Mafundi wa kitanzania wababaishaji sana nilimuuliza fundi mbona hubadilishi akaniambia hapa Tanzania hakuna.
Aisee pole...ndiyo mafundi wetu hao...
Lakini inashauriwa kwa dunia ya sasa fundi namba moja wa gari lako ni wewe mwenyewe....
Tumia smartphone yako kugoogle info mbali mbali za gari lako pia You tube kuna masomo mazuri sana....ukishapata idea fundi gonga nyundo hatakubabaisha...
Hawa mafundi wetu smart phones zao ni kwa ajili ya kubet, kuangalizia matokeo ya mechi za Yanga na kuangalia picha za mademu wazuri...bhaasss...hawatumii smartphone kujiendeleza kimaarifa kulingana na dunia inavyokwenda....
Most of them wanatumia akili kubwa pale wanapovuka bara bara bhaasss...
Hawataki kutumia akili kubwa kwenye changamoto mpya wanazokutana nazo..
Na ukitaka kuhakikisha kuwa mafundi wetu hawapendi kujishughulisha, we jifanye unamuomba ushauri wa ununuzi wa gari.... ataropoka tu TOYOTA... sababu zake za msingi zitaegemea kuwa ndiyo zinatengenezeka na spea ni bei rahisi....lakini kimsingi hakuna gari lisilotengenezeka endapo utaamua kulifuatilia teknolojia yake na mifumo yake...
Wajapani wanaweka thermal start, mafundi wetu wanazitoa....hatari sana....
Sasa tumefika mahali mafundi wetu wajiongeze, kwa sababu hata hizo TOYOTA walizozoea kuzichokonoa leo hii zinakuja na teknolojia ya juu zaidi, umeme mwangi n.k......ndiyo maana hawakawii kukuambia usinunue TOYOTA yenye engine ya D4
Sent using
Jamii Forums mobile app