n.k.
Mti huo picha yake ni hii hapa:
Angalia maua yake yalivyo ni tofauti na yale mekundu katika picha iliyooneshwa. Picha (Mti) uliyooneshwa wenye maua makubwa mekundu huku Umasaini tunauita mti huo
Olng'aroji.
View attachment 2071796
View attachment 2071800
View attachment 2071807