Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Mafundi wa kitanzania wababaishaji sana nilimuuliza fundi mbona hubadilishi akaniambia hapa Tanzania hakuna.
Aisee pole...ndiyo mafundi wetu hao...
Lakini inashauriwa kwa dunia ya sasa fundi namba moja wa gari lako ni wewe mwenyewe....

Tumia smartphone yako kugoogle info mbali mbali za gari lako pia You tube kuna masomo mazuri sana....ukishapata idea fundi gonga nyundo hatakubabaisha...

Hawa mafundi wetu smart phones zao ni kwa ajili ya kubet, kuangalizia matokeo ya mechi za Yanga na kuangalia picha za mademu wazuri...bhaasss...hawatumii smartphone kujiendeleza kimaarifa kulingana na dunia inavyokwenda....

Most of them wanatumia akili kubwa pale wanapovuka bara bara bhaasss...

Hawataki kutumia akili kubwa kwenye changamoto mpya wanazokutana nazo..

Na ukitaka kuhakikisha kuwa mafundi wetu hawapendi kujishughulisha, we jifanye unamuomba ushauri wa ununuzi wa gari.... ataropoka tu TOYOTA... sababu zake za msingi zitaegemea kuwa ndiyo zinatengenezeka na spea ni bei rahisi....lakini kimsingi hakuna gari lisilotengenezeka endapo utaamua kulifuatilia teknolojia yake na mifumo yake...
Wajapani wanaweka thermal start, mafundi wetu wanazitoa....hatari sana....

Sasa tumefika mahali mafundi wetu wajiongeze, kwa sababu hata hizo TOYOTA walizozoea kuzichokonoa leo hii zinakuja na teknolojia ya juu zaidi, umeme mwangi n.k......ndiyo maana hawakawii kukuambia usinunue TOYOTA yenye engine ya D4

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina gari aina Toyata Rav4 na ina tatizo la kunya sana mafuta na pia haikai silence ,,yaani uwe unakanyagia mafuta tu mda wote, ukiachia tu inazima .. Msaada pls

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina gari aina Toyata Rav4 na ina tatizo la kunya sana mafuta na pia haikai silence ,,yaani uwe unakanyagia mafuta tu mda wote, ukiachia tu inazima .. Msaada pls

Sent using Jamii Forums mobile app
Hi swali nilshalijibu huko nyuma; kuna mambo mengi yanayoweza kusababisha hali hiyo. soma post hii
 
Nataka kununua Verosa used kwa mtu, Sina ufahamu wowote kuhusu hizi gari hebu nijuze japo kiufupi mawili matatu juu ya hizi gari. Kwamba ninunue au niachane nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ununuzi wa gari yoyote used ni kama kucheza pata potea; kama huna uzoefu na magari, tafuta mtu anayeyajua akukagulie gari hilo kabla hujaingia mkataba wa kulinunua. Jina la gari siyo jambo la muhimu sana ila namna gari lilivyotumika na kutunzwa kabla ya mwenye nalo kuamua kuliuza.

wajua magari wana namna ya kuyakagua na kupitia ukaguzi huo anaweza pia kukusadia kukadiria thamani halisi ya gari wakati wa manunuzi
 
Ununuzi wa gari yoyote used ni kama kucheza pata potea; kama huna uzoefu na magari, tafuta mtu anayeyajua akukagulie gari hilo kabla hujaingia mkataba wa kulinunua. Jina la gari siyo jambo la muhimu sana ila namna gari lilivyotumika na kutunzwa kabla ya mwenye nalo kuamua kuliuza. wajua magarai wana namna ya kuyakagua na kupitia ukaguzi huo anaweza pia kukusadia kukadiria thamani halisi ya gari wakati wa manunuzi
Ni vitu gani haswa vya msingi kuvikagua mkuu ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vitu gani haswa vya msingi kuvikagua mkuu ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukaguzi wa gari kitaalamu ni process ndefu kidogo. Kwa jibu la haraka haraka ni kuwa kwanza angalia body yenyewe kama haijachoka kwa macho tu; yaani haijapakwa rangi juu ya putty (bondo); kuna chombo cha kuangalia kama gari ilishagongwa ikanyooshwa body kwa kupigwa putty, lakini hayo unaweza kuyaona kwa macho tu.

Baada ya hapo tafuta mtu anayejua magari akukaguria (a) Steering system, isjekuwa steering inayumbayumba imepinda, (b) Suspension system: asiangalie shock absorber na sping tu, bali aangalia hasa zile control arms ambazo nzdio uhai mkuu wa suspension yenyewe, (c) Transmission System, yaani kama kweli gari linabadili gia kiulaini, siyo gia za kugota, halafu mwisho (d) injini yenyewe kama bado ina nguvu zake;

hapo kuna vitu vingi ambavyo fundi atapenda kuvikagua ikiwa ni pamoja na cylinder pressure kama piston rings hazijaisha, fuel pressure kama fuele pump na fuele regulator zinafany kazi, emissions kuona kama sensors na injaector zote zinafanya kazi. kama fundi wako ana mitambo mizito anaweza pia kukupimia nguvu za injini ingawa siyo lazima.
 
Kwa nini wewe usingekaa kimya kama huwezi msaidia toa jibu.huoni ingekuwa heshima zaidi? Maana yeye amejibu ila wewe umetia kiherehere .angalia si nzuri sana hiyo tabia.mambo ya ngoswe mwachie ngoswe.

Ungekaa tu kimya kama ulikuwa huwezi kumsaidia muuliza swali...ingekuwa heshima zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom